Kwa muda mrefu kumekuwa na hoja kutoka kwa wana CCM kwamba kwa nini Mbowe amekuwa mwenyekiti kwa muda mrefu kama kwamba ni mfalme na kwa nini hataki kupisha watu wengine wakiongoze chama hicho.
Je, CCM wanakitakia mema Chadema? Jibu ni wazi ni hapana. Wanafanya hivyo ili kukiondolea Chadema uongozi wenye uzoevu chini ya Mbowe. Mambo yafuatayo yameongeza shida katika chama tawala—ruzuku ya chama tawala imepungua baada ya Chadema kuongeza viti vingi bungeni na katika mabaraza ya serikali za mtaa kufikia hata baadhi ya maeneo nyeti na mikoa mikubwa, kuwa chini ya upinzania, mathalani, Jiji kubwa la kibiashara—Dar es Saalam na majiji ya Mbeya, Arusha, na manispaa za Moshi na Bukoba. Hapa lazima Mbowe apingwe na aonekane king’ang’anizi ndio maana wanamfananisha na mfalme. Nia ni kuwafanya wana Chadema wamwone hafai wamtupe chini, ili iwe rahisi kwa cha tawala kurejesha ufalme wake.
Mbowe ni kiongozi mwenye misimamo usioyumba—hasa kwa nafasi yake kama Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni. Hili nalo nikikwazo kikubwa kwa chama tawala. Wanafikiri kwamba kuwa na mtu imara na jasiri kama Mbowe, kutaendeleza msuguano mkubwa kutoka kambi ya upinzani na kwa jinsi upinzani unavyosimama kwa umoja, imekuwa vigumu sana kuwagawa chini ya uongozi wa Mbowe. Kuondoka kwa baadhi ya Wabunge kutoka Chadema ni mbinu moja wapo ya kumdhoofisha Mboye kisiasa.
Mbowe amekuwa kiungo muhimu sana katika umoja wa Katiba ya wananchi ( Ukawa), pamoja na baadhi ya wenyeviti wenza kuchechemea, yeye ameendelea kusimama imara, hivyo kwa vyovyote ni mtu asiyetakiwa na chama tawala—maanan ni sehemu ya kikwazo cha maslai ya chama tawala
Mbowe ni mjuvi wa siasa za majukwaani, ni miongoni mwa wanasiasa wachache sana hapa nchini, wanaojua kujenga hoja mujarabu wawapo jukwaani, ni mzungumzaji mzuri sana, hivyo kumzima kwakupiga kelele kuwa hafai, ni ndio kiwango cha uzito wake katika kujenga hoja na ni mwiba kwa CCM. Inabidi aondolewe katika majukwaa ya kisiasa kwa namana yoyote ile. Kuhamahama kwa wanachama hasa kutoka Jimbo la Hai analoliwakilisha bungeni, wanachama wa Chama cha Mapinduzi wanamnyooshea vidole Mbowe kwamba ndiye chanzo cha wanachama kikimbia Chadema.
Lakini pia ni jambo la kujiuliza toka lini CCM kiliamua kupigia kelele uwenyeviti wa Augustine Mrema wa TLP, John Cheyo wa UDP na akina Dovutwa, Prof Lipumba na wengine wa aina hiyo. Jibu,ulalo kichwani mwako. Akili za kuambiwa changanya na zako.
Kama magufuli alivyosema watatawala milele tanzania [emoji1241] basi ni lazima police watumike kuinyanyasa chadema kinyume na sheria na kuhakikisha mbowe anachafuliwa kwa namna yoyote ile
Mbowe ametafutwa sana kwenye biashara zake ili tu wampate na kosa lakini hawajafanikiwa sasa wanatumia mbinu ileile ya kumzushia kuhusika katika kifo cha wangwe na sasa wanayatumia ipasavyo magazeti ya tanzanite, uhuru na jamvi la habari kumuhusisha tena na kupigwa risasi Tundu lisu
Bahati mbaya kwao lisu yuko hai na anazipinga hoja zao kwa mbowe kikamilifu
hii Hama Hama pia inahusika kwa lengo lile lile la kumchafua mbowe
Mbowe kama mbowe ana mapungufu yake kama binadamu lakini cha kushangaza toka ccm ikabiliwe na upinzani mkali wa Chadema na vyama kuungana ccm ni kumtukana mbowe pamoja na Chadema
Sote tunajua wakati Nccr mageuzi ikiwa juu nini walizushiwa
Sote tunajua wakati Cuf ikiwa juu nini ilizushiwa
Na sasa chadema inatafutwa vilevile ila tofauti ni kwamba wamekumbana na mwamba Mbowe ambaye anazijua mbinu zao zote
Mwaka 2004 nilikuwa ccm kindakindaki lakini mtu mmoja tu aliibadilisha akili yangu mwaka uliofuatia 2005 naye si mwingine ni Freeman Mbowe kiongozi shupavu barani Africa
Tuendelee kumuunga mkono
Anayefikiri kutumia tume ya uchaguzi, police, magereza, mahakama ataiua Chadema anajisumbua sana