Tunaomba muangalie na hizi Microfinance zinazo kopesha, riba imekuwa kubwa sana watu wanaumia especially na apps mfano wanajiita flying shilling ili uweze kupewa laki mbili ni lazima ukope laki 4 na urudishe ndani ya siku sita ukichelewesha watu wanapewa vitisho tunaomba na BOT wajulishwe.
Ushahidi ni huu hapa. Wenye apps hizi ni wachina tunaomba mfuatilie ila wafanyakazi ni watanzania na polisi hata wakipelekwa hawakai huwa wanatolewa na wakitoka wanabadilisha jina lakini ni watu hao hao
Na vi Apps vingine ni Kamata pesa, Yako Mkopo e.t.c
Wanakuvutia kwa matangazo ya kiasi kikubwa cha mkopo kwa riba nafuu na muda wa marejesho kuwa mrefu lakini kiuhalisia baada ya kuwapa taarifa zako wanatoa mkopo kiasi kidogo sana mfano kutoka 1 Mil mpaka 100k na kukutaka ulipe kwa muda wa hata siku 3 kwa riba ya zaidi ya 40%.
Ukiwasumbua kulipa wanaanza kukutisha na kuwapigia watu mbalimbali uliowaweka kama watu wa karibu na kukuchafua kuwa wewe ndiye tapeli wa mtandao.
Mtaendelea kula block zangu pande zote mpaka WhatsApp mpaka akili iwakae sawa.
Tala Tanzania pekee ndiye alikuwa muaminifu wa kuzingatia makubaliano.
Vyombo husika fuatilieni hao wakopeshaji kwa njia ya mtandao (Apps)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.