Uonevu mashuleni ni janga la kitaifa

Uonevu mashuleni ni janga la kitaifa

Nikiwa darasa la nne Kuna mwalimu wa kike aliwahi kunifukuza kwenye somo lake la sanaa na sayansi kimu, kwasababu nilikataa adhabu yake iliyopitiliza,

Nilipaswa kuinua mawe juu huku nimepiga magoti kwa dakika 60, hakika nilishindwa na kumuomba msamaha lakini alinikatalia, akaunganisha fimbo mbili kwa pamoja anipige kichwani, ikanibidi kukimbia kurudi nyumbani.

kosa langu kupelekea adhabu hiyo nilishindwa kupeleka sanaa ya kamba ya kufungia mifugo yake (alikuwa mfugaji)

Nilirudi shule baada ya wiki kupita, nyumbani nilijifanya naumwa sana hivyo wakaniruhusu kupumzika, hapo shuleni nikamueleza mwalimu wa nidhamu akawa amenisaidia kurudi darasani.

Changamoto iliyofatia yule mwalimu akawa ananitukana darasani matusi hadi ya nguoni, mara nafanana na mbwa nk.

Yule mwl namchukia yeye na kizazi chake.
Wazazi tuwe karibu na watoto kwasababu wananyanyasika na hii huwapelekea kuchukia shule na kuporomoka kitaaluma
Wafunzeni watoto kuwaeleza yanayotokea shuleni. Sasa Kwa nini hukuwaeleza wazazi wako yaliyokusibu?
 
Kuoneana sasa inakuwa mpaka kwenye mfumo wa maisha.
Shuleni huwezi kutofautisha uonevi kati ya wanafunzi Kwa wanafunzi, nawaalimu Kwa wanafunzi wao.
Vyuoni ndio mpaka mambo ya ngono yanaingizwa, wakufunzi wanawaonea wanafunzi.
Mtaani, nako hali kadhalika, hupati kazi, huduma muhimu Kwa sababu mwenye wajibu huo anakunyanyasa na hakuna pa kukimbilia.
Wanasiasa wananyanyasa wananchi, haijalishi Kwa ngazi gani, mpaka rais, anadiriki kutopeleka huduma za muhimu ambazo ni haki ya kila mlipa kodi kisa hakuungwa mkono kwenye uchaguzi.
Jeshini, bila ya kuyatofautisha, kuoneana baina yao, jeshi moja na jingine, na majeshi Kwa ujumla wao dhidi ya wananchi.
Wafanyakazi popote ni kuoneana tu, wafanyabiashara, baina yao wenyewe na pia na wateja.
Wananchi mitaani, baina yao , na pia majambazi na wananchi.
Kina umuhimu wa Katiba, si tu iwe mpya, bali itakayosimamiwa ili mtu yeyote bila ya kujali umri, alindwe, asikilizwe na kuhakikishiwa haki za utu wake.
 
Kuoneana sasa inakuwa mpaka kwenye mfumo wa maisha.
Shuleni huwezi kutofautisha uonevi kati ya wanafunzi Kwa wanafunzi, nawaalimu Kwa wanafunzi wao.
Vyuoni ndio mpaka mambo ya ngono yanaingizwa, wakufunzi wanawaonea wanafunzi.
Mtaani, nako hali kadhalika, hupati kazi, huduma muhimu Kwa sababu mwenye wajibu huo anakunyanyasa na hakuna pa kukimbilia.
Wanasiasa wananyanyasa wananchi, haijalishi Kwa ngazi gani, mpaka rais, anadiriki kutopeleka huduma za muhimu ambazo nivhski ya kila mlipa kodi kisa hakuungwa mkono kwenye uchaguzi.
Jeshini, bila ya kuyatofautisha, kuoneana baina yao, jeshi moja na jingine, na majeshi Kwa ujumla wao dhidi ya wananchi.
Wafanyakazi popote ni kuoneana tu, wafanyabiashara, baina yao wenyewe na pia na wateja.
Wananchi mitaani, baina yao , na pia majambazi na wananchi.
Kina umuhimu wa Katiba, si tu iwe mpya, bali itakayosimamiwa ili mtu yeyote bila ya kujali umri, alindwe, asikilizwe na kuhakikishiwa haki za utu wake.

Kama hujaelewa mada bora uulize
 
Back
Top Bottom