Uongo wa Mizengo Pinda kuwekwa hadharani 14.02.2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongo wa Mizengo Pinda kuwekwa hadharani 14.02.2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Feb 11, 2011.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mmojawapo wa Watanzania waliokerwa sana na mauaji ya Arusha mjini ya raia 2 Watanzania na Mkenya 1.Tarehe 10/2/2011 wakti WM Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa papo aliamusha hisia kali kuhusiana na mauaji hayo alipokuwa anajibu swali la Mhe.Mbowe(MB)Hai na kiongozi wa upinzani Bungeni.Ndipo Godbless Lema(MB)Arusha mjini kwa kutoridhika na majibu ya Pinda aliomba mwongozo wa Spika kuhusiana na majibu ya WM afanyeje kwa uongo aliousema Pinda Bungeni. Kama kawaida ya Spika Makinda aliwaka na kumtaka Lema alete maelezo ya ushahidi wa kuonyesha kuwa WM amelidanganya Bunge.
  Sasa basi mimi napenda kumshauri Mhe. Godbless Lema kuleta uthibitisho wa uhakika ambao utakuwa na mambo ya msingi yafuatayo:

  1.Kwamba SI KWELI kuwa polisi wa walianza kupiga risasi za moto mita 50 kabla ya waandamanaji kukifikia kituo cha polisi chenye silaha. Uthibitisho: (1)Waliopigwa risasi na kuuawa hawakuwa mita 50 maana miili ya marehemu na majeruhi haikuuchukuliwa eneo la mita 50 toka kituo cha polisi. (2)Je, mkenya aliyeuawa naye alikuwa anaenda kuvamia kituo cha polisi ili achukue silaha kupeleka wapi?Je,polisi wanaweza kuthibitisha kuwa naye alikuwa ni mwanachama wa CDM? SI KWELI. Huu ni UONGO namba 1.

  2. Kwamba SI KWELI kuwa polisi walitaka kuzuia maandamano kwa kisisingizio cha Intelijensia. Maana baada ya mauaji ya tarehe 5/1/2011 maandamano yaliyofanyika siku ya mazishi ya marehemu 2 HAKUKUWA NA ULINZI WA JESHI LA POLISI NA HAKUNA FUJO WALA UVUNJIFU WA AMANI kama walivyodai polisi kwenye maandamano ya tarehe 5/1/2011. Badala yake wana CDM wenyewe ndiyo waliamua kusimamia shughuli zote za mazishiHapa lazima ikumbukwe kwamba siku ya mazishi watu ndiyo wangelikuwa na uchungu/hasira na wangeweza kufanya fujo zaidi. Lakini they proved the Police force totally wrong. No intelligency issue no nothing. Huu ni UONGO namba 2.

  3. Kwamba polisi walianza kuwapiga waandamanji kwa risasi za moto,mabomu ya machozi na maji ya washawasha katika eneo la Stand kilomita 2 toka kituo cha Polisi kinachodaiwa kutaka kuvamiwa na waandamanji. Huu ni UONGO namba 3. Urhibitisho: Lema lazima alete PICHA ZA VIDEO kuonyesha maeneo ambayo polisi walianza kurusha risasi za moto.

  4. Lema aandae PICHA ZA VIDEO kuonyesha kwamba Polisi walianza kuyashambulia magari ya Wabunge wa CDM kwa kuvunja VIOO v wakitumia virungu huku wakiwanyang'anya simu na vitu vingine vya thamani. Mchumba wa Dk.Slaa ni mmoja wa wahanga waliopigwa sana na kutokwa damu nyingi. Huyu naye hakuwa umbali wa mita 50 toka Police post. UONGO namba 4.

  5. Kwamba MIKANDA YA VIDEO YA Polisi iliyo onyeshwa kwenye vituo vya Televisheni ya TBC1 na ITV ilikuwa imechakachuliwa UONGO kwa maana ilikuwa imefutwa kwa maana kuwa EDITED and DELETED some of the sensitive areas,kama marehemu wakipigwa risasi au wakibwebwa kupelekwa hospital or mortuary! Hakuna hizo picha. Uongo namba 5.

  6. Kwamba baada ya MAUAJI, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Vuai Nahodha aliahidi kuvikutanisha vyama vyote viwili CDM na CCM ili wakae meza moja kumaliza mgogoro huu uliopelekea mauaji LAKINI WAZIRI NAHODHA HAKUFANYA HIVO na WALA PINDA HAKUZUNGUMZIA TAMKO HILO LA NAHODHA. Uongo na 6.

  7. Picha zote za VIDEO zenye kuonyesha MATUKIO HALISI YA MAUJI ZICHEZWE KWENYE VIDEO PLAYER MBELE YA BUNGE LOTE ili kuweza KUJIRIDHISHA nani MKWELI na nani MWONGO kati ya Mbunge Lema na PM Mizengo Pinda.

  8. Naomba wabunge wote na Wanasheria wote wa CHADEMA wakiwemo kina Tundu Lissu na Mabere Marando ili kuweka mkakati wa USHAHIDI WA KUAMINIKA ILI KUWEZA KULITHIBITISHIA BUNGE KUWA CHADEMA WAKO MAKINI NA WANACHOKISEMA.
  God bless you Godbless Lema.
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I concur
   
 3. escober

  escober JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  have my maximum support
   
 4. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  :clap2:
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  aah! Huyu baba anamatatizo sana, anatumiwa na mafisadi kutupoza, NAIMAN LEMA ATAWEKA UKWELI KWEUPE!
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Lema tunayemfahamu anamgaragaza ma makinda. Tutajicha wapi kuwa na spika mbovu kiasi hiki.
   
 7. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni muungwana gani asiyejua uhalifu wa polis kule arusha? Sasa wamemchokoza wenyewe akitoa ushahidi watadhalilika mno na ni fedheha kwa pinda, maza na sirikali yao dont4get sisimu
   
 8. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Wana JF

  Ahsante kwa wale mnaoendelea kuchangia topic hii kuhusu kile kinachotakiwa kupelekwa Bungeni na Mhe. G.Lema kuthibitisha madai yake kuwa PM Pinda alilidanganya Bunge wakti akijibu swali lenye kuhusiana na mauji ya Waandamanaji tarehe5/1/2011.

  Napenda tu kuongezea kwenye point ya kuhusu yule Raia wa Kenya aliyepigwa risasi kwenye maandamano hayo wakti alikuwa hahusiki wala hakuwa mita 50 toka kituo cha polisi.
  Kwamba Jeshi la Polisi walitaka kughushi JINA LA MAREHEMU NA KUMWITA GEORGE WAITARA na kuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Mara. Lakini baada ya Viongozi wa CHADEMA kufuatilia kwa uhakika ili kujua huyo marehemu alikuwa nani na anatoka wapi ndipo WALIPOGUNDUA KUWA MAREHEMU HAKUWA GEORGE WAITARA baali alikuwa ni PAULO NJUGUNA KAIYEHE(26) MKAZI WA ENEO LA KAJIADO,NGONG-KENYA.


  Lema lazima apeleke ushahidi wa tukio kama hili la KUUA RAIA WA NCHI NYINGINE AMBAYE HAKUWA MFUASI WA CHADEMA WALA HAKUWA KWENYE MAANDAMANO NA PINDA AULIZWE POLISI WALITAKA KUFICHA NINI KWA KUMWITA MAREHEMU KUWA NI GEORGE WAITARA. Lema vilevile katika ushahidi wake amwulize PM PINDA NA BUNGE LOTE KAMA SERIKALI IMEWAHI KUOMBA RADHI KWA SERIKALI YA KENYA KUTOKANA NA MAUAJI YA RAIA WAKE AMBAYE HAKUWA NA HATIA!

  PINDA,MAKINDA NA BUNGE LOTE LAZIMA WAPATE HIYO PICHA ILI WAJUE NANI AMESEMA UONGO.
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  pinda alisema waliopoteza maisha katika tukio la arusha ni watanzania watatu... ukweli uliopo ni kwamba waliokufa ni watanzania wawili na mkenya mmoja...hata kama aliteleza lakini...ule ni uongo tosha
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Mbona wanachelewa kumuumbua, yaani Pinda nilikua namuona mtu wa maana lakini since the day alivyopitishwa pale bungeni akaanza kwa mipasho ya kejeli nikajua tayari haka nako kameshalewa madaraka. hebu fanyeni fasta basi tumuone aibu yake
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kuna wengine walipigwa risasi ndani ya kanisa katoliki. Kanisa liko mbali zaidi ya mita 50. Makinda aeleze ni adhabu gani atampa Pinda kwani ni dhahiri alilidanganya bunge.
   
 12. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  wako kwenye mpango mahususi wakupoteza /kuharibu nyaraka zote na lema asiruhusiwe kusoma utetezi
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hawa tuwajuavyo, wapo hovyo sana......waroho, hakuna hata mtu mmoja atskayeweza kufanya umafia kwa Lema
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi naye lema ni mafia pia?

  Kweli hatuna wabunge huko chadema.
   
 15. peck

  peck JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kaka tupo pamoja
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kosa lenye heri alilofanya Spika Makinda kwa kumkingia kifua Pinda ndio amemdhalilisha zaidi Pinda wakati hoja ya kuonyesha uwongo wa kauli ya Mizengo utakapoletwa bungeni na Lema ambaye ni mhusika mkuu katika sakata la Arusha. Busara ya kujibu swali ni muhimu sana badala ya kujengo hoja ya kujitetea tu. Spika wa Bunge kuwa mwanasheria inasaidia kuwa na upeo wa kuelewa hoja za wabunge. Lakini Makinda ameonyesha dhahiri si mwanasheria na uspika kaupata kwa njia wanazojua wakubwa zake. Badala ya kujibu hoja ya mbunge yeye anapaniki na kuanza vitisho kwa Lema.
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja!
  PINDA kubali vyombo vya dola vilikosea jinsi ya ku-handle suala la arusha.kubali kosa,omba msamaha at least kwa ndugu wa marehemu then unda tume ya uchunguzi na baadae chukua hatua stahili dhidi ya wahusika(iwe CDM,CCM or polisi).Hii ndio njia sahihi ya kushughulikia jambo hili.kumbukeni damu ya 'mmachinga' mmoja kule Tunisia imeangusha serikali mbili sasa fikiria kuhusu damu ya watu watatu inaweza kufanya nini.
  TO ALL GOV.OFFICIALS:Once mnapokua kwenye nyadhifa zenu mnatakiwa kuwajibika kwa wananchi wote sio vyama,kabila au dini zenu.


  "HATUHESHIMU WAZEE KWA SABABU HAWATAMBUI HESHIMA TUNAYOWAPA"
   
 18. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :clap2:
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anajibu swali la mbunge wa Manyara alietaka Waziri mkuu aelezee kilichotokea Arusha. kupeleka picha na video za matukio ya tarehe 5-1-2011 ni sawa lakini kinacho takiwa ni kiini cha matatizo ya Arusha ambapo ndipo kwenye uongo wake soma attachment za Josephine.
   
 20. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Endapo baada ya ushahidi kutolewa na GLema, na Spika kama ilivyo kawaida ya CCM wakapiga kura ya kumpa adhabu yeyote kama walivyofanya kwa Zito, Ninashauri vijana kote nchini tufanye kweli kama Tunisia na Eqypt. Tarehe 14 February 2011, siku ya wapendanao igeuke siku ya ukombozi. A LUTA CONTINUA!!!
   
Loading...