Unyama wa Serikali Iringa Vijijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyama wa Serikali Iringa Vijijini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimox Kimokole, Mar 20, 2012.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimepata habari Serikali imeamua kuwanyang'anya na kuvunja nyumba za wananchi wa vijiji vya Kibengu, Wami, Usokami, Mapanda, Ilogombe nk bila kuwapa sehemu mbadala ya kwenda.

  Mbunge wa Iringa Vijijini Ndugu Mgimwa ameitisha kikao jana tarehe 19/03/2012 na baadhi wa wanakijiji na kuwaambia Rasilimali ya maeneo hayo yalishauzwa toka Mwaka 1976 hivyo maeneo hayo yatachukuliwa na wenye kumiliki rasilimali.

  Wananchi wa maeneo hayo wako hapo toka enzi na enzi leo Serikali inawaambia maeneo yao yameshauzwa toka 1976 bila wao kushirikishwa wala kupatiwa fidia, mbaya imewaambia watafute pa kwenda.

  Kwa mfano kijiji cha Kibengu - Mgwao kina nyumba takribani 300 na wakazi wapatao 4,000 wametaarifiwa waondoke kuanzia kesho maana wakati wowote nyumba zao zitavunja.

  Je ni kwa namna gani wananchi hawa watasaidiwa?

  Naomba kuwakilisha
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tutafutie japo ka-picha basi ndio tupate cha kujadili zaidi humo mkuu, pamoja!!
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Saaafi sana. Wacha pengine Watanzania tutaamka kwenye usingizi wa pono tuliolala. Mtu tunauawa kila siku na polisi, sisi tawire, tunanyanganywa ardhi, sisis tawire... tunafanyiwa kila aina ya ufisadi na kebehi, sisi tawire.... sasa unategemea nani atuonee huruma?
   
 4. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Siku ya wajinga ni tarehe 1 april. Habari hii si ya kweli. Kwasababu nyingi tu. Kibengu iko mufindi na si iringa vijijini na mgimwa si mbunge wa iringa vijijini, hakuna jimbo la uchaguzi la iringa vijijini wala mgogoro wa kunyang'anya watu ardhi yao. Mgimwa tunaemfahamu hawezi kuvuruga watu kiasi hiki.
   
 5. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu mi niko Dar nimepigiwa na mtu aliyeko huko leo hivyo sijapata picha ya kuweka hapa
   
 6. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndio ni Mufindi mimi nimezoea kuita Iringa Vijijini kwa sababu ni vijijini sana

  Mapenzi yako kwa Serikali ya CCM yasikupofushe macho Mkuu. Huko ninakokwambia kuna mtu wangu wa karibu. Ni Kibengu - Mgwao baada ya kupita Usokami Mission Hospital. Ninaongea nililo na uhakika nalo kwa 100%

  Mpigie simu mbunge Mgimwa muulize kuhusu hili na kikao alichofanya tarehe 19.03.2012 Kitongoji cha Mgwa Kata ya Kibengu
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hadi hapo wananchi wa maeneo hayo watakapojua thamani ya kura yao ndipo hayo manyanyaso yatakwisha! lakini wakiendelea kuthamini Tshirt na khanga basi kazi kwao!
   
 8. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu wananchi wa huko wana hali mbaya sana kimaisha, hawajui hata pa kwenda baada ya kuambiwa waondoke haraka iwezekanavyo hapo wanapoishi toka enzi za mababu zao
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nenda ka-check tena facts, mwaka 1976 hakukuwa na uuzaji wa Rasilimali. Unless useme kwamba labda serikali ilichukua eneo hilo na kulifanya hifadhi or something else kama Ranchi. Halafu zilipokuja sera holela za Mkapa akawauzia wawekezaji ambao wengi wao huko wanatafuta ardhi.

  Pia kumbuka kwamba zama za utawala wa Nyerere hakukuwa na swala la umiliki wa ardhi kubwa in terms of eneo au mashamba. Sasa hivi ndio kuna watu wanamilikishwa ardhi kubwa ya mashamba. Zama hizo ardhi ilikuwa ni mali ya kijiji kizima.

  Kwa hiyo kwa kutumia kigezo cha huo mwaka, kuna walakini wa habari hii. Pia kwa sheria za sasa linapokuja swala la kuuza ardhi kwa mwekezaji, serikali ya kijiji huwa inashirikishwa hatua kwa hatua, japo kuna wajanja wachache ambao hutumia wana siasa ili kufanikisha hiyo agenda ya kujipatia ardhi.
   
 10. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Basi ni wakati mwafaka wa kuwapatia elimu ya uraia ili ifikapo 2014 wachague viongozi wa wananchi na si viongozi wa mafisadi kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na then, wamalizie mwaka 2015 kuchagua mbunge wakuwatetea siyo huyo anayewapa taarifa kuwa eneo lao lishauzwa tangu 1976! bila kueleza kachukua hatua gani kuwatetea wapiga kura wake.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Maandamano ya kwenda kumwondoa Rais ikulu shaanza kunukia.
   
 12. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wacha wavunjiwe labda watatusikia kwamba CCM ni wabakaji wa haki na hawatakiwi kuendelea kutuongoza,
  huko njombe wamesha ambiwa sana wameshupaza shingo zao nakumchagua bi kiroboto
   
 13. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani sasa wataanza kuelewa!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Jitahidi mkuu upate details zote kuhusiana na hii issue halafu uwasiliane na watu wa Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa msaada zaidi. Pia jitahidi kuwasiliana na baadhi ya media. Naamini watasaidia.

  Contacts za LHRC ni hizi hapa,

  HQ – Justice Lugakingira House
  Kijitonyama, Behind Institute for Social Work
  P.O. Box 75254
  Dar es Salaam
  Tanzania
  Tel: +255 22 2773038/48
  Fax: +255 22 2773037
  E-mail: lhrc@humanrights.or.tzWebsite: www.humanrights.or.tz

  Arusha Sub-Office:
  Engira Road, Plot No. 48
  P. O. Box 75254 Arusha
  Tel: +255 27 2544187
  E-mail: lhrcarusha@humanrights.or.tz

  Legal Aid Centre – Justice Mwalusanya House
  Isere St. Kinondoni
  P. O. Box 79633
  Tel: +255 22 2761205/2761215
  Fax: +255 22 2761219
  E-mail: legal@humanrights.or.tz

  Legal And Human Rights Center
   
 15. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi naongea kile wananchi walichoambiwa kwenye mkutano, hizi nyimbo zako wale wanakijiji hawazielewi.

  Hebu mpigie simu Mgimwa umuulize hawa wananchi wa vijiji hivi anawapeleka wapi?
   
 16. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wameripoti vibaya kwako. Tuna watu pale kibengu. Pale kuna mgogoro wa mpaka kati ya kilolo na mufindi mgogoro ambao unakuzwa na wanasiasa kwa hofu ya kukosa kura za kutosha. GN inaonesha eneo hilo liko kilolo ingawa wapiga kura wameandikishwa kama wapiga kura wa mufindi. Anachosema mbunge ni kuwa atalirejesha eneo hilo mufindi na si kuhamisha watu kwa maelezo ya kuuzwa ardhi. Kumbuka pia kuwa tarafa ya kibengu imeanza mwaka 1952 na vijiji vyake vimesajiliwa kisheria.
   
 17. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shukran Mkuu nishawaandikia hili
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kama hutajali, wapigie simu kabisa...huwa wako makini kusaidia!!
   
 19. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kesho nitawapigia hakika.

  Pia kwa wale niliowasiliana nao nimewapa elimu ya uraia wakaelewa somo nimewaambia wawaelimishe na wengine
   
 20. v

  vangilichuma Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huo ndoo mshahara wa kuchagua ccm maana watu hawa wanajifanya hicho ndo chama kilicho wakuza elim ya uraiya 2014 ichukue hatam chandema huyeee hao wananunuliwaga KOMONI wanatoa kura wacha wakome ndoo watajuwa joto ya jiwe:wink2:
   
Loading...