University of Dodoma - Photos !


hivi unalipwa nshilingi ngapi kwa kuanza kampeni mapema!!!mbona houngelei daraja alilosema atalijenga mto kilombero within 2 years za madaraka yake...
 
Saa nyingine huwa tunaponda lakini kwa hili amefanya kazi nzuri sana kwa wale wenye moyo safi sio kila kitu cha kuponda tu jamani
 
JK ni mtekelezaji tu, hiyo yote ni plan ya Mkapa! Mbaya zaidi hiyo ndiyo plan pekee ambayo Mkaapa aliiacha na JK ameikamilisha. Barabara zilizokuwa vipande vipande ameshindwa kuzikamilisha japo pesa zilikuwepo!
Tuwe wakweli na tusifu pale panapotakiwa kusifu,sio kwasababu wewe si mlokole basi Kakobe akifanya Jema lazima ulishambulie!Udom ni zao la JK na kwa ushahidi onana na Profesa M.Luhanga aliyekuwa VC wa UDSM.Penye ukweli uongo ujitenga,tatizo ni kuchukia watu hata kama ndiye anayekulisha(huo pia ufisadi),badilika mwanajamii!!!!!
 
Nijuavyo pesa za Chuo hiki ni collection kutoka sehem tofauti sio Gates pake yake.
Pale UDOM ukifika sehem kubwa ni NSSF, then mifuko mingine ya Hifahi like PFF, PSPF etc...
Funds za hapo wahusika labda mradi ukishakamilika ndio watuambie.

Let us say kama pesa za Kujenga UDOM nazo zingeliwa kama EPA tungesemaje au kama za KILIMO Kwanza zilivyoanza tafunwa?

Kwa Usimamizi wa hili la UDOM JK ameacha Landmark. si pekee na wote ambao wamepewa Jukumu la Kusimamia. Binafsi nilipita UDOM japo kwa muda mfupi.

Kuhusu Ubora wa Majengo hapo sasa wahusika wawe makini Mapema. ..kutoka Uongozi wa UDOM hadi wahusika wa MIFUKO na wadau wengine.
 
Chuwa na wengine:
Akijenga na kusimamia, si ndiyo kazi yake?

Tunamlipia safari za nje hadi na familia yake. Anatesa na magari ya bei mbaya na kuvaa suti kali kali. anakula na kulala vizuri na kuwa na ndege yake. Akimaliza kazi bado ataendelea kutesa kabla ya mjinga mmoja kuja kuwapeleka Mahakamani yeye na Mkapa na ukimalizia na Mwinyi kwa kuuza Loliondo. Kama asipokuja, basi wataendelea kutesa hadi siku Malaika Jibril atakuja kuwachukua.

Sasa unafikiri hivi vyote anapata bure? Afanye kazi na zaidi ya hiyo. Ilitakiwa kuwa kunajengwa kila sehemu. Badala ya kuangalia mechi na kupiga gumzo na Drogba, alitakiwa kuwa kwenye mafuriko na wanajeshi kuwaamrisha waanze kazi ya ujenzi mara moja hata kama daraja la muda (JWTZ nina uhakika wana uwezo ila sijui kama huyu bwana anafahamu).

Hii kitu ya Chimwaga ilianza siku nyingi sana. Hawa akina PPF sijui wakiongezewa pesa na Bill Gates wamekuja kumalizia. Sijui yeye anahusika hata vipi na sijui hata kama ana uwezo wa kuingilia pesa za hao jamaa. Nina imani angelikuwa anaweza, basi kungelikuwa na ka EPA kengine. Mbona pesa za ujenzi wa barabara CHALINZE- MSATA ambako ndipo yapo mahekalu yake zimeliwa? Tena kuna member aliandika kuwa ni mdogo wake (Kikwete Jr) alihusika kuziepa hizo hela.

Sijui tumsifu kwa lipi. Kuwa wamemnyima kuweka mkono wake (CCM kwa ujumla) na sasa kazi imeonekana? I wish wangeliondolewa kabisa madarakani na hao wajenzi wa UDOM ndiyo wawe watawala nchi, nina imani tungeliona hadi foleni za Dar zinapungua mwaka hadi mwaka.
 

Hakuna aliyebisha kuwa ahadi nyingi za JK hazijatimia.,nilichosema mimi ni kwamba hii ni moja ya ahadi iliyotimia, si unakumbuka kabla hajachaguliwa chuo hiki hakikuwepo kabisa..? usiwe mgumu wakuelewa ndugu yangu..,tushukuru hata kwa ili ingawaje bado tunamdai mengi.
 


Ndio majibu ya maswali hapo juu? Umetukana watu hapa then majibu huna tukuitaje one of the great thinkers? Kama hujui usiropoke tu. Hiyo haikuwa ahadi ya Kikwete Finito - Finished - Kwishnei - Peleka hizo ngonjera somewhere else.
 
Miti na majani hayaoti hapo? Au picha za zamani tu hizi. Wakiotesha mimea kuzingira chuo watakuwa wamekamilisha mandhari niipendayo mimi. Kwasasa panaonekana kama research department fulani hivi kwenye moja ya majangwa pasipokuwa na jamii yoyote inayozingira!
 
Namshukuru aliyepiga picha. Swali ni kwamba is the university only buildings? Angetuonyesha laboratories and library ndio tujue kweli wanajitahidi, laniki structures means nothing.
 
majengo mazuri lakini je chuo ni majengo au ubora wa elimu. let's see. its too early to judge
 

Wewe Si mbongo kama huelewi hata nani aliyeanza na plan ya hicho chuo. SI Kikwete ni Mkapa Ndo aliye initiate hiyo project.
 
Jama Mkuu wa chuo hicho amejibu maswali yote ambayo yalikuwa yanaulizwa na juu ya ufadhili wa chuo hiki, Ila ni Pesa za Watanzania na hivyo kuhusu walimu ni janga la kitaifa maana hata baadhi hata vyuo vingine navyo havina walimu
 
Only kitu cha kujivunia............JK baada ya hapo anakumbatia washikaji...
 
Wana JF, Taarifa nilizo nazo kwa kifupi ni kuwa anayejiita Mtume Mwingira wa Kanisa moja pale Mwenge amefanya ubabe wa kuvunja na kuharibu mali za wawekezaji wa eneo lililo jirani na Kanisa lake na kupora ardhi kinyume cha sheria. Ninaomba mwenye taarifa za kina kuhusu suala hili atujuze. Ninasikia anajenga mnara wa kurushia matangazo ya TV yake. Je sheria Tanzania zinasemaje kuhusu hili? Tusije tukawa na matatizo ya watu wenye madhehebu mbalimbali kupindisha sheria kwa ajili ya 'dini'.
 
Utamsifu JK kafanya nini wakati hela katoa bill gates tena wakati wa Nkapa...Jk tunataka miaka 5 ijayo aseme atafanya nini kama kujenga uwanja wa netball au nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…