Uonevu huuponda Moyo, huuzunisha, unapovuka mipaka mtu hufikia kiwango cha kuchagua kufa kuliko kuendelea kuishi

Oct 7, 2019
51
156
I can't breath ni kauli ambayo Kama duru za kiusalama hazitacheza vizuri pale

Marekani inaweza kubadili mfumo wa kisiasa au kumuathiri Trump kisiasa kwenye uchaguzi ujao. Bado Hali ya hewa imechafuka mzimu wa George Floyd unataka kuitikisa Marekani. Mtu mmoja tu anayejulikana Kama Dereck ambaye kwa uzembe wake kwa kutokufuata kanuni za Kazi yake amesababisha hasara kubwa Sana pale Marekani.

Tukio hili ni matokeo ya uonevu ambao watu hufanyiwa. Kuna siku niliwahi kuandika kuwa uonevu usiachwe ukakomaa maana huletha athari, hujenga visasi na mwisho wa siku huleta matokeo mabaya Sana. Niliwa simulizi za picha...

Picha ya Kwanza : Ni picha iliyopigwa 29/11/2017 miaka mitatu sasa imekamilika. Ni picha ya Jenerali wa zamani wa Croatia Slobodan Praljak akiwa kwenye harakati za kunywa sumu, sekunde chache baada ya majaji wa mahakama ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu wa kivita kutupilia mbali rufaa yake kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela.

Kabla ya Praljak hajanywa Sumu hiyo ambayo alikuwa kaiweka mfukoni mwa Koti lake alisema kuwa "Praljak hausiki na uhalifu wa Kivita" Kisha akanywa sumu aliyokuwa ameibeba na alikufa muda mfupi baadaye.

Kama mahakama hii itakuwa na makosa juu ya hukumu ya Slobodan aidha kwa kufanya Upelelezi vibaya juu ya kesi yake basi Slobodan ataingia kwenye Kumbukumbu ya Mashujaa waliojiuua kwa kupinga dhuluma na manyanyaso juu yao.

Pichaa ya Pili
Ilipigwa Tarehe 18.12.2010 kule Tunisia ni rais wa Tunisia alipokwenda kumtembelea Bouaziz muda mfupi baada ya kujilipua kupinga manyanyaso aliyofanyiwa na Polisi wa Tunisia. Muda mfupi baada ya kisa cha Bouaziz kutangazwa haikutumia siku tatu tayari Rais wa Tunisia Ben Ali alikuwa ameshaondelewa Ikulu.

Bouaziz anatajwa kama chanzo cha kuhitimisha Uongozi wa Ben Ali pale Tunisia na kuanza kwa mapinduzi yaliyoitikisa North Africa. Ndio mapinduzi yaliyoifanya Libya nayo kutikisika na kuwa kama ilivyo.

FUNZO
Uonevu huuponda Moyo, huuzunisha, unapovuka mipaka mtu hufikia kiwango cha kuchagua kufa kuliko kuendelea kuishi.
Uonevu ukipevuka lolote linaweza kutokea, tuheshimu hisia za watu na tujiridhishe kwa kile tunachotaka kukifanya kabla ya kukifanya.

Tusione Fahari Kuonea, tusiwakebehi walionewa bali tuwafariji na kuwapa matumaini ili hisia zao zipoe. Kwa kufanya hivyo tutawaepusha na maamuzi yenye Athari.

Uvumilivu una Kikomo, Kikomo cha kutokuogopa Risasi au Bomu, tusitayarishe watu kutokuogopa. Tujifunze sisi kwa sisi kuhisi maumivu ya wenzetu walipondeka moyo, walioonewa, wanaotaka kukata tamaa, nk.

Maneno ya faraja ni tiba tosha kwao, Ukiipa nafsi Moja iliyoumbwa na Mungu faraja umempa Mungu Mwenyewe heshima na utukufu. Tujifunze kusamehe, tujifunze kukaa pamoja sisi ni ndugu kabisa.

Mungu wetu wa Mbinguni ampe kila mtu wepesi wa kusikia roho zinazofadhaika kwa ajili ya kuonewa. Mungu awape wepesi wa kusameheana.

Dereck ni mtumishi wa Umma, sisi ambao ni watumishi wa Umma tuna la kujifunza kupitia visa hivi. Tuweke Kumbukumbu ya hivi visa na Mungu atuongoze katika kufanya kazi kwa uadilifu.
Screenshot_2020-06-03 Thadei Ole Mushi Facebook.png
Screenshot_2020-06-03 Thadei Ole Mushi Facebook(1).png
 
Mbaya zaidi watu wakionewa na mifumo yao ya kutoa machungu yao kwa angalau kusema ukaona nayo inaondolewa, kwa wanaojua psychology za malezi na uyawala wa watu wanajua kuna jambo baya lipo mlangoni
 
Jeshi la polisi duniani kote linapaswa kuangaliwa kwa makini sana. Hawa jamaa ukiwaacha hivihivi wanaweza kuumiza watu sana.
 
Kuna haja ya kurejea mfumo mzima wa utoaji mafunzo ktk jeshi la police hata hapa kwetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom