Ungependa Zuhura Yunus atoke na mkeka kipindi cha Pasaka au baada Eid?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Tukubali kwamba Rais amekwazika sana na ripoti ya CAG. Nilipomsikiliza akitamka neno stupid nilimkumbuka Rais wa sasa wa Zambia Hichilema alipowaambia Wazambia kwamba, siku anaingia ofisini alikuta majalada yanayomtaka aidhinishe fedha za magari na samani nyingine za ofisi kwa kigezo kwamba magari na samani zilizotumiwa na mtangulizi wake haziwezi kutumika na utawala wake.

Hoja hii aliikataa na ikawapa picha wasaidizi wake kuelewa yeye ni mtu wa aina gani.

Mhe. Rais naamini anatafakari kuona wale aliowateua wakaamua kutingisha kiberiti, anawaondoa ofisini ili TAKUKURU na taasisi nyingine ziweze kuanza uchunguzi.

Ni vigumu kumchunguza mteule wa Rais akiwa bado yupo ofisin, naamini sasa vyombo vya uchunguzi vinasubiria awafungulie baraba lakini je, amfungulie baraba pasaka hii au baada ya Eid?

Asipomfungulia baraba mapema upo uwezekano mabaraba wakadestroy ushahidi na akiwafungulia mapema anaweza kuwakwaza baadhi walio kwenye mfungo.

Zuhura Yunus tunasubiri kalamu yako imwake wino kuelekea kunako umma wa Watanzania kuwaambia hasira za mama zimeisha? Sitegemei ziishe kimya kimya au ziishe baada ya azimio la Bunge, maana akisubiri kelele za wabunge italeta tafsiri kwamba serikali inasubiri kufundishwa na Bunge.

Pasaka njem, funga njema kuelekea Eid.
 
Tukubali Kwamba mama amekwazika Sana na ripoti ya CAG. Nilipomsikiliza akitamka neno stupid nilimkumbuka Rais WA sasa WA Zambia Hichilema alipowaambia Wazambia kwamba, SIKU ANAINGIA OFISINI ALIKUTA MAJALADA YANAYOMTAKA AIDHINISHE FEDHA ZA MAGARI NA SAMANI NYINGINE ZA OFISI KWA KIGEZO KWAMBA MAGARI NA SAMANI ZILIZOTUMIWA NA MTANGULIZI WAKE HAZIWEZI KUTUMIKA NA UTAWALA WAKE. Hoja hii aliikataa na ikawapa picha wasaidizi wake kuelewa yeye NI MTU WA Aina gani.

Mhe. Rais naamini anatafakari kuona wale aliowateua wakaamua kutingisha kiberiti anawaondoa ofisini ili TAKUKURU na taasisi nyingine ziweze kuanza uchunguzi. NI vigumu kumchunguza mteule wa Rais akiwa bado yupo ofisini; naamini sasa vyombo vya uchunguzi vinasubiria awafungulie baraba; lakini je amfungulie baraba pasaka hii au baada ya Eid?

Asipomfungulia baraba mapema upo uwezekano mabaraba wakadestroy ushahidi na akiwafungulia mapema anaweza kuwakwaza baadhi walio kwenye mfungo...........Zuhura Yunus tunasubiri kalamu yako imwake wino kuelekea kunako umma WA Watanzania kuwaambia hasira za mama zimeisha? Sitegemei ziishe kimya kimya au ziishe baada ya azimio la Bunge maana akisubiri kelele za wabunge italeta tafsiri kwamba serikali inasubiri kufundishwa na Bunge. Pasaka njema; funga njema kuelekea Eidtokr
Atoe mkeka usiku wa mkesha wa Pasaka,ili wa kusherehekea pasaka asherehekee vyema na wa sonona asonone vyema,ili hata awezeliwazwa na shamrashamra za pasaka🤸🤸
 
Tukubali Kwamba mama amekwazika Sana na ripoti ya CAG. Nilipomsikiliza akitamka neno stupid nilimkumbuka Rais WA sasa WA Zambia Hichilema alipowaambia Wazambia kwamba, SIKU ANAINGIA OFISINI ALIKUTA MAJALADA YANAYOMTAKA AIDHINISHE FEDHA ZA MAGARI NA SAMANI NYINGINE ZA OFISI KWA KIGEZO KWAMBA MAGARI NA SAMANI ZILIZOTUMIWA NA MTANGULIZI WAKE HAZIWEZI KUTUMIKA NA UTAWALA WAKE. Hoja hii aliikataa na ikawapa picha wasaidizi wake kuelewa yeye NI MTU WA Aina gani.

Mhe. Rais naamini anatafakari kuona wale aliowateua wakaamua kutingisha kiberiti anawaondoa ofisini ili TAKUKURU na taasisi nyingine ziweze kuanza uchunguzi. NI vigumu kumchunguza mteule wa Rais akiwa bado yupo ofisini; naamini sasa vyombo vya uchunguzi vinasubiria awafungulie baraba; lakini je amfungulie baraba pasaka hii au baada ya Eid?

Asipomfungulia baraba mapema upo uwezekano mabaraba wakadestroy ushahidi na akiwafungulia mapema anaweza kuwakwaza baadhi walio kwenye mfungo...........Zuhura Yunus tunasubiri kalamu yako imwake wino kuelekea kunako umma WA Watanzania kuwaambia hasira za mama zimeisha? Sitegemei ziishe kimya kimya au ziishe baada ya azimio la Bunge maana akisubiri kelele za wabunge italeta tafsiri kwamba serikali inasubiri kufundishwa na Bunge. Pasaka njema; funga njema kuelekea Eid
Mkeka wa nini, wakati watu walitekeleza kwa vitendo alichoagiza Hangaya: watu wale kwa urefu wa kamba zao?
 
Ingawa nimesoma headline tu lakini naona ni kama muendelezo ule ule wa kumtetea Raisi na kujaribu kumtenga na failure yake mwenyewe.

Kuwaondoa au kuwaamisha hakuna tija kwa Taifa, mtu amekwapua bilioni 88, zaidi ya bilioni 120, hasara ya bilioni 204, magari ya bilioni 35.29, bilioni 21.5 haijulikani aliyekopa n.k

Unadhani ukimtoa mtu aliyepata huo mgao, ana hasara gani?

Yaani kama gharama ya kupoteza ajira kwasababu ya ukwapuaji ni kuwa bilionea, unadhani kuna ambaye atasikitika au kuumia? Napiga bilioni 10, naambiwa, haya huo ndo mgao wako, tembea tusikuone; kesho na mwingine naye atataka kufukuzwa hivyo hivyo.

Nani atafanya kazi serikalini miaka 36 apate hata bilioni 1 jumla ya mishahara yake yote? Sasa apate hiyo 10m akiwa na umri wa 37yrs tu, akisukumwa na matamanio ya pisi kali na matanuzi ya Dubai ataacha hiyo fursa?

Wakikwapua, HAKIKISHA WANAZITOLEA KWENYE MATUNDU YOTE YA MIILI YAO kisha waache.
 
Lini mtafunguka akili na kujua hilo nalo lilishapita?ya kale yameisha baada ya paska na Eid tunaanza upya,tushalitazama na tmewasamehe,kazi iendelee na iishe🙏🤣
 
Tunataka pesa ya umma irudi kwanza,

Warudishe pesa ndo wapishe.
 
Tumerudi enzi ya JK. Kila mtu apige awezavyo.
Ndugu, kwani kuna awamu ambayo CAG hajawahi kuibua madudu? Hebu download na ujisomee report ya mwaka 2018/2019 aliyosomewa Mzee!
Screenshot_20230408-135051.jpg
Screenshot_20230408-135147.jpg
 
Ingawa nimesoma headline tu lakini naona ni kama muendelezo ule ule wa kumtetea Raisi na kujaribu kumtenga na failure yake mwenyewe.

Kuwaondoa au kuwaamisha hakuna tija kwa Taifa, mtu amekwapua bilioni 88, zaidi ya bilioni 120, hasara ya bilioni 204, magari ya bilioni 35.29, bilioni 21.5 haijulikani aliyekopa n.k

Unadhani ukimtoa mtu aliyepata huo mgao, ana hasara gani?

Yaani kama gharama ya kupoteza ajira kwasababu ya ukwapuaji ni kuwa bilionea, unadhani kuna ambaye atasikitika au kuumia? Napiga bilioni 10, naambiwa, haya huo ndo mgao wako, tembea tusikuone; kesho na mwingine naye atataka kufukuzwa hivyo hivyo.

Nani atafanya kazi serikalini miaka 36 apate hata bilioni 1 jumla ya mishahara yake yote? Sasa apate hiyo 10m akiwa na umri wa 37yrs tu, akisukumwa na matamanio ya pisi kali na matanuzi ya Dubai ataacha hiyo fursa?

Wakikwapua, HAKIKISHA WANAZITOLEA KWENYE MATUNDU YOTE YA MIILI YAO kisha waache.
Yaan kuna mtu anaiba mpaka boss wake aliye mteua anaona aibu ya kumfukuza😂😂😂
 
Zuhura Yunus tunasubiri kalamu yako imwake wino kuelekea kunako umma wa Watanzania kuwaambia hasira za mama zimeisha? Sitegemei ziishe kimya kimya au ziishe baada ya azimio la Bunge, maana akisubiri kelele za wabunge italeta tafsiri kwamba serikali inasubiri kufundishwa na Bunge.

Pasaka njem, funga njema kuelekea Eid.
Kwa mujibu wa ratiba za Bunge, ripoti ya CAG huwa ni last item baada ya bajeti zote, na baada ya kujadili ripoti ya CAG ndipo bunge linatoa Azimio la Bunge kuhusu ripoti ya CAG na kuipeleka serikali kwa utekelezaji.
Unless Spika Dr. Tulia, kufuatia public interest na lots and lots of misconceptions, aamue Bunge liijadili mapema.
P
 
HUU MJADALA WA SASA NI CHA MTOTO,ILA NINA HAKIKA KINACHOOFUATA WAKATI WOWOTE BILA KUJALI BUNGE,PASAKA WALA MFUNGO WA RAMADHANI "WAHAFIDHINA NA WAKAANGA MBUYU WATABAKI MIDOMO WAZI".
 
Kwa mujibu wa ratiba za Bunge, ripoti ya CAG huwa ni last item baada ya bajeti zote, na baada ya kujadili ripoti ya CAG ndipo bunge linatoa Azimio la Bunge kuhusu ripoti ya CAG na kuipeleka serikali kwa utekelezaji.
Unless Spika Dr. Tulia, kufuatia public interest na lots and lots of misconceptions, aamue Bunge liijadili mapema.
P
Naomba utusaidie akina sisi. Ndiyo kusema mikono ya rais inafungwa kabisa kikatiba kiasi kwamba hawezi kumfuta kazi mtu yeyote aliyetajwa na ripoti ya CAG mpk mjadala uishe bungeni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom