Unyama wa Serikali Iringa Vijijini

Nimepata habari Serikali imeamua kuwanyang'anya na kuvunja nyumba za wananchi wa vijiji vya Kibengu, Wami, Usokami, Mapanda, Ilogombe nk bila kuwapa sehemu mbadala ya kwenda.

Mbunge wa Iringa Vijijini Ndugu Mgimwa ameitisha kikao jana tarehe 19/03/2012 na baadhi wa wanakijiji na kuwaambia Rasilimali ya maeneo hayo yalishauzwa toka Mwaka 1976 hivyo maeneo hayo yatachukuliwa na wenye kumiliki rasilimali.

Wananchi wa maeneo hayo wako hapo toka enzi na enzi leo Serikali inawaambia maeneo yao yameshauzwa toka 1976 bila wao kushirikishwa wala kupatiwa fidia, mbaya imewaambia watafute pa kwenda.

Kwa mfano kijiji cha Kibengu - Mgwao kina nyumba takribani 300 na wakazi wapatao 4,000 wametaarifiwa waondoke kuanzia kesho maana wakati wowote nyumba zao zitavunja.

Je ni kwa namna gani wananchi hawa watasaidiwa?

Naomba kuwakilisha


Wanyalukolo bado wamelala hawapendi kuiga wenzao wa Iringa Mjini waliomchagua Pastor Msiigwa. Nyie na watu aw Morogoro hata wakiwafukuzia Baharini ni sawa tu mtie akili ili 2015 msilogwe mkaichagua CCm. Kuchagua CCm mtahamishwa Kama mifugo na nchi wataiuza kwa wahindi Juzi Jakaya Kikwete ameanzisha kampain ya kuwauzia Akina Somji and Sons Hecta tano tano waendeleze ndoto yake ya kilimo kwanza na Leo kusema waanzishe Benki ya ushirika eti wakulima wapate mikopo yenye RIBA nafuu. Huyu ni juha serikali ya Nyrere ilianzisha CRDB Mkapa akaibinafsisha tatizo la CCM hawajui uchumi. Cha kufanya sio kuanzisha utitiri aw Benki Mara ya akina Mama Mara ya Vikoba Mara ya vijana! This is rubbish just let BOT do it's Regulatory work let them control interest rates. Akina Jakaya na serikali yake sijui walisoma wapi uchumi? Elimu haina regulator hivyo hivyo Kila ambacho mafisadi walichoshikilia no regulation hivi Huko CCM kuna watu au misukule sishangai Masaburi kusema wanafikiria Makalio?
 
Kesho nitawapigia hakika.

Pia kwa wale niliowasiliana nao nimewapa elimu ya uraia wakaelewa somo nimewaambia wawaelimishe na wengine


Jitahidi sana ndugu,

Ukiweza kufanikisha hilo na kuzuia uonevu kwa watu ambao wanaonewa kwa sababu ya ujinga walo. utakuwa umetoa mchango mkubwa sana...!!

Kwa sasa wanahitaji msaada badala ya lawama.....

Kila la heri ndugu,
 
huo ndoo mshahara wa kuchagua ccm maana watu hawa wanajifanya hicho ndo chama kilicho wakuza elim ya uraiya 2014 ichukue hatam chandema huyeee hao wananunuliwaga KOMONI wanatoa kura wacha wakome ndoo watajuwa joto ya jiwe:wink2:

Unajua nini vangilichuma? Hawa wananchi uelewa wao kuhusu upinzani ni mdogo sana wanahitaji kuelimishwa vya kutosha. Bado wana ule ushabiki kama wa Simba na Yanga. Lakini kwa hili wataelewa tu somo
 
Saaafi sana. Wacha pengine Watanzania tutaamka kwenye usingizi wa pono tuliolala. Mtu tunauawa kila siku na polisi, sisi tawire, tunanyanganywa ardhi, sisis tawire... tunafanyiwa kila aina ya ufisadi na kebehi, sisi tawire.... sasa unategemea nani atuonee huruma?

Maoni yako ni mazuri,lakini naomba nikusihi uwe mvumilivu,mwaka 2015 tunakwenda kubadilisha siasa za huko kwetu,unajua sisi tumeamua kutema mate kwa magamba[tufunyite yisisiemu],MGIMWA NA WENZIE WAMALIZIE UFISADI WAO].MKWAWA SHUJAA TUTAMTUMIA 2015.
 
Maoni yako ni mazuri,lakini naomba nikusihi uwe mvumilivu,mwaka 2015 tunakwenda kubadilisha siasa za huko kwetu,unajua sisi tumeamua kutema mate kwa magamba[tufunyite yisisiemu],MGIMWA NA WENZIE WAMALIZIE UFISADI WAO].MKWAWA SHUJAA TUTAMTUMIA 2015.

Mkuu waelimishe ndugu zako wananyanyasika sana kule. Mimi na wewe ndio tutakaoamsha watu hawa kutoka usingizini
 
Back
Top Bottom