Uonevu wa Jeshi la Polisi dhidi ya raia

ndunajr

Senior Member
Apr 28, 2015
174
191
Mheshimiwa Rais,
Mheshimiwa Kamanda Sirro,

Polisi wenu wananyanyasa kupita kiasi raia wa Tanzania,raia hawana amani na askari wao,traffick police ndio kilio majanga kupita kiasi mheshimiwa Rais sijui kama ndivyo jeshi la polisi lina maagizo haya.

Pengine minong'ono ya kusema kwa kila fine kutoka kwa dereva,traffick police nae anapata chochote kama bonus.

Hasira kwa wananchi zinaongeza barabarani pamekuwa sio mahala salama kuendesha magari,mataa ya barabarani yamechezewa hakuna taa NJANO kuwaka ni kijani ikiisha ghafla nyekundu askari mbele mkono hataimae fine,alama za zebra nyingi zimefutika ukisimama mahali askari anakuja anakuambia umekanyaga Zebra lete leseni hatimae cheti,ukipita lugalo njia panda ya kawe unakuata kwa komba kuna askari ashakumulika tochi anakuambia kuna kibao cha speed limit ya 50km eti nasikia huwa askari wanakigeuza kisionekane mwenyewe ninejaribu kuangalia kwa umakini sijakiona.

Askari nyinyi ni binafamu tu kama sisi roho zenu mbaya hizo endeleeni kutengeneza uadui na wananchi,kulikuwa na maaskari miaka flani ya nyuma maaskari wenye hekima na busara wanapima kiwango cha kosa tu wanaona hili ni la kumueleimisha tu mtu na kuonya.Kwa sasa hamna kuonya Shida.

Mwigulu Nchemba usitegemee siju moja kutakuwa na ule msaada wa wananchi kwa askari police sababu wanatengeneza chuki na uadui.Mimi hata askari aombe lifti asahau. Muogopeni Mungu enyi askari na sisi ni watu acheni kutunyanyasaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ya police umeyasema, ni kweli, wana matatizo kibao. umejikita zaidi kwa trafic, huko kuna janga lingine. madereva wa nchi ni balaa. nidhamu yao barabarani ni sifuri. hawana tofauti na mpumbavu yeyote akakalishwa kiti cha dereva na kushikishwa usukani.
 
Mm askari aliniomba lift nikamkatalia, nikamwambia gari yangu sio gari ya jeshi la polisi, akakasirika, nikaondoka. Si sheria ni ombi, laweza kukubaliwa au kukataliwa!
 
Mimi huwa nashuhudia wanavyonyanyasa bodaboda...ndio hawa bodaboda wana matatizo yao ila daa ninayoyashuhudia sio mazuri....nguvu hii ingetumika na kupambana na uhalifu pia
 
Hawa ndugu zetu wameonda traffic ndio sehemu ya kutupiga ngeta madereva maana wanacho kifanya nizaidi ya ukabaji maana sikuizi wamejipangia kabisa hauna kosa elfu tano ukipatikana na kosa teni yaan kwa sasa Tz ukiendesha gari hao jamaa wanakuchukulia kama muharifu
 
Back
Top Bottom