Unywaji wa pombe una athari mbaya kwenye ubongo, utafiti wabaini

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford wanasema hata unywaji kiasi wa pombe unahusishwa na kuenea zaidi kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali. Utafiti huo umebaini kwamba kiasi chochote cha unywaji wa pombe kinaweza kukuletea madhara kwenye ubongo wako.

Utafi huo uliofanyika kwa kutumia hazina ya sampuli za Ulaya unasema : "Hakuna kiasi salama cha pombe kwa ubongo kilichobainika. Unywaji wa kiasi wa pombe unahusishwa zaidi na kusambaa kwa athari mbaya kwenye ubongo kuliko ilivyotambuliwa awali."

Utafiti huo uliwahusisha washiriki 25,378 kwa kutumia data kama vile umri, jinsia, elimu , ripoti binafsi ya kiwango cha unywaji wa pombe, ukubwa wa ubongo na afya kwa kutumia scan za MRI, taarifa kuhusu hospitali na matibabu ya bila kulazwa, pamoja na vipimo vya kumbukumbu. Pia ulibaini kuwa unywaji wa pombe ulichangia kwa kiasi kikubwa athari nyingine zilizosababishwa na mambo mengine, ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara.

Walibaini kuwa hapakuwa na kiwango "salama" cha unywaji wa pombe, ikimaanisha kuwa unywaji au kiasi chochote cha pombe ni kibaya kuliko kutokunywa kabisa pombe. Walibaini pia kwamba haijalishi unakunywa aina gani ya pombe. Na kwamba hali fulani alizonazo mtu kama vile shinikizo la juu la damu, unene wa kupindukia wa mwili, vinaweza kuwaweka watu katika hatari ya juu. Watafiti waliongeza.

Wataalamu wa magonjwa ya ubongo wanasema wakati bado hatujapata dawa za tiba kwa magonjwa yanayoathiri ubongo kama dementia, kufahamu juu ya mambo yanayoweza kuzuia madhara ya ubongo ni muhimu kwa afya ya umma.

Source: BBC
Wafunge viwanda vya pombe basi.
 
Back
Top Bottom