Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,484
- 3,400
Hivi nani amekuambia TCU inafutwa au haitaki? Umeelezwa kuwa mfumo mpya unawajibisha, kama ilivyokuwa zamani, mdahiliwa kufikiri kimkakati kabla ya kuamua university ipi aombe kudahiliwa kwa kozi anayoitaka kusoma. universitie zinatakazokosa kupta wanafunzi wa kudahili kuna maanisha jambo moja kubwa; kwamba mbele ya wadahiliwa, universities hizo zinaonekana kutokuwa na hadhi (not competitive) ya kuendesha mafunzo ngazi ya chuo kikuu. Sasa hli si suala la wanafunzi bali wamiliki wa vyuo hivyo. Wewe ni msemaji wao?Ndugu yangu kabla ya kujibu tafadhali jaribu kutafakari angalau kidogo,mnaweza wengi mkawa na sifa stahiki na kuchagua course na chuo kimoja kuzidi uwezo wa chuo husika, na hiyo inatokea hivyo basi, kuwa salama inakubidi huombe zaidi ya chuo kimoja, na kinyume cha hapo pia kuna vyuo vinakosa waomba wa kutosha.
NB : Na kwa faida yako na wanajamii wengine TCU bado ipo na inaendelea na shughuli zake za udahili kwa staili tofauti, baada ya waombaji kujaza maombi yao na kuchaguliwa katika vyuo husika, majina ya waliochaguliwa yatawafikia TCU kwa ya kuhakiki kabla ya vyuo husika kuruhusiwa kutangaza wanamaombi waliochaguliwa.
Source : Tafadhali google Admission Procidure for 2017 / 2018 Admission Cycle.