Eng Kimox Kimokole
JF-Expert Member
- Jun 9, 2010
- 1,041
- 772
Nimepata habari Serikali imeamua kuwanyang'anya na kuvunja nyumba za wananchi wa vijiji vya Kibengu, Wami, Usokami, Mapanda, Ilogombe nk bila kuwapa sehemu mbadala ya kwenda.
Mbunge wa Iringa Vijijini Ndugu Mgimwa ameitisha kikao jana tarehe 19/03/2012 na baadhi wa wanakijiji na kuwaambia Rasilimali ya maeneo hayo yalishauzwa toka Mwaka 1976 hivyo maeneo hayo yatachukuliwa na wenye kumiliki rasilimali.
Wananchi wa maeneo hayo wako hapo toka enzi na enzi leo Serikali inawaambia maeneo yao yameshauzwa toka 1976 bila wao kushirikishwa wala kupatiwa fidia, mbaya imewaambia watafute pa kwenda.
Kwa mfano kijiji cha Kibengu - Mgwao kina nyumba takribani 300 na wakazi wapatao 4,000 wametaarifiwa waondoke kuanzia kesho maana wakati wowote nyumba zao zitavunja.
Je ni kwa namna gani wananchi hawa watasaidiwa?
Naomba kuwakilisha