Emanuelkonki
New Member
- Jan 14, 2019
- 4
- 70
MSIKITI WAVUNJWA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM), WAISLAM KUMI NA MOJA (11) WANATAALUMA NA WAENDESHAJI CHUO KIKUU CHA DODOMA WAHAMISHWA (Prof. Petter Msoffe) asimamia kikamilifu zoezi hilo
Tumepokea kwa Masikitiko makubwa sana uhamisho wa watumishi waislamu Chuo Kikuu cha Dodoma uliofanyika ijumaa tarehe 11 January, 2019. Uhamisho huo umefuatia baada ya Amri ya Prof. Msofe DVC ARC (Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) na Acting VC kuvunja Msikiti uliokuwa unajengwa Chuoni hapo.
Viongozi wote waliokuwa waislam Udom wakiwemo ma Lecturers, Administrative Staffs, Lawyers na Directors wamehamishiwa taasisi zingine za umma.
Harakati hizi za kuondoa waislamu hawa zilishika hatamu mara baada ya kifo cha Prof. Edig Beautus Mobofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo kufariki dunia mnamo tarehe 18 Desemba, 2018. Huku jamii ya UDOM ikishutumu kuwa waislamu wamemloga Prof. Mobofu kwasababu ya kusimamisha ujenzi wa MSIKITI hali ya kuwa vipimo vya hospitali vilionyesha kaagua ugonjwa wa kiharusi.
Kufuatia sintofaham hizo mnamo tarehe 9 Januari , 2019 Siku ya. Jumatano, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo aliyeshika nafasi ya Prof. Mobofu naye ni Prof. Peter Msoffe (DVC - ARC) na Acting VC alitoa amri ya kuvunja Msikiti huo kwa madai kuwa kapokea amri hiyo kutoka juu na kisha watumishi hao waislamu kumi na moja kuhamishwa (11). Tunajiuliza amri hiyo iliyotoka juu imetoka juu kwa nani?
Hatuna shaka na kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu mpendwa John Joseph Pombe Magufuli na hatujui kama Mh. Rais anajua hili linaloendelea katika taasis mbalimbali za umma hususani UDOM. Tunamuomba Mh. Rais alitazame hili ktk sura ya kipekee kwani kuachia haya yaliyofanyika yaendelee ni kuleta uhasama na chuki ktk jamii ya wasomi waliobakia Chuo Kikuu cha Dodoma jambo ambalo linaweza kupelekea migogoro ya kidini mpaka kwa wanafunzi. Hivyo ni vyema na busara uhamisho ukatazamwa kwa jicho la kipekee na kuwarejesha watu hawa kuepuka kupandikiza chuki zisizonatija katika jamii ya wasomi..!!!
--------
Uhamisho UDOM
1. Dr. Mariam Khamisi - UDSM
2. Dr. Yusuph Kambuga - ADEM Bagamoyo
3. Dr. Masoud - DIT
4. Dr. Ibuni Kombo -
5. Khamisi Mkanachi - UDSM
6. Mohammed Mwandege - Arusha Atomic Energy
7. Omar Simba - Wizara ya Ardhi
8. Subira Issa Sawasawa - Wizara mambo ya ndani
9. Wema Mbegu - Wizara ya Ardhi
10. Aziz Gendo - Arusha Technical
11. Dr. Mwinyikondo Ameir - UDSM mbeya branch
Pia soma > Gaudensia Kabaka aeleza sababu za kuzuia Ujenzi wa Msikiti UDOM na kuhamisha wafanyakazi wa hapo