Uongo ambao dunia inauamini kuwa ni ukweli

Uongo ambao dunia inauamini kuwa ni ukweli

Mit 16:4
BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.



NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.


Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.



Kuna wakati Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno haya;

Yohana 13:7 “Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye”.

Ikiwa na maana kuna mambo ambayo Mungu anayafanya , kamwe hatutakaa tuyaelewe kwa sasa, bali baadaye sana. Na “Baadaye”, inaweza kumaanisha kipindi kirefu kijacho, au wakati wa baada ya haya maisha.

Hivyo basi, hakuna mwanadamu anayeweza kutolea majibu kila jambo analolisoma kuhusu Mungu, isipokuwa tu tunapapasa-pasaka, na kuelewa yale tuliojaliwa kuelewa na Roho Mtakatifu kwa sasa (Matendo 17:27).

Leo kwa sehemu tutaona, kwanini Mungu alisema maneno haya.

Sehemu: Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.

Swali linaloulizwa hapo, Je! Ni kweli Mungu aliwaumba wabaya ili kutimiza kusudi la ubaya?

Jibu ni ndio kama ilivyoandikwa.

Utauliza, ni kwanini sasa aseme yeye ni Mungu wa upendo, apendezwaye na haki? . Jibu ni lile lile, afanyalo leo hatutalijua, sasa lakini tutalijua vizuri baadaye. Na mawazo yake si mawazo yetu.

Ni vichache tu tunaweza kujua kwanini amewaumba watu wabaya kama ibilisi na mapepo yake, na waovu kama akina Kaini, kora, Belshaza? Ili wafanye mabaya duniani?

Majibu tuliyopewa kuyaelewa, ni ili kutimiza makusudi yake matatu makuu;

kufundisha
kuadhibu
kuonyesha uwezo wake.
Kwamfano tunapoona hatma ya ibilisi na matendo yake maovu, hakuna hata mmoja anapendezwa na tabia kama zile, hivyo na sisi tutajilinda na dhambi ya uasi, kwa gharama zote, kwasababu tunajua mwisho wake utakuwa wapi. Hivyo yeye na watu wabaya wamekuwa funzo kubwa kwetu sisi, juu ya madhara ya dhambi.

Kama wasingekuwepo, tusingejua uzuri wa haki. Huwezi kujua sukari ni tamu kama hujawahi kuonja kitu kichungu, huwezi kujua hili ni joto kama hujawahi kuhisi baridi kabisa. Vilevile hatuwezi kujua Mungu ni wa upendo kama hatujakaa na watu wabaya, kama vile wauaji, wabinafsi n.k

Vilevile ameruhusu kwa lengo la kuadhibu, pale tumkoseapo Mungu. Anaruhusu watu kama akina Nebukadreza wa Babeli, kutuadhibu, kama wafilisti kwa Israeli walipomkosea Mungu. Hivyo wanasimama pia kama fimbo ya Mungu kwa watu wake kuwafunza.

Na vilevile kuwapa sababu zote hao watu wabaya kwanini wanastahili hukumu siku ile ya mwisho kwa matendo yao.

Pia sababu ya tatu ni ili kudhihirisha uweza wake mwingi. Mungu huwa anaruhusu wachawi kama Yane na Yambre washindane naye ili atoe maajabu yake yote, anaruhusu watu kama Farao wawe na mioyo migumu ili aonyeshe uweza wake mkuu wa uokozi, aliruhusu taifa lake Israeli lizungukwe na maadui zake aonyeshe jinsi anavyoweza kuokoa.

Soma hapa;

Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.

18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.

19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?

21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;”

Hivyo basi, hizi ni baadhi ya sababu, lakini zipo nyingine zaidi ya hizo ambazo tutakuja kuzifahamu baadaye.

Hii ni kutufundisha nini?
Ni kutufundisha unyenyekevu, tukubali kufanyika watu wema, ili tusiwe vyombo vya ubaya, Kwasababu kila jambo unaloliona duniani, liwe baya liwe jema, lipo chini ya makusudi ya Mungu, hakuna linalotokea kwa bahati mbaya, na ndio maana mengi ya hayo bado hayajaondolewa yote. Lakini utafika wakati yataisha.

Kumbuka hatuna miaka 100 tu ya kumjua Mungu, bali tuna umilele mbeleni, Hivyo kwa kipindi hichi kifupi hatuweza kutoa habari zote za Mungu, na kumuuliza kwanini umeruhusu haya, au yale..tuwe watulivu.

Tupende mema tuwe salama, tumpe Kristo maisha yetu ili tusiwe vyombo vya ghadhabu kama Farao, bali vya heshima.

Bwana akubariki.
haleluuuuuuuuuuyaaaaaaaaaaa
 
. Anga Kama Kuba Thabiti (Firmament / Dome)
Katika cosmolojia ya kale, anga lilichukuliwa kama bakuli thabiti lililopinduliwa juu ya dunia ili kuzuia maji ya juu yasianguke chini. Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni "Raqia" (רָקִיעַ), ambalo linaashiria kitu kilichopondwa au kupondwa kwa nyundo kikawa kigumu (kama bati la shaba):
• Mwanzo 1:6-7 — "Mungu akasema, Na liwe anga (raqia/firmament) katikati ya maji, likatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akatenga yale maji yaliyokuwa chini ya anga na yale maji
yaliyokuwa juu ya anga; ikawa hivyo."

• Ayubu 37:18 — "Je! Waweza kutandaza anga pamoja naye, lililo imara kama kioo kilichoyeyushwa?"

• Zaburi 148:4 — "Msifuni, enyi mbingu za mbingu, nanyi maji mliyoko juu ya mbingu."

2. Dunia Kujengwa Kwenye Misingi Chini ya Bahari
Mistari hii inaeleza dunia kuwa na misingi na nguzo zilizosimamishwa ndani ya maji makubwa ya chini (the deep/abyss) ili ardhi isitikisike:

• Zaburi 104:5 — "Aliiweka nchi juu ya misingi yake, isitikisike milele."

• Zaburi 24:1-2 — "Nchi na vyote viujazavyo ni vya BWANA... Maana aliiweka juu ya bahari, na kuiweka imara juu ya mito."

• 1 Samweli 2:8 — "...Maana nguzo za dunia ni za BWANA, naye ameweka ulimwengu juu yake."

• Ayubu 38:4-6 — "Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?... Au msingi wake ulizikwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeweka jiwe lake la pembeni?"

3. Dunia Kuwa Tambarare (Bapa / Flat)
Mistari hii inataja vitu vinavyowezekana tu ikiwa dunia ni tambarare (bapa), kama vile kuona dunia nzima ukiwa juu ya mti mrefu au mlima mrefu, au dunia kuwa na mipaka na pembe:

• Danieli 4:10-11 — "Maono ya kichwa changu kitandani mwangu yalikuwa hivi; naliona, na tazama, mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa mkubwa sana. Mti huo ukakua, ukawa na nguvu, na urefu wake ukafika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake kulifika mpaka mwisho wa dunia yote." (Kwenye tufe huwezi kuona mti mmoja ukiwa pande zote za dunia).

• Mathayo 4:8 — "Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wao."

• Ufunuo 7:1 — "Baada ya hayo naliona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia upepo nne za nchi..."

• Ayubu 38:13 — "...ili ishike miisho ya dunia, na wabaya wakung'utwe kando yake?"

Watafsiri wengine WA theolojia wanatafsiri kuwa lugha iliyotumika ni USHAIRI mara ni lugha ya picha haikuwa na MAANA hiyo ..LENGO ni KUAMINISHA watu kuwa DUNIA ni duara.

Lakini NENO linasema kwamba
• Luka 12:2 – "Hakuna kilichositiriwa ambacho hakitafunuliwa, wala kilichofichwa ambacho hakitajulikana."

• Mathayo 10:26 – "Kwa hiyo msiwaogope; kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana."
na wanavyotuaminisha kuwa dunia ni duara toka tukiwa watoto wadogo wanatuficha kitu gani ama ni kitu gani hasa hawataki tujue iwapo tutafakamu kuwa dunia ni tambarare
 
na wanavyotuaminisha kuwa dunia ni duara toka tukiwa watoto wadogo wanatuficha kitu gani ama ni kitu gani hasa hawataki tujue iwapo tutafakamu kuwa dunia ni tambarare

LENGO KUU ni KUMTAWALA MWANADAMU, KIFIKRA/ELIMU,kiafya ,kiuchumi,na hata IDADI YA WATU...Na KUMFICHA ELIMU KUBWA ZAIDI KUUJUA UKWELI KNOWLEDGE IS POWER WITHOUT KNOWLEDGE wanadamu wanakuwa weak KUAMINI KILE WANACHOAMBIWA NA WANACHOAMULIWA ..ni kama KUABUDU MFUMO ambao upo kinyume na mpango WA Mungu,mpinga KRISTO Beast system

Wanazuai usijue UKWELI KUHUSU ANTARCTICA , Antarctica sio Bara Bali ni ukuta wa barafu japo chemical composition yake ni tofauti na barafu ambao INAZUNGUKA duniani tambarare kwa MFUMO WA duara pembeni ya kingo za DUNIA.

Uwepo WA firmament kwa juu glass dome ngumu inayofunika anga la DUNIA kutenganisha maji YALIYOPO angani,Ina madirisha na milango ya mbinguni,Juu kuna mbingu ya Mungu

Misingi ya DUNIA nguzo zake zipo chini ya bahari zinazoishikilia DUNIA

Kwa chini ya DUNIA KATIKATI kuna shimo la KUZIMU SHIOLE AMBAPO hata wanasayansi walichimba shimo refu ARDHINI wakafunga mic recorder ika record sauti za vilio vya watu walioko KUZIMU zikiteswa kwa sekunde chache kabla ya mic hiyo ngumu sana kuunguzwa na moyo mkali ULIOPO kwenye shimo la KUZIMU

GRAVITY NI UONGO hakuna force of gravity nguvu ya mvutano WA dunia ,BALI VITU VINAELEA angani au kwenye maji ,ama kuzama kutokana na TOFAUTI ya Density na BUOYANCY kati ya vitu,na Wala sio kwa sababu ya gravitational force ambayo HAIPO ni UONGO

UWEPO WA DUNIA NYINGINE NYiNGI kama hii ya kwetu other civilisations,ambazo zinaonekana mbele ya ukuta wa Antarctica amabazo zime advance kuliko hii ya kwetu,hata Hawa A
LIENS wengine wanatokewa huko,na kuna spiritual portals za kuingilia HUKO

ELIMU ZA KWELI ZA ANCIENT EGYPT ANCIENT WORLD ZIMEFICHWA ,Mapiramidi yalivyojengwa n.k

ELIMU HALISI za nature,tumeletewa MFUMO WA ELIMU NA PESA na AJIRA ILI KUTUTAWALA NA KUTUANGAMIZA


NA ELIMU ZILIZOFICHWA NI NYINGI TU..ELIMU HALISI NA MAARIFA HALISI YA KUMSAIDIA MWANDAMU AMBAYO HAYAHTAJI KUWALETEA FAIDA WAO NA VIWANDA VYAO(MAPINDUZI YA VIWANDA BIASHARA ZAO)

mfano
KILIMO UFUGAJI NA CHAKULA--zipo elimu na MAARIFA Bora ambayo hayahitaji MBOLEA za VIWANDANI,MBEGU ZA viwandani GMO,hata katika mazingira ya JANGWA lakini ELIMU HIZI ZINAFICHWA KWA MASLAHI YA VIWANDA BIASHARA.

Mavyakula yasiyo na afya ya viwandani..wakati upo uwezekano WA KUZALISHA vyakula vya ASILI vitakavyobiresha afya za watu..kuliko ulaji usiofaa WA sukari za viwandani,vinywaji VYA VIWANDANI,vyakula FAST FOODS JUNK FOODS matakataka yanayozalisha magonjwa

AFYA -madawa ya viwandani---ambayo yanamadhara makubwa kiafya na kusababisha magonjwa pamoja na machanjo yake --badala ya ELIMU ya mitishamba vyakula dawa natural foods na mtindo Bora WA maisha
 
Pia DUNIA haizunguki IPO stationary,ila JUA NA MWEZI vilivyopo angani ndani ya firmament NDIVYO vinazunguka KUPATA usiku na mchana,katika duara la DUNIA flat
 
KILA KITU NA KILA ELIMU ILIOPO DUNIANI IPO KIMKAKATI CHINI YA UTAWALA WA MPINGA KRISTO..kwa manufaa Yao..na LENGO kuu sio kumsaidia mwanadamu ila ni kumiharibu mwanadamu kumfnaya tegemezi DHAIFU mtumwa WA KIFIKRA maamuzi , KUABUDU MFUMO,KUTUMIKISHWA CHINI YA MFUMO

na wao wanaoendresha MFUMO wawe kama miungu(gods)

na wanasema wazi

BILI GATES kuhusu machanjo na madawa na uzazi WA mpango wanasema LENGO NI KUPUNGUZA IDADI YA WATU Duniani

ELON MASK anasema AI na MICRO CHIP AU NEURO LINK DIGITAL ID

ni KUMTAWALA MWANADAMU ,na ku HACK ,haya ma NANO TECHNOLOGY YALIYOPO ndani ya machanjo yakiresoond kwenye wave frequency za 6G wanadamu watakuwa CONTROLED na technology iliyopo ndani yao from within kutokea ndani yao,sio NJE TENA

na wanasema MAROBOTI yanauwezo WA kuua mabilioni ya watu AI NA KUNA WAKATI YATAFANYA MAAMUZI PEKE YAO..na yanaweza ku MISBEHAVE

KITABU CHA ufunuo WA DANIEL ameelezea kuchanganya UDONGO wanadamu na CHUMA MAROBOTI AI na havutashikana kwa sababu vina ASILI tofauti..hii combo ya mwanadamu na MAROBOTI italeta chaos
 
Hata vipaumbele na malengo ya kitaifa mnapangiwa kienndana na malengo ya UMOJA WA mataifa nani wanao ongoza UMOJA WA mataifa ,the beast system MFUMO WA mpinga KRISTO,nani anayemiliki UCHUMI..

Mtawala WA DUNIA hii,kama UKIIPENDA DUNIA ni rahisi KUMTUMIKIA mfalme WA DUNIA hii na UFALME WA DUNIA hii WA beast system.

Kwa KIFUPI HATUKO HURU kivyovyote MFUMO WA SHETANI UNATAWALA DUNIA YOTE MIFUMO YOTE ya DUNIA
 
nakuelewa mtumishi. naomba chombo cha sadaka( niko very serious na hili)

kingine mtumishi naomba niulize kama kuna hii layer Firmament / Dome ambayo ni kama kizuizi mungu ameweka wa ndani wasitoke nje je shetani anawezaje kurandaranda maana kwa ayubu alijiudhurisha kwa Mungu maana kwamba alipita kwenye hii layer si ndio? anapitia wapi?

afu kingine wale malaika walioasi waliwezaje kuvika hiki kizuizi Firmament / Dome na kuweza kuja huku duniani maana kama nimekuelewa vizuri kupenya hicho kizuizi ni mpaka Mungu mwenyewe akufungulie madirisha.

na kingine sijui nitakuwa nje ya mada hawa aliens na reptilians ni viumbe wanao exist kweli kwenye dunia yetu ama ni story tu. na kama ni kweli watakuwa wametoka wapi.

Asante
 
Pia DUNIA haizunguki IPO stationary,ila JUA NA MWEZI vilivyopo angani ndani ya firmament NDIVYO vinazunguka KUPATA usiku na mchana,katika duara la DUNIA flat
halafu wakaja kutudanganya kuwa jua ndio iko centre na kila sayari inalizunguka . kumb jua tunalo sisi tu hapa. Dah basi Mungu aliumbaaaaaa . hapa tunadanganyana na solar system kumbe hatujaona bado mambo yenye ushahidi wa uumbaji wa Mungu. Ni kama mpinga kristo anajaribu kudogosha kazi ya Mungu na uumbaji wake imagine siku tukija kushuhudia uumbaji wa Mungu zaidi ya huu tunaoujua. nasikia zipo mbingu kumi. ahh cant wait na Mungu anisaidie na kunirehemu.
 
Unafikiri kwanini NISHATI YA JUA NA UPEPO NA MAWIMBI YA RADIO AU SAUTI AU UPEPO ,HAYATUMIKI KUZALISHA ENERGY..

kwa sababu HAINA FAIDA kwenye VIWANDA VYA KUZALISHA MAFUTA OIL PETROL..DUNIANI haihitaji NISHATI YA MAFUTA YA PETROL ...lakini for the sake ya VIWANDA BIASHARA ZAO..

KWANINI WANAZUIA WATU KU EXPLORE ANTARCTICA?

KWANINI wanatuletea MBOLEA ZA VIWANDANI...KILIMO haihitaji MBOLEA za VIWANDANI kwa sababu ya VIWANDA VYAO VYA MBOLEA.

KWANINI DR SEBI na wataalamunwa DAWA ZA MITISHAMBA WALIOWEZA KUTIBU UKIMWI,KISUKARI NA MAGONJWA YOTE KWA MITISHAMBA WANAUWAWA...kwa sababu ya FAIDA za VIWANDA VYAO VYA MADAWA NA MACHANJO.

MAGONJWA YOTE YANATENGENEZWA ili WAFANYE BIASHARA YA MACHANJO NAADAWA YAO YA VIWANDANI...Mungu haleti magonjwa..magonjwa yanaletwa na shetani na washirika wake..

KILA MFUMO INAOENDELEA DUNIANI UMETENGENEZWA NA MPINGA KRISTO BEAST SYSTEM kwa manufaa Yao ...na KUMFANYA MWANADAMU MTUMWA WA KIFIKRA LIUCHUMI KILA ANGLE
 
.
 

Attachments

  • 51819.jpeg
    51819.jpeg
    143.6 KB · Views: 2
CHINA WANAFUNDISHA WATOTO WAO JINSI YA KUYATAWALA MAZINGIRA YAO NA KUONGEZA TIJA KATIKA MAISHA YAO NA KUTOA MAJIBU YA MATATIZO YA JAMII

HUKU BONGO TUNAFUNDISHANA KUPASUA VYURA NA KUCHORA PANZI

MTU ANAMALIZA CHUO KIKUU KCHWA KIMEJAA UJINGA ANAKOSA AJIRA ....NDIO ANAANZA KUJIFUNZA BODA BODA BAADA YA KUMALIZA CHUO...MWISHO WA SIKU AJALI...

 
Back
Top Bottom