figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Hii hatari sana!! Mwanaume anayejulikana kwa jina la Remy Joseph (35) anashikiliwa na polisi kwa kumchinja mke wake wa ndoa kabisa aitwaye Josephine Ndengaleo Mushi waliyeishi naye miaka 10 na kuzaa watoto wawili. Tukio hilo la kutisha lilijiri ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya Hotel Friend's Corner Ltd iliyopo Manzese Argentina, Dar ambapo walikuwa wamechukua chumba katika hoteli hiyo kwaajili ya kulala hapo.
Polisi walifanya uchunguzi chumbani na kugundua kuwa, marehemu Josephine alichinjwa shingoni, akakatwa mbavu mbili, moyo na maini vilikuwa nje ‘vikimwagika', mwisho alichomwa kisu utosini.. Cha kusikitisha zaidi, mwili wa marehemu Josephine ulipigishwa magoti, sehemu ya miguu mpaka magoti ikiwa sakafuni na kifuani kulalia kitanda. Halafu ulifunikwa shuka
Katika hali iliyoonesha kuwa, mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitaka kujinyonga, polisi walikuta waya wa umeme wa tivii ukining'inia kwenye pangaboi lakini ukiwa umekatika. Na pia damu na alama za kujikata visu shingoni.
Sababu ya kufanya hivyo haijujulikana ila ndugu wa mke wa marehemu walielezea kuwa mme alikuwa akimhisi vibaya mkewe.
R.I.P Josephine Mushi