Uongozi uhitaji busara sana, si kila mtu anaweza kuwa RAIS

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Kuna mijadala isiyo na mwisho. Kwamba kiongozi uzaliwa au utengenezwa. Mimi naamini katika vyote, uzaliwe ukiwa na hiyo trait ya uongozi, kisha utengenezwe. Lakini hilo siyo lengo la mada hii.

Kila kiongozi ana maoungufu yake, mimi si muumini wa Kikwete kabisa. Lakini kila kiongozi hakosi strength yake. Nakumbuka nyakati fulani Kikwete alikuwa akisema "kuna viongozi wenzangu wananiambia tupige marufuku mikutano ya upinzani, lakini mimi nawaambia hapana, acha waongee watoe gubu"

Nimejaribu kufikiria maneno hayo na sasa. Unapokuwa kiongozi mahali popote pale hata kama ni kwenye shirika, hakikisha unakuwa tofauti na watu wenye rank za kawaida. Ndani ya CCM wako watu wamepewa madaraka makubwa lakini ukweli hawana uwezo wa kuongoza, wamefika hapo kwa sababu wana uwezo mkubwa wa kujipendekeza kwa wakubwa, au ni washabiki wakubwa wa vyama.

Akili ndogo wakibahatisha kupata madaraka huwa hawajiamini, watahakikisha wanapambana na yeyote anaetishia kuchukua nafasi zao, hata ofisi za kawaida za serikali akili ndogo huwa wapo, wakiona kuna mtu mjanja ameletwa wata hakikisha wanamfanyia fitna ili aondoke, ikibidi wataenda hadi kwa waganga wa tunguli.

Watu hao ambao akili zao ni ndogo ni rahisi kupenyeza fikra zao za chuki kwa mkuu wa nchi.

Ukiwa kiongozi wa nchi unatakiwa ujivue ushabiki wa vyama uliopitiliza, usiwe na ukada uliopitiliza maana wewe ndie kiongozi wa wote, akili yako inabidi ifukirie zaidi changamoto za watu wako, ukiweza kuzitatua wala uhitaji kuangaika na kelele za wapinzani.

Sasa ukiwa siyo mjanja kama Kikwete wataanza kukuambia, ebu tuzuie mikutano ya upinzani, utakubali. Watakuambia tena, mpinzani akipinga serikali afunguliwe kesi, utakubali, tuzuie bunge live ili wasisikike, utakubali. Ukishakubali yote hayo hawa akili ndogo wataanza ku advance kidogo, watateka mpinzani wa kwanza na kumuachia halafu watasubiri wakuone utasema nini, ukikaa kimya watakwenda next level, watapiga risasi na kujeruhi mpinzani, ukikaa kimya watakwenda level nyingine, watateka na kuua kisha kutupa baharini bila kujua kumbe mawimbi hurudisha miili iliyokufa, ukikaa kimya watajua sasa ndiyo wakati sahihi wa kuua wapinzani. Wewe kama kiongozi ukiendelea kutizama, iko siku watafanya tukio kubwa ambalo watakuaibisha hata wewe na kukuchafua, mfano mauwaji ya Akwilina, lakini wakifika level hiyo maana yake na wewe umeruhusu ingawa katika mipango yao hawakushirikishi. Hii hali itaendelea na kujikuta umeweka historia ya kuwa kiongozi mkatili, pia unaweza kuondoka madarakani kwa aibu kubwa sana.

Kizazi na kizazi kitaisoma historia yako ya ukatili hata hakuna mtu mmoja atatamani kutizama kabuli lako
 
Kweli, sasa hivi ni kama tuna dubwasha tu lenye mwili pasi na kichwa, linatuongoza!
 
Back
Top Bottom