Uonevu dhidi ya Waislam UDOM: Msikiti wavunjwa, wafanyakazi wanataaluma 11 wahamishwa

Emanuelkonki

New Member
Jan 14, 2019
4
70
MSIKITI WAVUNJWA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM), WAISLAM KUMI NA MOJA (11) WANATAALUMA NA WAENDESHAJI CHUO KIKUU CHA DODOMA WAHAMISHWA (Prof. Petter Msoffe) asimamia kikamilifu zoezi hilo

Tumepokea kwa Masikitiko makubwa sana uhamisho wa watumishi waislamu Chuo Kikuu cha Dodoma uliofanyika ijumaa tarehe 11 January, 2019. Uhamisho huo umefuatia baada ya Amri ya Prof. Msofe DVC ARC (Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma) na Acting VC kuvunja Msikiti uliokuwa unajengwa Chuoni hapo.

Viongozi wote waliokuwa waislam Udom wakiwemo ma Lecturers, Administrative Staffs, Lawyers na Directors wamehamishiwa taasisi zingine za umma.

Harakati hizi za kuondoa waislamu hawa zilishika hatamu mara baada ya kifo cha Prof. Edig Beautus Mobofu aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo kufariki dunia mnamo tarehe 18 Desemba, 2018. Huku jamii ya UDOM ikishutumu kuwa waislamu wamemloga Prof. Mobofu kwasababu ya kusimamisha ujenzi wa MSIKITI hali ya kuwa vipimo vya hospitali vilionyesha kaagua ugonjwa wa kiharusi.

Kufuatia sintofaham hizo mnamo tarehe 9 Januari , 2019 Siku ya. Jumatano, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo aliyeshika nafasi ya Prof. Mobofu naye ni Prof. Peter Msoffe (DVC - ARC) na Acting VC alitoa amri ya kuvunja Msikiti huo kwa madai kuwa kapokea amri hiyo kutoka juu na kisha watumishi hao waislamu kumi na moja kuhamishwa (11). Tunajiuliza amri hiyo iliyotoka juu imetoka juu kwa nani?

Hatuna shaka na kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu mpendwa John Joseph Pombe Magufuli na hatujui kama Mh. Rais anajua hili linaloendelea katika taasis mbalimbali za umma hususani UDOM. Tunamuomba Mh. Rais alitazame hili ktk sura ya kipekee kwani kuachia haya yaliyofanyika yaendelee ni kuleta uhasama na chuki ktk jamii ya wasomi waliobakia Chuo Kikuu cha Dodoma jambo ambalo linaweza kupelekea migogoro ya kidini mpaka kwa wanafunzi. Hivyo ni vyema na busara uhamisho ukatazamwa kwa jicho la kipekee na kuwarejesha watu hawa kuepuka kupandikiza chuki zisizonatija katika jamii ya wasomi..!!!

--------
Uhamisho UDOM
1. Dr. Mariam Khamisi - UDSM
2. Dr. Yusuph Kambuga - ADEM Bagamoyo
3. Dr. Masoud - DIT
4. Dr. Ibuni Kombo -
5. Khamisi Mkanachi - UDSM
6. Mohammed Mwandege - Arusha Atomic Energy
7. Omar Simba - Wizara ya Ardhi
8. Subira Issa Sawasawa - Wizara mambo ya ndani
9. Wema Mbegu - Wizara ya Ardhi
10. Aziz Gendo - Arusha Technical
11. Dr. Mwinyikondo Ameir - UDSM mbeya branch

Pia soma > Gaudensia Kabaka aeleza sababu za kuzuia Ujenzi wa Msikiti UDOM na kuhamisha wafanyakazi wa hapo
 
Mimi ninakaa Dodoma na Udom kila mara nipo kule kwa kiasi tunajua kitu gani kilikuwa kiktendeka wakati wa prof Kikula na prof Mlacha hakuna asiyejua hata Mkuu mwenyewe anajua kwamba kulikuwa na Udini ulio vuka mipaka.

Kama Waislamu wakitaka kujenga msikiti chuoni tena chuo cha Umma na Dini singine zikidai kujenga makanisa na mahekalu kuktakuwa kuna kusoma au kutangaza dini na madua.

Mbona chuo Kikuu cha st john hakuna msikiti na waislamu wamepewa sehemu nzuri tu ya kufanyia dua.

Mbona CBE hakuna msikiti wala makanisa na kila kitu kinakwenda vizuri bila shida.

Vyuo vyote dodoma havina misikiti wala makanisa isipokuwa chuo kikuu cha st johns na wao hilo kanisa lilikuwepo toka enzi za mkoloni kwa maana chuo hiko ilikuwa shule ya kanisa la Anglikani miaka za 1940 na baadaye kutaifishwa na kuwa shule ya sekondari mazengo na baadaye tena kurudishwa kanisa la Anglikani kwa St John university.

Haya yanayotokea UDOM ni dhambi ya prof Kikula na Prof Mlacha kuendeleza Uislamu katika Chuo hicho kikubwa Afrika mashariki na kati.

Narudia kusema Wailamu wengi walioajiriwa Udom waliajiliwa kimkakati wa kuwainua na kuwaendeleza Waislamu.

Sina uhakika lakini yalisemwa hapo Udom kwamba kuna fist lady mmoja naye anahusika sana na kupandikiza kwa makusudi/kimkakati Uislamu hapo Udom.

Ombi kwa serikali ni kuchuja na kufuatilia kikamilifu mienendo ya chuo kikuu cha Dodoma wakati wa prof kikula na Prof Mlacha (walikuwa ni zaidi ya Miungu watu Hapo chuoni kwa maana prof Mlacha alikuwa Mkuu wa Administration na Fedha na Kikula alikuwa ni Mkuu msaidizi wa chuo juu yake akiwepo Mh Mkapa).

Prof Mlacha ni Mpare. Wapare ni kabila dogo hapa nchini lipo kwenye wilaya moja tu. Lakini chunguza waajiriwa wapare hapo UDOM ndio utashangaa.

Sina chuki na mtu Ila ninachukia sana Ukabila na Udini unawafanya makabila na dini zingine kuwa wanyonge sana katika nchi yao.
 
Tatizo lenu hua mnaleta ubaguzi wa hovyo sana, kujitenga na kutengeneza ka_ uadui ka kijinga. Mimi naunga mkono kubomoa na ningekua karibu hapo ningeshiriki zoezi kikamilifu kabisa. Mkitaka kuswali nendeni sijui mnapaita Makulu au mjini. Shenzy kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
acha chuki za kidini, uislam na waislam wamekukosea kitu gani mpaka kufikia kutoa lugha ya kuudhi kwao na dini yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina chuki na waislam, nimesoma nao kwahiyo nawajua vizuri sana. Nilipo kua form five waliwahi kuleta mtafaruku shuleni shauri ya mambo ya dini. Kwahiyo Msikiti wakajenge nje ya chuo na wakristo vivyo hivyo wakajenge makanisa nje otherwise waombe room kama ilivyo kwa taasisi za elimu karibia zote. Wasije anzisha mavurugu ya hovyo
acha chuki za kidini, uislam na waislam wamekukosea kitu gani mpaka kufikia kutoa lugha ya kuudhi kwao na dini yao?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ni kawaida kwa nyumba za ibada kuwepo maeneo ya vyuo vikuu. Hapo UDOM inakuwaje? Sitaki kuamini kuwa mchora ramani akumbuke kuweka viwanja vya michezo halafu asahau kuweka msikiti, hadi itokee unajengwa na kuvunjwa

Kuna dini 2 au 3 kuu hapa nchini. Na madhehebu zaidi ya 100 sasa kila dhehebu likiruhusiwa kujenga kanisa au msikiti si itakuwa chuo cha theolojia na kupoteza maana kabisa.
 
Kwa maoni ya kawaida tu ndg waislamu hujipenda wenyewe na hii ni hali ambayo ipi katika shughuri na taasisi mbalimbali kwa kuwekana wao huku wengine wakisema ni makafiri, kwa pale UDOM ni taasisi ambayo haitakiwi kufungamana na kikundi chochote, ukisema sehemu za kuabudia waislamu wakijenga msikiti, kuna wasabato nao watataka, mashahidi wa yehova, gwajima atataka eneo, mwingira, lusekelo, lwakatare, katoliki, lutherani, moravian, siloamu, anglikana na wengine wengi ambao kwa namna nyingi hawafungamani ila wanakubaliana kuwa kila mtu anaabudu kwa namna yake. Tukubaliane tu kuwa ile ni taasisi ya elimu sio sehemu ya kukutania kushindanisha dini.
 
Chuo kikubwa kama UDOM ina ramani ambayo iliandaliwa, sasa nyie mkimtegemea mabofu kama ndo mtu wa kuwasimamia mambo yenu hap chuoni huku akikiuka utaratibu kwa kuwa alikuwa na cjeo kwenye uongozi hiyo haikuwa sawa, halafu hamjui kuwa hata kwenye kitabu chenu imeandikwa usimtegemee mtu kwa ajili ya kufanya mambo yako hasa ya kidini, yaani huyo mobofu ndo aliubeba uislam hapo UDOM?
 
Sina chuki na waislam, nimesoma nao kwahiyo nawajua vizuri sana. Nilipo kua form five waliwahi kuleta mtafaruku shuleni shauri ya mambo ya dini. Kwahiyo Msikiti wakajenge nje ya chuo na wakristo vivyo hivyo wakajenge makanisa nje otherwise waombe room kama ilivyo kwa taasisi za elimu karibia zote. Wasije anzisha mavurugu ya hovyo

Sent using Jamii Forums mobile app



Nyinyi au wewe unazungumza kitu usichoelewa, unasema waislamu wapewe Room ili wawe wakiswalia, tayari ukishakuwa na Room kwa ajili ya kuswalia huo ni Msikiti kwa istilahi ya dini ya kiislamu, kulingana na ukubwa wa UDOM, tujiulize ni Room ya ukubwa upi itakayoweza kuchukua hao Waumini wote kwa wakati mmoja mfano katika sikuu za Ijumaa??, na ikumbukwe waislamu wanatakiwa kuswali swala za lazima mara 5 kwa siku.

Kwa mazingira hayo, waislamu wanayo haki ya msingi ya kuabudu, hivyo kama waliomba eneo la kujenga msikiti, je wengine nao waliomba kujenga nyumba zao za Ibada wakanyimwa??!!,ni hapo sasa ndipo Udini unapokuja na sio kwa kujenga msikiti ndiyo udini.

Hao hao viongozi wa serikali utawasikia wakipaza sauti wakiwaomba Viongozi wa dini wawaase waumini wao ili wawe raia wema na wenye maadili, halafu hapohapo hawataki nyumba ya Mungu ijengwe na mbaya zaidi INABOMOLEWA bila khofu!!!, je mkishikwa na laana mtasema Waislamu wamewaroga?!!?.
 
Back
Top Bottom