Uongozi CHADEMA,mmejiandaa kwa hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi CHADEMA,mmejiandaa kwa hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makamuzi, Nov 21, 2011.

 1. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Nimekuwa muumini wa demokrasia makini itakayoleta mabadiliko nchini.Nimeamua kutoa uchambuzi kidogo ambao unaweza kukisaidia CDM kiweze kuungwa mkono na watu wa visiwan Zanzibar.
  Kwanza kutokana na kuwa Zanzibar kuna mfumo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa unaohusu Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Wananchi CUF,hii inaashiria kupungua kwa upinzani na kwa maana nyingine naweza kusema there is no strong opposition political party in Zanzibar.
  Pili nlifuatilia siku maoni ya mchakato wa katiba nkagundua kuwa vijana wengi na wananchi kwa ujumla hawataki muungano na hata kama wanahitaji wanataka Muungano unaohusu serikali tatu yaani Tanganyika,Zanzibar na Serikali ndogo ya Muungano.Hii imekuwa ajenda ambayo CUF wamekuwa wakitaka lakini wameshindwa kuitetea sana hasa kwa kupitisha mchakato wa muswada wa katiba ambao unataka mambo makubwa ya Muungano yasijadiliwe

  Tatu CDM imekuwa inasisitiza katika serikali tatu ambayo ni ajenda ambayo Wazanzibar wanaitaka,lakini kupitia Bunge Mh.Tundu Lisu amekuwa akisemwa kuwa ana nia mbaya na Zanzibar na hivyo ana chuki na Wazanzibar japo sitaki kuamin hivyo

  Kutokana na maelezo hayo japo kwa uchache nawashauri viongozi wa CDM waingie Zanzibar hasa kwa kuwatumia John Mnyika na Zitto Kabwe kupata wanachama vyuo vikuu hapo Zanzibar.Nimewataja hawa vijana na viongozi katika CDM kwani wana uwezo mkubwa wa ushawishi na ni watu makini katika utendaji kazi wao.Kupitia vyuo vikuu Zanzibar CDM itaweza kupata wafuasi kwani naamini wasomi wana ushawishi mkubwa katika jamii.Tundu Lisu ni mwanasheria mzuri lakini asiende Zanzibar kutokana na chuki iliyopandikizwa kwake na wana CCM pamoja na CUF.
  CDM ikijipanga vizuri naamini hata Zanzibar itapata wafuasi kwani wananchi wengi hasa wasomi wanapenda chama kinachoikosoa serikal ambapo CUF imeshindwa kutokana na kuwa sehemu ya serikali.
  Ushauri wangu ndiyo huo kwa wana CDM.Wana CUF chukuen ushauri huu kama challenge kwenu ili mzidi kuimarisha chama chenu hasa kutokana na kuwa kimekosa mvuto bara.
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  wazo zuri!
   
 3. N

  NIPENDEMIMI Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  suala la cdm kusemwa na ccm juu ya hotuba yake ni MKAKATI WA KUPINDISHA MANTIKI YA HOJA YENYEWE NA KUPOTOSHA WANANCHI ILI MIND ZAO ZIHAME KWENYE KATIBA NA KUWASHAMBULIA WANAMAPINDUZI WA KWELI, HOTUBA ILIKUWA NZURI ILA IMEBADILISHWA NAKUWA CHUKI KWA SABABU YA UKOSEFU WA UMAKINI WA WANASIASA WA CCM,
   
 4. N

  NIPENDEMIMI Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmmhhh
   
 5. y

  yaya JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni makadirio tu haya. Kwamba 85% ya Waunguja ni wana CCM na 95% ya Wapemba ni CUF, kwa hiyo CHADEMA wakaokote wastani wa asilimia 20 (ambayo nadhani tayari wanayo), kati ya wastani wa Wazanzibari 800,000 ambao ndio politically active. Mhhh, sijui! Hata hivyo ni ushauri mzuri.
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  ili wakubalike Zanzibar itawabidi wawe wazi kuhusu hili udini linalozungumzwa sana kuhusu chama hiki.Nalog off
   
 7. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Usipende kuishi kwa propaganda.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Yaani hata useme nini DHAMBI hii ya ubaguzi walioinesha CDM kwa watanzania wa visiwa vya ZANZIBAR kamwe hawawezi kuitubu hata siku moja. Halafu nashangaa wanaomshambulia TINDU LISU wakati ile hotuba ilikuwa ni kutoka kambi rasmi ya Upinzani ambao kwa asilimia 99 ni CDM na kwa maana hiyo imeandaliwa na CDM , TINDU LISSU amepewa kusoma tu. Watanzania tumbuke maneno ya MWALIMU dhambi hiyo haitakaa iishe, ni kama kula nyama ya mtu. Wanachadema na hasa wale wasio kutoka kanda ya Kaskazini sijui wamejiandaa vipi kupokea ubaguzi wa mwingine baada ya ule wa Zanzibar kufanikiwa. Mimi sishangai kuona wakiwabagua wazanzibar, kwa vile TAFSIRI YA sera yao ya UMAJIMBO ndiyo hiyo.


  KAMA MNATAKA KUONA MOTO NJOONI ZANZIBAR
   
 9. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Siamini na sijawahi kusikia CDM wakiwabagua wazanzibar,hiyo ni propaganda inayoenezwa na CUF na CCM
   
 10. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Ccm ndiyo vinara Wa Udini Tanzania Watachonganisha watu weee!!!!! wakishapata tu kura basi wanawaacha solemba.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mchanga wa siasa za zanzibar na wala hujui upinzani zanzibar una mizizi yake toka 1957 ulipofanyika uchaguzi wa kwanza, na baadae 1963 kabla ya mapinduzi ya 1964. Kwa uchanga wako ndo unakurupuka na kudhani kwamba hao wahuni wako watapata ufuasi zanzibar, wakati huku kuna mikoa lukuki hata tawi hamjawahi kufungua. Unazungumzia kutaka kumhudumia mtoto wa mwenzio wakati wako anatembea mtaani makalio yakiwa wazi.
   
 12. j

  jigoku JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mbopo akili yako inakuambia kuwa ZNZ kuna vyama 2 tu?yaani CCM A na B?au unadhani wanzanzibar wote ni wajinga na wote wanafuata mkumbo? au unadhani hawawezi kuchambua kitu au jambo la kisiasa?kwa taarifa yako hotuba ya upinzani iliyotolewa juzi kwa wananchi wa ZNZ ndio hasa wanaitaka isipokuwa kwa viongozi wa CCM na CUF a.k.a CCM B.Hujui last week waZNZ juzi walitaka kuandaman juu ya muungano ivunjwe?Kwa taarifa wazo la kuipeleka CDM znz linawezekana
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  The whilms of politics always keeps on changing/evolving overtim
   
 14. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kuwa mchanga au mzee katika siasa si issue,toa hoja inayoeleweka!mbona Mnyika ni mchanga katika siasa lakini tumeona anavyoweza kujenga hoja kuzid hao wakongwe kama Wassira,jenga hoja..
   
 15. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  well said!
   
Loading...