Uongo na Hadithi za Kutungwa vilivyogeuka ukweli wa Dunia Kumuhusu Samaki Mtu

nabiidaniel

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
836
1,000
Kwa hiyo we unaona mabaharia wakuu wote ma wasafiri maarufu baharini kama kina columbas ni wazushi kwa sababu hawajapeleka mabaki maabala kuthibitisha. Hao ni mashetani ya baharini, yanaonekana yanapotaka yenyewe na sio wewe unapotaka, ni kama popobawa na mapepo mengine, kutaka watu wathibitishe haitawezekana, ila ipo siku yatakutokea, na wewe utashindwa kuthibitisha na utaonekana mzushi.
 

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
250
Kwa hiyo we unaona mabaharia wakuu wote ma wasafiri maarufu baharini kama kina columbas ni wazushi kwa sababu hawajapeleka mabaki maabala kuthibitisha. Hao ni mashetani ya baharini, yanaonekana yanapotaka yenyewe na sio wewe unapotaka, ni kama popobawa na mapepo mengine, kutaka watu wathibitishe haitawezekana, ila ipo siku yatakutokea, na wewe utashindwa kuthibitisha na utaonekana mzushi.

Mkuu kwa hiyo unataka kuniaminisha kuwa kuna viumbe wengine wanaitwa majini, nitaaminije wakati sijawahi kuona? kwa nini nisiziite hadith za masimulizi? maana mwanadamu amepewa uwezo mkubwa wa kutunga hadithi ikafanana na ukweli kabisaaaa, embu kama wewe ni mfuatiliaji wa movies angalia movie inaitwa ,Jack the Giant slayer, uwaone viumbe wa kufikirika, sidhani kama hizo hadithi za kutungwa zinatofautiana na imani uliyonayo hapa, walatini wanasema EX NIHILO NIHIL FIT(NOTHING COMES FROM NOTHING)
 

Neriah

JF-Expert Member
May 7, 2012
267
250
hao samaki wapo tatizo ni ngumu kuthibitisha maana humtokea mtu mmoja mmoja na inaogopesha inakuwa ni ngumu hata kuchukua picha
 

miku

Senior Member
Oct 24, 2011
148
225
Hz ni hadithi za kufikirika tu zilianza karne nyingi sana hasa hasa wkt mabaharia wakirudi safari zao na kuja kutoa habari nyingi za uongo.hakuna tofauti na vampires,wolfs nk.
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,071
2,000
Nachojua mm hao viumbe wapo ila co watu km wanavyofikiria, ni majini, hata ukiangalia kwnye pirates of caribean utagundua kuwa mermaids sio viumbe wa kawaida, ni majini.
Na kwa historia fupi ni kuwa huko miaka ya zamani sana kuna malikia alimuua mpenz wake kwa bahati mbaya,ss ile kujutia ndo akaamua kujigeuza jini samaki mtu na kuishi baharini

Kwa hiyo wewe unaamini wapo kwa ku refer pirates of the caribean?
Hiyo ni movie tu kama ilivyo avatar just fictions tu.
 

King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
250
sijasema naamini refer to pirates of caribean, ila nitoa pirates km mfano

kaka imani kuwa samaki mtu ni.kama majini umeipatia wapi? umeulizwa hapo, kwenye movie au wapi au ulisimuliwa na kusoma story za watu kama akina columbus?
 

egentle

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
771
500
Habari ya siku ya leo wadau, ni kwa mara nyingine tena naileta kwenu mada nyingine inayomuhusu Kiumbe wa ajabu ambae inasemekana anaishi majini/baharini, kiumbe huyu habari zake huwa zinazungumzwa maeneo yote ya dunia yetu hii na asilimia kubwa ya watu wana amini kuwa kiumbe huyu ni kweli yupo, kiumbe huyu inavyosemwa ni kwamba ana umbo la samaki nusu yaan kuanzia mkiani mpaka kiunoni ni samaki, wakati kuanzia kiunoni mpaka kichwani ni umbo la bibadamu. Kiumbe huyu anafahamika kama SAMAKI MTU wazungu wanamwita MERMAID. Na maeneo mengi ya dunia wanasimulia hadithi mbalimbali kumuhusu samaki mtu, na inavyosemekana samaki mtu wapo wa kike peke yake.

Lengo kuu la kuileta mada hii, kwanza ni kutaka kuonyesha imani yangu juu ya uwepo wa kiumbe huyu, binafsi mimi siamini hata kidogo, samaki mtu ni kiumbe wa kufikirika kama vile hadithi za mazimwi. pili naomba nielezee kifupi uwongo ulioenea ambao sayansi haijathibitisha mpaka leo kuhusu yoote yanayosemwa kumuhusu kiumbe huyu

1. Hii ni maalumu kwa watanzania na wote wanaoiongea lugha ya kiswahili, kumekuwepo na upotoshaji mkubwa katika hili, wengi wanamwita samaki mtu kuwa eti ndiyo NGUVA, huu ni uwongo mkubwa, samaki mtu sio nguva, nguva anatambulika kibaiologia na ushahidi wa uwepo wake upo, ni mnyama anayeishi baharini na hafanani na binadamu, ushahidi wa nguva upo jumba la makumbusho Dar es saalam, samaki mtu hakuna ushahidi wa mwili wake uliotunzwa sehemu yoyote ile duniani. Hivyo tujirekebishe wale wote tunao litumia jina Nguva tukimaanisha samaki mtu.

2. Si afrika tu tulio na imani ya uwepo wa samaki mtu, hata kwa wenzetu wazungu uvumi wa kuonekana kiumbe huyo ulijitokeza zamani sana miaka ya nyuma, na mtu alieneza habari hizo ni mtu mashuhuri sana katika historia ya dunia, mtu huyo ni Christopher Columbas kwa wasiomfaham Bwana Columbas alikua ni muhispania baharia na Mtu alievumbua bara la america, yeye alisema katika safari zake za baharini alikutana na samaki mtu watatu ila si wazuri wa sura kama watu wengi walivyowasimulia kwenye hadithi na kuwachora, na pia alisema hawaongei kama binadamu.

3. Ukiacha mbali hadithi na maelezo ya bwana columbas, vile vile habarivza kuonekana kwa kiumbe huyo zimesikika sehemu nyingine nyingi kama vile Canada, Israel na Zimbabwe, mfano baada ya kuzuka kwa minong'ono mingi ya kuonekana kwa samaki mtu maeneo ya fukwe za jiji la Kiryat Yam, nchini israel, jiji lilitoa ofa ya kiasi cha pesa cha dola millioni moja kwa yeyote atakae leta ushahidi wa habari hizo, lakini mpaka leo hakuna lolote.

4. Nchini Zimbabwe, mwaka wa2012 wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi kwenye reserve moja ya maji waligoma kuendelea kufanya kazi kwa madai kuwa wamefukuzwa na samaki mtu, na tukio hilo lili reportiwa na waziri wa maji wa Zimbabwe

5. Kipindi cha gharika la Tsunami, ili lipotiwa kuwa yameonekana mafuvu ya samaki mtu ambayo yalitupwa nje na maji, lakini wanasayansi walipoyachunguza hawakutoa tamko kuwa ni kweli mabaki hayo ni ya samaki mtu.

6. Taasisi inayohusika na utunzaji wa bahari na viumbe wa baharini ya marekani (The US National Ocean Service) mwaka 2012 ilitoa tamko kuwa hakuna ushahidi wowote ule mahali popote uliowahi kuonekana unaothibitisha kuwa kuimbe huyo yupo.

Je? wewe unaamini uwepo wa kiumbe huyu?
Tamaduni nyingi kutoka jamii mbalimbali duniani zimeonyesha imani kubwa sana ya uwepo wa kiumbe huyu, ukiangalia baadhi ya kazi za sanaa hasa filamu na sanaa ya uchoraji kiumbe huyu ameonyeshwa kwa namna mbalimbali. Mfano filamu inayojulikana kama Splash(1984), nyingine ni Pirates of Carribean: On stranger Tides (2011).

Wewe umesikia au unasikia nini kuhusu uwepo wa kiumbe huyu, nakaribisha michango ya wavuvi na wale wakazi waliokulia muda mrefu maeneo ya pwani.
Asanteni

attachment.php

I thnk ishu za mermaid zipo ki spirit zaid uwezi prove machoni.
 

Chambo81

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
442
0
Hiyo picha imenifurahisha sana naona kuna huyo binti samaki Ana sidiria ameinunulia wapi huko baharini!!?Ni Kweli hii ipo kiimani zaidi sio halisia!!
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,673
2,000
Mkuu usibishe samaki mtu kweli yupo,nakumbuka siku moja[2001] nilizinguana na demu wangu so nikaenda kutuliza zangu akili pwani kisiwani pemba,ilikua jioni flani hivi na eneo hilo nilikua peke yangu ghafla nikaona kiumbe kama demu anaogelea katika kina kirefu cha bahari kuu ya pemba[wapemba nadhani wanaelewa sehemu gani naizungumzia] kwanza nikapata mshtuko coz sio rahisi kwa bahari kuu kuogelea watu tena demu halafu yupo peke yake mimi nilidhani jini c unajua mambo ya pemba.
Kile kiumbe kikatoka hadi kandokando ya bahari karibu na nilipokua mimi,
Nilishindwa kuvumilia kwani sikuwahi kutegemea kuona mtu chini samaki,
Nilipoteza faham kilichoendelea sikujua kwakweli.
ANGALIZO
Samaki huyu yupo ila ngumu kumsibitisha coz anatokea mazingira tata na pia mara nyingi humtokea mtu mmoja,mfano angalau jini yupo ila huwezi thibitisha uwepo wake
Wewe ulikuwa unazinguka na demu wako ndipo ukapata hayo maruweruwe!hakuna samaki mtu kama ilivyokuwa hakuna dragons,hecules,medusa,pandora box,andromeda,goblins,ni utunzi mahiri wa hadith tu ndugu yangu!
 
Oct 12, 2013
95
70
jamani hawa viumbe mbona wapo.na si samaki kama hao wasemavyo bali ni DJINN yaani JINN na kwa macho ya kawaida huwezi kuwaona ni ki spiritual zaidi.ila wapo hilo halina ubishi na hao wanaosema ni wakike tu si kweli sema labda wao huofia kuwavua wa kiume kwa woga wa kuzidiwa nguvu maana viumbe hawa wana nguvu kali mithili ya ngurumo za radi akikupitia bahari ya hindi sekunde hiyohiyo unaibukia bahari ya sham.wapo we amini tu hivyo ila huwezi waona wala kuamini kama huna elimu juu yake.plz wasije kuniadhibu bure
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,574
2,000
hakuna kitu kama hicho, eti kuna samaki mtu....hizo ni hadithi
 

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,246
2,000
Nguva ni sawa na hadithi ya Vibwengo; hadithi hizi ni za wavuvi na mauzauza wanayokutana nayo baharini.

Kama yupo samaki nguva, basi ndio vibwengo wenyewe wanaojigeuza kuwa mara watu mara vibwengo.

Hayo ni majini tu kama majini yanayojigeuza kuwa watu.

Vv
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom