Uongozi wa Chama Kipya Ukiingia; CCM kifutwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi wa Chama Kipya Ukiingia; CCM kifutwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 10, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tunisia wamekifuta kilichokuwa chama chao tawala ili nchi nzima ianze upya; nadhani serikali ya chama kingine itakapokuja kushika madaraka itabidi suala la usajili wa CCM liangaliwe upya. Hii ikiwemo uwezekano wa kukifuta ili mashabiki wake na wanachama wake waanzishe chama kipya kabisa.

  Naamini kosa kubwa alilolifanya Nyerere wakati wa kurudisha vyama vingi ni kuiacha CCM kama de fact ruling party na hivyo hawakutakiwa kuanza moja. Nadhani itapaswa waanze moja kabisa kwa chama hicho kufutwa.
   
 2. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri hilo lkn haliwezekani kwa CCM maana ni kijiwe chao cha kuchumia, mafisadi ndio wanamokimbilia maana kuna ulinzi na kipindi cha uchaguzi kikifika wanalipa fadhila kwa kulindwa.
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi CCM hawafanyi kazi kama chama cha siasa, wanafanya kazi kama mhimili wa dola. Kwa tabia hiyo siku Chama kingine kikichukua nchi CCM itakufa yenyewe, viongozi wake wengi ni watu wasio kuwa na pa kushika zaidi ya kutegemea kuchukua posho za vikao na kufanya ufisadi ili waendeshe maisha.

  Kadri ruzuku inavyopungua ndio na chama kinapokosa nguvu ya kiuchumi na waroho wa madaraka kukikimbia. Tujipange vizuri wananchi tuwe tayari kukitimua chama hiki kwa nguvu zetu wenyewe kwani hali ya maisha inazidi kuwa mbaya kila kukicha!
   
 4. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM sio Chama bali ni genge la wahuni au ma-criminal yanayoiba mali za watanzania, likiongozwa na Fisadi papa Kikwete. Hiki chama inabidi kifutwe ili Watanzania tuwe na amani na utulivu.
   
 5. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete + Makamba + Mkapa x CCM + AU (African Union) = Criminal :wink2:
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,162
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwa dhana hiyo si CCM tu bali vyama vyote vifutwe kwani vyama vyote hivi vilianzishwa na Serikali na vilianzia Ikulu.
   
 7. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hili nadhani kweli ni kosa lililofanywa, tena hasa pale ambapo mali na uchumi uliojengwa na wananchi wote katika mfumo wa chama kimoja haukurudishwa serikalini au kugawanywa kwa usawa katika kila chama ambacho kingeanzishwa. Kwa sasa tunashuhudia CCM ikiwa inamiliki maeneo makubwa katika karibu kila kata lakini chimbuko haswa si uwezo wa CCM kama chama bali hali ya mfumo wa chama kimoja iliyosukuma hivyo.

  Nadhani mjadala mpana hususan katika mali na vitega uchumi CCM inayo sasa unapaswa uangaliwe upya hivyo aidha virudishwe serikalini na kuwa vitega uchumi vya serikali au vigawanywe kwa kila chama cha siasa.

  Kulipaswa kutoa mazingira sawa na mapana ya vyama vyote kukua
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hiyo itakuwa ngumu. Itawezekana tu kama utafuta dola za serikali ikiwemo na usalama wa taifa. Maana unaposema CCM, ujue ina-affiliations zake (mfano. Dola, Ufisadi, umaskini wa mali na elimu kwa wananchi nk.) ambazo zipo kuhakikisha wanaendelea kufyonza.
   
 9. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kitakufa natural death....,sasa hivi kipo ICU.
   
 10. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuna ukweli kwenye hilo.

  Italeta changamoto kubwa, na kupata watu wenye uchungu na nchi na wala sio wanaotafuta umaarufu na chakula tu kama ilivyo sasa
   
 11. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM imekuwa ni sehemu ya Dola kiasi kuwa ni vigumu kufikiria kuwepo kwe CCM isiyokuwa na dola. Vyama vyote vya aina ya CCM, baada ya kupoteza madaraka vimejikuta katika hali isiyoeleweka na kusema kweli havijengeki tena. Nakubaliana na aliyesema kuwa CCM itakapoondoka madarakani haitahitaji kufutwa, kitakuwa tayari kimefutwa kwa kuondolewa madarakani.

  Angalia fate ya KANU ya Kenyatta kule kenya, UNIP ya kaunda kule Zambia, UPC ya Obotte kule Uganda, Rwanda, Burundi na hata Congo. Ok baadhi ya nchi kama Uganda, Congo na Rwanda vyama tawala vya uhuru viliondolewa na mapambano ya vita. Lakini nchi zilizofanya uchaguzi na kuving'oa vyama tawala vya uhuru kwa kutumia kula kama Kenya, Zambia na Malawi vyama hivyo havioneshi kuwa vitakuja kuinuka tena. Tanzania CCM inavyoelekea itaondolewa kwa uchaguzi (kama si 2015 basi 2020) kama ilivyofanyika Malawi, Zambia na Kenya. Uchambuzi wa kilichotokea kwa hao majirani wote unaonesha kuwa siku ikiondolewa madarakani CCM, utakuwa ndo mwisho wake.

  Ndiyo maana wako tayari kufanya chochote ku 'hang' on power ikiwa hata kulazimisha serikali ya umoja wa kitaifa. Watu wa CCM haya ninayoyaandika hapa wanayajua, ingawa mahali chama kilipokwisha kufikia hakirekebishiki tena na kushindwa kwenye uchaguzi ni jambo ambalo halizuiliki. Ni ama CCM ikubali kushindwa, iondoke madarakani na ife au ing'ang'anie madarakani nchi iingie kwenye matatizo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe tuishie kama ilipo Somalia! Hakuna kitu cha kati katika haya mawili!

  Mwenendo wa CCM katika siku za hivi karibuni unaonesha kuwa wako tayari kung'ang'ania madarakani na nchi iingie kwenye machafuko, kwani watatupia lawama kwa wale wanaotaka kuwang'oa madarakani! Inaonekana wana mawazo kama Ghadafi kuwa walibya wanampenda mno na wanaompinga ni wabwia unga na mawakala wa al-qaeda. CCM nao wanaonekana kuamini kuwa watanzania wanaipenda mno CCM na wanaoipinga CCM ni waleta vurugu na fujo kwa hiyo CCM iko tayari kutumia nguvu zote kupambana nao! Hayo kwa haraka haraka yanaonekana kuwa ni mawazo miongoni mwa viongozi wengi wa CCM.

  Sasa hali ikiwa hivyo tujiandae. CCM hairekebishiki tena. Kufa kitakufa tu. Suala ni kitakufaje? Ni ama Kitakufa na nchi yote (pale kitakapokataa kutoka madarakani baada ya kushindwa kihalali) au kitakufa chenyewe pale kitakapokubali kuondoka madarakani. Kukataa kuondoka madarakani kwa CCM ni pamoja na kuzuia uwezekano wowote wa kuwa na uchaguzi huru na haki, ili kiendelee ku chakachua matokeo ya chaguzi zote zitakazofanyika. Na iwapo kutakuwa na uchaguzi ulio huru na haki, itakuwa ndo uchaguzi wa mwisho kwa CCM!
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mbona hata wao wenyewe walishahisi hivyo! Zile mali za serikali zilizotaifishwa na CCM si tayari wamejiuzia wenyewe karibu zote!
  Mwanzo wa kufa CCM ni wakati hizo mali wanazoita zao zitakapokwisha!
   
 13. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM ni sehemu ya dola kwani viongozi wengi wa CCM ni mawakala wa vyombo vya usalama (hasa usalama wa Taifa). Huwezi kutenganisha CCM na Dola halafu ukasema CCM ipo! Hayo ndo matatizo ya muundo wa vyama vilivyokulia kwenye mfumo wa chama kimoja au Chama dola. Kimuundo na kiutendaji chama kinabaki kuwa sehemu ya dola. Kuondoa dola mikononi mwa chama ni kuondoa chama!

  Ni vigumu kurekebisha huo muundo kwani ili kufanya hivyo itakuwa ni kama kufanya mapinduzi. Hakuna anayefanyaga mapinduzi ya kujipindua mwenyewe! Hivyo CCM haiwezi kujirekebisha!!
   
 14. MFUKUZI

  MFUKUZI JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ni kweli naungana na wewe Mwanakijiji, maana haiwezekani mali zote za CCM (viwanja, majengo na nyumba za kuishi) zilijengwa kwa nguvu za watanzania wote. nakumbuka hata sisi tulisomba mawe kujenga viwanja vya michezo leo CCM imehodhi vyote. CCM lazima ifutwe au mali zake zitaifishwe kianze upya kama vyama vingine vilivyoanza
   
 15. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :hand:

  Kwa mtazamo wangu kisifutwe ila tukinyang'anye miundombinu yote tuliyoijenga kwa nguvu zetu watanzania ikiwamo viwanja vya michezo, majengo mengi w3aliyonayo katika mikoa na wilaya

  Kwa kufanya hivi kitafutika chenyewe maana wanaoishi ndani ya CCM hawaishi kwa sababu ya ITIKADI na FALSAFA ya chama bali UKWASI
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  alifanya hivyo makusudi?
   
 17. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,525
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Na pia vyama vyote vimedesa hata set up ya CCM. i.e Muundo na uongozi
   
 18. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri, CCM ifutwe baada ya cdm kuchukua nchi
   
 19. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  ... if wishes were horses, ...!!!
   
 20. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  This is exactly what is wrong with Africa. Mkifute ili nini? Kinachotakiwa nikwaonyesha jinsi yakuendesha serikali ili wawe opposition wajifunze. Dejure and De facto lazima watakuwa the main opposition party in the short to medium term. How can you have an adversarial system of government bila kuwa na opposition. Itakuwa one CCM for one CDM. Wataiba tuu... Its a fact kwasababu ndio watanzania wenyewe sisi. Lazima kuwa na balance of power. Tusifanya makosa ya kufikiri kuwa kuna chama fulani ambacho kimetumwa na Mungu or something. Wote hawa wanasiasa ama angalau wengi wao ni wale wale.
   
Loading...