Miss Cherry
Member
- Oct 2, 2020
- 36
- 249
Awali ya yote ningependa kuwatakia wana JF heri ya Mwaka mpya na Mwenyezimungu atufanyie wepesi katika shughuli zetu za kila siku, na bila kupoteza muda ningependa kwenda moja moja kwenye lengo la uzi huu.
Bullying in school is a total mess, watoto wetu wanaathirika kisaikolojia kwa ajili ya uonevu unaondelea mashuleni, kibaya zaidi tunaweza kuchukulia kawaida lakini hii kitu ni mbaya na inaweza kumnyima mtoto amani maisha yake yote.
Nakumbuka kipindi nasoma shule ya msingi nilikua na mwili mdogo maana nilikua nasumbua sana kwenye suala la msosi, nilikua sipendi kula kiasi kwamba wazazi wangu walijitahidi kunipa dawa za kuongeza hamu ya kula lakini haikusaidia.
Sasa kuna marafiki zangu walikuwa wananiita “Chaupepo” yaan nilikua naumia lakini sikua na cha kufanya kwa sababu kweli nilikua chembamba mpaka basi, kuna kipindi nikawa sitaki kwenda shule nalia kabisa na kuomba kuhamishwa lakini wazazi wangu waliona hoja yangu ni dhaifu hivyo ilinibidi kuendelea na shule japo sikua na furaha kabisa.
Turudi kwenye current situation, Kama tujuavyo kipindi hiki cha likizo watoto wa ndugu zetu wanakua majumbani kwa maana shule zimefungwa. Basi bwana kipindi hiki cha sikukuu nikaenda kigamboni kuungana na familia ambapo nimepata fursa ya kukaa na kupiga story na watoto wa kaka yangu ambao walikua shule za bweni.
Mimi huwa nina kawaida ya kujenga urafiki na watoto na wananikubali sana na wapo radhi kuniambia chochote wanachokutana Nacho pindi wawapo mashuleni. Kuna huyu Dogo anaumri wa miaka 11 basi kuna kipindi aliteleza koridoni wakati akielekea bafuni na aliumia kiukweli hadi kupelekea kushonwa nyuzi kadhaa kwenye paji lake la uso. Jeraha lilikua kubwa kwaiyo amebaki na kovu linaloonekana sana usoni.
Sasa wakati tunapiga stori za kuhusu maisha ya shule akaniambia “aunt mimi sitaki tena kurudi kwenye ile shule naomba kuhamishiwa shule nyingine kama anayosoma Husein” (kayumba) nilistuka sana nikahisi kuna kitu kibaya cha kikatili anafanyiwa na wenzie ikabidi nimuweke kirafiki zaidi ili aweze kufunguka.
Nilimchukua nikaenda naye chumbani nikamwambia haya mtoto wangu naomba niambie kila kitu kinachokusumbua na usinifiche, siunajua nakupenda ee? Akajibu yes aunt. Akaanza kuongea kwa uchungu mpaka nikaona machozi yanamlengalenga.
“Teacher kaniambia nina makovu kama kibaka, wenzangu baadhi wananiambia mm ni kibaka sitaki tena kwenda shule, ongea na baba nikasome shule nyingine aunt plz I beg you” aisee roho iliniuma sana, yaan dah!
Nikawa najiuliza hivi walimu wengine wanaakili kweli? Unawezaje kumkashifu mtoto kiasi hicho na unajua kabisa alipata ajali tena akiwa katika mikono yenu? Unawezaje kumwambia mtoto mambo ya kipuuzi tena mbele ya wanafunzi wenzie? Ni ukosefu wa weledi au ni utaahira wa aina gani huu?
Nilichogundua ni kwamba tayari huyu mtoto ameshakua affected na hizi bullying, nikaanza kuongea naye kumuweka sawa na kumsihi kwamba yeye ni handsome sana na hao wenzie wanamuonea wivu tu na kwa mantiki hiyo basi awapuuze maana hawajui walitendalo.
To make it short, suala hili ni tatizo sana na tusipokua makini tutakua na kizazi cha ajabu kwa maana mtoto akishazoea kuonewa kuna uwezekano akakua na roho ya chuki na visasi, kuna umri ambao mtoto ni ngumu kusahau vitu, sasa hii inaweza pia kuharibu psychology ya mtoto completely.
Je ulishawahi kupitia majanga kama haya wakati ulivyokua shuleni au hata mtaani, kukashifiwa, kubezwa au hata kudhihakiwa kutokana na muonekano wako eidha rangi, kimo au vinginevyo? Uliwezaje kuepukana au kupambana na hii hali? Karibuni kwa michango zaidi wakuu.
Natanguliza shukrani