Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,351
- 1,372
Mkuu umeona mwenyewe jinsi watu hawa wanavyochangia bila hata kujua mantiki ya hoja ni nini? Mantiki ni kuwa utaratibu huo ni mzuri wa kuomba vyuo unavyoona vitakufaa kwa sababu mbalimbali ikiwemo aina ya kozi utakayo na jiografia ya mahali penyewe. Shida iko kwenye ongezeko la gharama. Wakati wa TCU tuliona wazazi wengi wa kipato cha chini hiyo fee ya 50 thou ikiwahenyesha na sasa wataingia mifukoni zaidi jee wataweza?
Tatizo la wenye fikra potofu kila aandikaye jambo huwa wanadhani anaandika kwa kujipigania yeye mwenyewe. No, sie wengine tumeshawasomesha watoto wetu na wategemezi wengi tuu lakini tunaishi kwenye jamii ambayo tunaijua iko katika dhiki kiasi gani na jaribio lolote la kuwaongezea magumu tutalisemea kwa sauti. Gharama zimeongezeka.
Kinachoshangaza ni kuwa kesho na kesho kutwa mzee wa maamuzi ya kukurukakara akijua kuwa vyuo vinafanya hivyo na kibao kinamgeukia anaweza kusimama jukwaani akasema hakuna sabau ya kuweka fee hiyo kubwa iwe 5000 kwani wanaomba online, kisha hawa wapambe upepo watageuka na kupongeza pia wakati wanakataa sasa hivi kwa vile wanajiangalia wao na sii wengine
Unajua maana ya apllication fee? kuna application fee na kuna admission fee unajua zitofautisha?
FYI application fee lazima ilipwe wakati wa maombi sababu iyo pesa ndo italipa wanaokagua hizo application zako kununulia chai na lunch na stationeries. sasa usipolipa hawa watu watalipwa na nini?
Na hii system ilikuepo kabla ya TCU kuna vyuo vilikua vinachaji 30000 na vingine 50000 na watu waliapply sasa sasa hivi mnalalamika nini wakati nyie ndo mliosema TCU inawapangia vya kusoma?
Application fee inachajiwa vyuo vyote duniani na nyingine unakuta ni gharama kuzidi hata vya hapa Tanzania.
Tusiwe twalalamika bila sababu unafanya research kwanza