Uongo uletao madhala kwenye jamii

sunguruma

Member
Sep 14, 2012
34
6
[h=5]Tatizo sio Imani zetu, tatizo sio utamaduni wetu, LAKINI Tatizo ni mazoea tuliyoyajenga, tatizo ni mzoea tuliyoyaaendekeza kwa muda mrefu, mazoea ya kusema uongo, Mazoea ya KUDANGANYA. Karibu kila mtanzania awe mwenye dini au asiye na dini awe mtu mzima au mtoto awe mwenye akili timamu au punguani kwenye eneo hili tumejizoesha vibaya.

Mazoea ninayoyasema hapa ni mazoea ya kuwaambia watoto wetu mambo ya UONGO na kuwaaminisha. Mara nyingi nimewasikia watu wazima wanawaambia watoto wao “usilie mtoto mzuri nitakuletea na pipi” Mtu mzima anasema hivyo hali akijua kuwa hatatimiza hiyo ahadi yake, anasema hivyo hali akijua kuwa anamdanganya mtoto. Huu ni UONGO kama UONGO mwingine, na hatuwatendei haki watoto.

Kuna vitu vingi sana tumewaaminisha watoto vitu ambayo sio kweli. Kwa mfano mimi nilipokuwa mtoto mdogo niliambiwa ukimruka mwenzio utamfanya asikue, au ukiota moto kimgongo mgongo mama yako atafariki au ukila chukula huku umelala basi wazazi wako wote wawili watafariki.

Sasa inaonekana kasumba hii imeingia mpaka kwenye Dini. Vurugu na machafuko yaliyotokea Mbagala kuzuiani chanzo chake ni UONGO alioambiwa mtoto na watu wazima. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi chanzo cha vurugu hizo ni ubishani wa watoto wawili kuhusiana na nini kinaweza kutokea kama Quaran inatemewa mate au kukojolewa.

“Akizungumzia suala hilo, mkazi wa Mbagala Mission, Nassor Mohamed alisema vurugu hizo zilitokea baada ya mtoto mmoja kukojolea Quran. Alisema mtoto huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo na ubishi na mtoto mwenzake ambaye wanasoma wote katika Shule ya Sekondari Chamazi.

Mohamed alisema mtoto huyo mwenye miaka 14, alikuwa akibishana na mwenzake mwenye umri kama huo kwamba mtu akikojolea kitabu hicho hugeuka kuwa nyoka. Alisema kuwa mtoto huyo aliamua kufanya kitendo hicho ili kuona kama atageuka nyoka na wakati akifanya kitendo hicho mzee mmoja alimuona na…...” Source Mwananchi, October 13

Kila mtu anajua kuwa watoto ni wadadisi. Sasa kosa la huyu kijana kukojolea Msaafu nani wa kulaumiwa? Nadhani wa kulaumiwa hapa ni sisi watu wazima ambao badala ya kuwaambia ukweli watoto kuwa msaafu kama kitabu kitakatifu unapswa kuheshimiwa, na kuwaambia sababu za ukweli kwa nini kitabu kitakatifu kinapaswa kiheshimiwe. Sasa wewe mtu mzima, hali ukijua kabisa kuwa unatenda dhambi, unamjaza mtoto uongo kuwa ukichana ukurasa wa Msaafu au Biblia sijui unageuka mjusi, watu wengine wamejichokea maisha ya kuwa binadamu wanaamua kwa makusudi kabisa wachane Msaafu au Biblia wageuke kuwa mijusi wanaona Olaaa! Na baada ya hapo tunapata madhara makubwa sana, maana kwanza watu kama hao wanapoteza imani yao kwenye hivyo vitabu kabisa, maana alichoaambiwa akifanya kitatokea anajikuta hakijatokea.

Nimesikia mara nyingi kuwa ukimkosea Muislamu akienda akakusomea aya fulani fulani kwenye msaafu unakufa au mambo mabaya yanakutokea. Jamani tuache uongo kama huu, uongo kama huu ndio unasababisha watu wasimjue Mungu. Watu wanaaminishwa mambo ambayo sio ya kweli. Mungu hata siku moja hawezi kushusha kitabu ambacho watu watakitumia kwa ajili ya mambo ya kishirikina, mambo ya kurogea watu, SIO KWELI hata siku moja, Mungu wetu hawezi kuwa Mlozi kama kweli unaamini katika Mungu aliye Hai. Matokeo ya uongo wetu kama jamii ndio haya. Vurugu za Mbagala Kizuiani zinatokana na jamii yetu kukwepa kujibu maswali ya msingi tunayoulizwa na watoto, Jamii nzima tunjaribu kukimbilia majibu mepesi mepesi.

Karatasi za vitabu vyote vilivyopo duniani sasa hivi zimechapwa kwenye mashine za kawaida na ni karatasi za kawaida zinazoweza kuungua kwa moto, zinaweza kulowa na mvua hata kuharibiwa na mchwa. Tunachopaswa kufanya ni kuweka ukweli, kwanini tunaviamini hivyo vitabu, iwe Biblia au Quaran. Mambo ya kudanganyana yamepitwa na wakati, huu ni wakati tofauti. Sasa hivi tunasoma maandiko matakatifu kwenye computer zetu, tunayatafuta kwa google, na google hiyo hiyo inatumika kutafuta hata picha za ngono, tunajifunza mbinu za ujasusi, ugaidi, mauaji, na za mambo mengine mabaya yanayopingana na imani na mafundisho ya dini zetu. Sasa tukanyage na kutia moto komputa zote???

Shida nyingine iliyoko kwenye jamii ni kuamini sana katika miujiza, jamii yetu sasa imekaa kusadiki sana katika miujiza. Watu wakisikia leo Fulani akikuminyia jicho moja basi unapata pesa , unakuwa tajiri unaona hao wamemiminika kwa mamilioni, wakisikia kuna mtu anatoa mchanga kwenye kijiko ukimeza umepona kansa kesho unapewa mamilioni ya pesa mpaka mtu unaweza kukosa mahali pa kutunzia. Ninadhani jamii iaanze sasa kuachana na tabia twa kusema sema uongo mdogo mdo[/h]
 
Ngoja nikaangalie kwanza picha ya mwalimu aliyekuwa na RPC kwenye gari, ntarudi.
 
Back
Top Bottom