Ungepewa nafasi ya Raisi nini ungefanya katika hali ya nchi ilivyo sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungepewa nafasi ya Raisi nini ungefanya katika hali ya nchi ilivyo sasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shapu, Sep 15, 2009.

 1. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kutokana na mijadala inayoendelea humu ndani. Nilitaka kujua mawazo ya watu kwamba nani angefanya nini na kwanini katika hali ya nchi kama anavyoiona mtu. Nafikiri hili nalo laweza kuibua changamoto kwa viongozi wetu. Napenda watu watoe IMMEDIATE measures tuu. Then tujadili tuone kama zinaweza saidia kupunguza matatizo tuliyonayo.

  Binafsi Ningefanya yafuatayo kwa kuanzia:

  1. Najitafutia ulinzi wa hali ya juu na wa kuaminika ya watu watakao nilinda hata ikiwezekana nakodisha nje.

  2. Natangaza hali ya hatari nchi nzima "state of emergence" - Swala hili litaniwezesha kufanya mabadiliko ya haraka bila kupata vipingamizi vya kisheria na kikatiba. Mfano kumfukuza Jaji Mkuu, Kumfukuza Mwanasheria Mkuu, Kumfukuza Bosi wa PCCB, Kumfukuza CAG etc

  3. Nita design mifumo (systems) mipya au kuboresha iliyopo na kuteua wasimamizi ninaowaamini kuhakikisha inafanya kazi. Hapa sitacheka na mtu ni swala la kufuata taratibu kama zilivyoainishwa kwenye katiba, sheria etc au mtu anaipata atakapo kwenda against. Itajumuisha kuidentify watanzania wachache wenye uwezo mkubwa kuendesha hii mifumo. Kwenye hili la kuidentify hata nikichukua gharama kiasi gani it does not matter swala ni ku-identify watanzania wenye uwezo irrespective of chama. Moja kwa moja Mtu kama Magufuli hatakosekana kwenye team yangu.

  Hivi vitakuwa vipaumbele vyangu vya kwanza....
  Naomba nione michango yenu. Mnafikiri vipi kuhusu hili au ungeanza na nini? WEWE UNGEFANYAJE?

  Ni katika harakati za kuamsha fikra endelevu.
   
  Last edited: Sep 15, 2009
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Katika uundaji wa mifumo:
  Ningefutilia mbali cheo cha U-DC na U-RC. Kwani wakurugenzi wa wilaya na mikoa kama wapo wanatosha. Swala la ufungaji wa ndoa lingishia kwa mashehe, wachungaji na mapadre ie viongozi wa dini au ktk halmashauri na si ma DC wanaongeza tuu gharama.
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Sep 16, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa Rais,vitabu 19 vya Lobsang Rampa,ninetafuta nafasi ya kuviweka katika mitaala ya masomo ya shule za Sekondari,katika somo la dini.
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Nitamtaka CAG aripoti moja kwa moja kwangu. Atakuwa na uhuru wa kufanya kazi independently kiasi kwamba anao uwezo wa kuajiri makampuni makubwa ya nje ya kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za serikali na any findings zinasimamiwa na utekelezaji unafanywa withing very short period of time.
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Nitafutilia mbali TAKUKURU kwani sioni inafanya kazi gani, na nguvu zote nitaziweka kwa CAG.
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Nitaongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikalini iwe na uwiano stahili na mishahara ya makampuni binafsi. Ambapo nitafuta allowance zote kama za mikutano na warsha. na nyingine zote ambazo hazina tija kwa taifa.
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Umenena. Zaidi ya hayo mimi nigefutilia mbali:-
  1: vibali vyote vya uwekezaji ambao hauna tija kwa Taifa

  2:Viongozi wote ambao kwa namna moja au nyingine wameusika au kutajwa kwenye kasfa zozote zile

  3:Ningefukuza wageni wote ambao wanafanya kazi ambozo wa Tz wanauwezo nazo, hii ikiwa ni pamoja na wageni wote ambao wanafanya biashara ndogondogo. (Nigeruhusu wageni wafanye biashra za jumla na wananchi wafaye biashara za rejareja ikiwa ni pamoja na za jumla kwa wale watakaoweza

  4:Ningeuza magari yote ya Serikali ambaya ni ya kifahari yanayogharimu pesa nyingi kuyahudumia, na kuweka utaratibu wa kila kiongozi kutumi magari ya serikali yenye gharama nafuu na gharama za kuliudumia ilo gari zitakuwa kwenye mshara wake. Hii itapunguza matumizi yasiyo ya lazima

  5: Kila kiongozi atawajibika kuwalipa wafayakazi wake wa nyumbani

  6: Kila kiongozi atajilipia matibabu

  7: Secta za madini na maliasili zimilikiwe 100% serikali

  8: Nisingekubali kuwa ombaomba (Kukubali mikopo isiyo na tija kwa Taifa) si unajua tu msemom usemao "A man in dept is caught in a net" na "all is not gold that gilters"
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ningevunja muungano wa tanganyika na zanzibar na kwaambia wazanzibari nchi imekua moja inayoitwa tanzania. Na yeyote anayebisha ana kesi ya uhaini.
   
 9. M

  Mchili JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ningebadilisha katiba kuunda mfumo unaotegemea taasisi kufanya kazi kisheria bila kufuata utashi wa mtu.
  - Madaraka ya raisi yapunguzwe
  - Madaraka ya mawaziri yapunguzwe
  - Uteuzi wa viongozi wa taasisi kama mkuu wa majeshi, polisi, TRA, TAKUKURU, Majaji na CEOs wa mashirika ya umma, uhakikiwe na kamati za bunge kuhakikisha wanapatikana watu wenye uwezo.
  - Uteuzi wa mawaziri upitishwe na bunge na wafanyiwe usaili ili 'vihio' na wasiokuwa waadilifu wakataliwe kuwa mawaziri
   
 10. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Mzee umeleta maada ambayo ni nzito maana mtu anaweza kukusoa wakati ajapewa nafasi ya kuonyesha njia mbadala.
  mimi ningekuwa rais ningeanzia mbali kidogo kwanza ni kubadili mifumo waliyotuachia wakoloni na kuunda ambayo itakuwa inaendana na nchi yetu. lakini kwa ujumla ningefanya yafuatayo
  1.kilimo
  kwa kuzingatia kuwa kilimo kinachukua asilmia 80 ya watanzania, basi kuinua kilimo ni kuikomboa tanzania.(hii ni kauli mbiu ambayo ni mbadala wa kilimo kwanza).kilimo ningeanza kuondoa kilimo cha kutegemea mvua,badala yake ni kuanzisha umwagiliaji, ningepandisha bei ya mazao yatokanayo na kilimo. ninge ondoa dhana ya kuonekana umefanya kazi ni mpaka utokwe na jasho. kwa kuleta na kutumia zana za kilimo zinazoendana na science na technology. kilimo kingekuwa ni ajira rasmi badala ya sasa ambapo ukimuuliza mkulima wewe ni mfanyakazi atakuambia hana kazi bali ni mkulima, ningewapatia identity card ili wajulikane na wakopesheke na mabenki,ikiwezekana kuyalazimisha mabenki yote yawe na utaratibu maalumu wa kuwakopesha wakulima. hapa ningepunguza ukosefu wa ajira kwa asilimia 80 ya watanzania. suala la njaa ingekuwa historia.ningeongeza mapato ya nchi kwa kuuza mazao ya chakula hususani kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na njaa.
  2. Elimu
  kwanza ningefanya somo la kilimo kuwa ndio somo la lazima, elimu ya kidato cha nne ni lazima, wala sio suala la option. ningebadili mitaala ya elimu ili iweze kumuwezesha mtu kujiajili hasa kwenye kilimo. ningerudisha elimu ya veta kwa wote wasioweza kuendelea na elimu ya juu. yaani ujiajili kwenye kilimo umeshindwa nenda veta. ningesomesha waalimu kwa kuangalia wito. ningeboresha maisha ya walimu kwa kiwango cha juu. hapa ningeweka posho ya kila aina hata kama mshahara usingepanda. semina ni muhimu kwa walimu waendane na mabadiliko ya kisayansi. ningefuta vyuo vyote vya kufundisha watu compyuta badala yake somo la kumpyuta lingefundishwa toka chekechea. vyuo vikuu ningesomesha watu kwa kuwalipia asilimia mia moja kufuatana na mahitaji ya nchi na si vinginevyo. Nisingeshomesha watu eti kwa sababu ya soko. Hapana.
  3. viwanda na biashara
  Hapa ningekuwa makini sana. Hasa kwa kuthibiti kwanza ubora wa bidhaa katika soko ili kuakikisha kunakuwa na fair competition. Ningewawezesha watanzania hata kwa mitaji ili waweze kuwekeza katika secta hii. Lakini ni lazima watumie malighafi kutoka ndani ya nchi. Ningeweka ushuru mkubwa kwa bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo hata nchini zinapatikana (hapa hapana mjadala).lakini pia ningeanzisha viwanda vinavyoweza kuendeshwa na serikali ili kuweka bei elekezo kwa mfano, yaani serikali ingekuwa na bei yake ya kuuzia hii ingesaidia kupunguza mfumuko wa bei wa kiolela. Pia ningerudisha viwanda vya pembejeo kama ZZK kwa kutumia watalamu kutoka VETA.
  4. huduma za jamii.
  Kwa kujumuisha nisingeweza kuachia secta nyeti kama maji, elimu na afya. Mtu aendeshe anavyotaka. Maji yangekuwa bado mikononi mwa serikali na si wawekezaji hapa serikali ingehakikisha ubora wa maji kwa wananchi wake. Ni si kama sasa suala la maji ambalo ni hitaji muhimu linaendeshwa kibiashara. Elimu limekwisha eleza hapo juu. Afya ningeaza kwa kusomesha watanzania kwa kuwalipia asilimia mia na kuwalipa vizuri ili watumikie taifa kwa uzalendo. Ningeondoa makanjanjawote kwenye afya. Hata hawa wataalamu wa mitishamba ningewaunga mkono lakini lazima tuzibiti ubora wa dawa zao. Na wale wapiga ramli hawana nafasi katika uongozi wangu.
  5. Madini
  Hapa ningeanza kwa kufukuza wawekezaji wote katika secta hii, tuanze mikataba upya na sio kuriview. Kwa secta hii kama noma na iwe noma. Ningetumia madini kama tanzanite kuendesha nchi zote zinazohitaji madini yaha. Ningepunguza uzalishaji kwa makusudi ili bei ipande hawataki wakatafute kwingine ukweli ni kwamba yapo Tanzania tu. Ningesomesha wataalamu wa mikataba ndani na nje na kuhusisha wataalamu wa madini katika kusaini mikataba. Na si kusainiwa na wanasiasa. Wawekezaji wote ambao wanajifanya jeuri ningewaita wakoloni.watoke. madini yetu hata kama kunaushindani siwezi kushindana kwa kuuza cheap. Bora niyaache kwa kizazi kijacho kama mwalimu alivyofanya.
  6. uwajibikaji
  Hapa nitatenganisha kabisa mihimili mikuu ya yaani bunge, mahakama na serikali. Na kila moja iwe na bajeti yake na kuandaa mfumo ambao serikali sio iombwe fedha bali itoe fedha kulingana na mahitaji ya mihimili mingine. Pia kutenganisha serikali na chama. Mtu anaweza kuongoza jamii hata asipokuwa mwanachama. Hivyo hatuitaji kunyanganyana kadi. Na kiongozi yoyote atakaye guswa na kasfa lazima awajibike kwa maslai ya umma.

  7. miundombinu, utalii jeshi na polisi.usimamizi wa fedha,muungano na vyanzo vya mapato. vitajadiliwa soon.
   
 11. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mkuu Magezi,
  Nimeipenda sana hiyo.
   
 12. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Ningefutilia mbali wazo la EA federation kwa maana ya kuwa na free movement of labour. Mpaka pale nchi itakapokuwa imewekeza vya kutosha ktk elimu na vijana wetu wawe na ushindani mzuri.
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kula five hapa! but mkuu Elimu ni crucial sana kwa maendeleo ya kweli TZ.....hungekuwa na mpango na hili?

  Sielewi kwanini hawa walioko madarakani hawalioni hili.......boresha maslahi ya wafanyakazi then futa allowances zote sisizokuwa na tija kwa taifa!
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tena kazi kubwa ilishafanywa na kamati ambayo kikwete mwenyewe aliiunda mwanzoni mwa utawala wake. katika ile ripoti yake (ambayo haijawekwa hadharani) tume hiyo ilionyesha ratiba ya jinsi ambavyo serikali inaweza kuongeza vipato vya watumishi na jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya nyongeza hiyo. zaidi ya miaka mitatu sasa hakuna kilichotekelezwa cha maana
   
 15. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sielewi kwanini hawa walioko madarakani hawalioni hili.......boresha maslahi ya wafanyakazi then futa allowances zote sisizokuwa na tija kwa taifa![/QUOTE]

  Yaani Allowance za hawa jamaa ukiziunganisha ni more than mishahara ya wale walioko ktk private sector. Wengine hawachukui hata mshahara wa mwezi kwa jinsi allowance zilivyokubwa. Ni heri zifutwe waongezewe mishahara tu ieleweke moja!
   
 16. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu MN,

  Tatizo sisi kila mahali tunatanguliza siasa hata kwenye masuala yanayohitaji utaalam! Hiyo tume iliundwa kisiasa zaidi na utekelezaji wa mapendekezo pia umefuata mkondo huo huo wa kisiasa..........!tutafika lini hapo?
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ningepata nafasi ya kuwa Raisi kwa kweli ningefanya haya yafuatayo.

  1. Ili kuboresha mfumo wa elimu nchini na kuweka mazingira mazuri na usawa kwa wananchi ningepiga marufuku shule zote za zinazoitwa english medium badala yake shule zote za serikali kuanzia primary hadi high school ningeziboresha kwa kupatia vifaa vyote muhimu km vile vitabu, walimu wenye sifa, madawati, maabara na kima cha chini cha mshahara kingekuwa Sh.700,000. Kila mtoto angesoma kwenye shule hizi. Pia tuition ingekuwa marufuku atakayekamtwa jela miezi 12 na viboko 6.

  2. Kila mkoa ningeweka hospitali ya rufaa yenye madaktari bingwa nao watalipwa mishahara kima cha chini kuanzia Sh. 1,200,000. Kuzipatia vifaa vyote vya matibabu na dawa. Nina imani hata hospitali binafsi zingekufa zenyewe na kila mtu angetibiwa huko.

  3. Kampuni zote za uchimbaji madini ningefukuza badala yake ningeunda shirika la umma kufanya ya kutafiti madini na kuchimba sana sana ningeweka consultants kwenye madini watakaofanya kazi na wazawa katika utafiti na uchimbaji.

  4. Kila wizara itaruhusiwa kuwa na magari yasiyozidi 2,500cc that means ningefanya arrangement na manufacture especially wa Landrover kupata hayo magari.

  5. Ningeazisha kampuni za usafirishaji za umma kama ilivyokuwa Kamata hasa hapa mjini ambapo wanafunzi wangepanda bure na watu wazima walipe nauli.

  6. Ningefukuza kazi board yote ya Tanesco na Management yake na kisha kuweka nyingine yenye ufanisi.

  7. Ningelishawishi bunge kupitisha sheria kila kiongozi au mwananchi yeyote atakayethibitika kutoa au kupokea rushwa achapwe risasi pale uwanja wa uhuru na wananchi waruhusiwe kushuhudia.

  8. Kungekuwa na sheria kuwa board of directors za mashirika na management zake zitakazosababishia hasara makampuni au mashirika wanakwenda jela miaka 5 wakitoka wanalipa hasara iliyotokea.....

  Ngoja nipumzike kwanza!!!!
   
 18. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Mhh wewe iko hasira sana na nchi hii eenhe.
  Ngoja tuchambue hoja zako.

  Nilipo bold naungana nawe kabisa. Ila utakapo piga marufuku shule za english medium jee hizi zitakazo boreshwa zingetumia medium gani.

  By the way kuna English medium, je how about English Large and Engils Small?


  Very good idea. Ingepunguza gharama sana.

  Hapa usimamizi (management) natumaini utaiweka very serious.

  Hapa ndo mkuu Dunia itakuangazia na utaitwa majina yote. Ila kama bunge litakuwa convinced na ikawekwa kwenye sheria na kukawa na seriousness on following up corruption issues then itakuwa ni Discpline moja nzuri sana. I think China wana kitu kama hii.

  Maana umetema cheche na hasira sana.
   
  Last edited: Sep 17, 2009
 19. I

  Inviolata Member

  #19
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mengi naona yameishatajwa ila naongeza yafuatayo katika yale yaliyoishatajwa

  1. Kama Kagame mawaziri wote, makatibu, wakurugenzi, ni marufuku kutembelea magari ya kifahari watumie Escudo suzuki. Ma-VX na GX yauzwe na fedha zake zikanunue Zana za Kisasa cha Kilimo cha umwagiliaji.

  2. Kama China, mafisadi wote adhabu yao iwe ni kifo na kutaifisha mali zao zote.

  3. Kuongeza kiwango cha kodi wanayolipa wawekezaji upande wa Madini, anayetaka alipe asiyetaka aondoke.
   
 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama Bingu Mutharika wa Malawi na wawekezaji ''wanyonyaji'' wa wakulima.....follow government policies hutaki ondoka! Good!
   
Loading...