Uongo ambao dunia inauamini kuwa ni ukweli

Uongo ambao dunia inauamini kuwa ni ukweli

KWAMBA X-MAS CHRISTMAS NI DECEMBER 25 BADALA YA MWEZI WA NISANI 1 APRIL 1
Wachungaji Kondeni: Luka 2:8 inasema usiku wa kuzaliwa kwa Yesu, wachungaji walikuwa kondeni wakilinda mifugo yao usiku. Kijiografia, mwezi Desemba huko Yudea ni kipindi cha majira ya baridi kali, mvua nyingi, na wakati mwingine theluji. Wachungaji wasingeweza kukaa nje usiku kucha na kondoo.



Mwezi wa Nisani (Machi/Aprili) ni majira ya masika (spring), ambapo hali ya hewa ni ya joto na ndio msimu wa kondoo kuzaa, hivyo wachungaji walikesha nje kuwasaidia kondoo wanaozaa.

Yesu ni mwanakondoo,na tunaona wachungaji wa kondoo waliokuwa kondeni usiku wakisubiri kondoo wao wazae wanakondoo,ndio walikuwa WA kwanza kupewa taarifa ya kuzaliwa mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu(Yesu)

Kitabu cha Kutoka kinasema kuwa Hema la Kukutana (mahali ambapo utukufu wa Mungu ulishuka na kukaa kati ya wanadamu) lilisimamishwa rasmi siku ya 1 Nisani (Kutoka 40:2).

Cahn anabainisha kuwa kuanzia wakati Musa alipopewa maelekezo mlimani hadi kukamilika kwa Hema hilo, ilipita takriban miezi tisa—muda unaolingana na mimba ya mwanadamu. Hii ilikuwa ishara ya unabii wa kuzaliwa kwa Yesu, ambaye ni Mungu aliyefanyika mwili na "kufanya hema" kati yetu.

Mwaka Mpya wa Kidini: Katika Kutoka 12, Mungu aliwaambia Waisraeli kuwa mwezi wa Nisani (mwezi wa Pasaka) utakuwa "mwanzo wa miezi" kwao. Cahn anajenga hoja kuwa ikiwa Masihi ndiye mwanzo mpya wa ukombozi wa mwanadamu, ni sahihi kabisa kuwa alizaliwa siku hiyohiyo ambayo Mungu aliiweka kuwa mwanzo wa mambo mapya.

Asili ya Desemba 25: Cahn anasema tarehe hii ililetwa na Kanisa la Kiroma karne nyingi baadaye ili kufunika sherehe za kipagani za Waroma kama vile Saturnalia (sherehe ya mungu wa jua) zilizokuwa zikifanyika kipindi hicho cha baridi, kwa lengo la kuwavuta wapagani wengi kuwa Wakristo.

Kalenda ya GREGORIAN calender ni kalenda yenye ASILI ya kalenda ya KIRUMI ya kipagani.

KIJANA Mmoja aliyebahatika kugundua na kuipata biblia ya 1775 imetaja miezi 13 ya kibiblia ,na kwamba Yesu alizaliwa APRIL MOJA ,NISAN 1

DUNIA na yule mwenye kuudanganya ulimwengu wamegeuza kuwa siku ya wajinga DUNIANI KWA lengo la kumpinga KRISTO

Credit kwa JONATHAN CAHN
Link below 👇🏿
 
Back
Top Bottom