Ungekuwa wewe ungemshaurije huyu jamaa?

mnyakyusa

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
248
39
Wana JF; kuna jamaa yangu mmoja aliamua kumtoa out rafiki yake wa muda mrefu kwenda kupata moja moto moja baridi baada ya rafiki yakwe kumweleza kuwa amefulia!!

Walipofika baa walianza kugida bia kama kawaida ilipofika bia tatu tatu kila mtu; yule aliyetolewa out akaanza kwa kumshukuru sana rafiki yake kwa kumtoa ile out maana alikua anajiona mpweke mno......

Baada ya muda kidogo bia ikiwa nusu chupa mtolewa out akaanza kumwambia rafiki yake kwamba kwa kweli tumejaaliwa wake tumeoa wake zetu ni wazuri sana jamaa akamjibu kwa upole na tabasamu kuwa ni kweli na ni jambo la kumshukuru mungu kwa kuwapatia wake wazuri na walio wema.

Ikaagizwa raundi ya nne kisha ya tano....mtolewa out akarudia yale maneno ya awali kumwambia rafiki yake... naye akamjibu ni kweli tumuombe tu mungu wazidi kuwa wake wema kwetu.. kisha mtolewa out akaweka msisitizo kuwa mke wa rafiki yake ni mzuri sana ameumbika vizuri, amejaaliwa wowowoo la kutisha sasa kasema ni lazima ambandue tuu... jamaa aliinuka akaenda mita kama tano akasimama akamtazama yule rafiki yako huku akisema jamani siamini ninayoyasikia kwa huyu best yangu au naota.???.......huku ameduwaa haamini kabisaa......huku mtolewa out akisistiza lazima ambandue mkewe mshikaji......

Wana JF hivi mngemshaurije huyu jamaa ???!!!!
 
hizo si pombe zinaongea tu! asuburi huyo rafki yake kesho akiwa mzima bila pombe kichwani amweleze hakufurahiwa na aliyokua anaongea jana then nafkr kwa majibu atakayo pewa anaweza pata picha kama jamaa yake huyo alijua alichokua anasema
 
Angemwongezea bia mbili zaidi halafu angemuuliza,ni mbinu gani utatumia kumpata?
baada ya hapo,no more beer,aahirishe kikao hadi kesho. kesho yake aagize soda nakuanza kumuuliza yale ya jana.
 
Mmmh lakini hiyo ni taswira ya kilichojificha nyuma ya sura ya mtolewa out! Kimsingi ni kitu anachokipigia mahesabu! Pombe zikiisha amweke chini na amweleze wazi! Du! Mie lazima nimnase na kibao cha kumtoa ulevi!
 
Angemwongezea bia mbili zaidi halafu angemuuliza,ni mbinu gani utatumia kumpata?
baada ya hapo,no more beer,aahirishe kikao hadi kesho. kesho yake aagize soda nakuanza kumuuliza yale ya jana.

Si ajabu kama angemwongeza bia zingine mbili jamaa angesema tayari alishambandua mke wa mshkaji! Inaelekea jamaa akilewa huwa ana ''fantasy'' na mke wa rafiki yake!
 
Inaonekana huyo mtolewa out kashammega mke wa jamaa.
Cha msingi Jamaa awe mpole tu, amlie taiming na yeye amlipizie kwa mkewe huyo mtolewa out.
Haipunguzi machungu lakini inarudisha hadhi ya kiume.
 
ngumi moja nzito ya chembe itamtoa pombe zote na kumkumbusha kwamba anaongea ujinga,i cnt tolerate this nonsense hata kama ni rafiki yangu,kesho yake akinilalamikia hata mimi ntamwambia nililewa bana.
 
Inaonekana huyo mtolewa out kashammega mke wa jamaa.
Cha msingi Jamaa awe mpole tu, amlie taiming na yeye amlipizie kwa mkewe huyo mtolewa out.
Haipunguzi machungu lakini inarudisha hadhi ya kiume.

Male ego; wewe kuiba ili ulipe kisasi ni uhayawani usio kipimo; do you have to stoop to that level? Je hiyo itamzuia mkewe kuto-do kama ndio tabia yake?
 
Jamaa angeongeza bia mbili zaidi, mambo ingekua mbaya sana... maana jamaa angeropoka jinsi alivyommega wiki iliyopita !!! Khaaaa.... wacha wewe !!!
 
...Huyo mtolewa out kifupi ni kuwa lazima aidha atakuwa alishamega mke wa jamaa au ana hayo mahesabu tangu siku nyingi..Kwa kweli ningekuwa mimi ningeachana nae tu maana ni wazi ina dhamira mbaya!
 
Wana JF; kuna jamaa yangu mmoja aliamua kumtoa out rafiki yake wa muda mrefu kwenda kupata moja moto moja baridi baada ya rafiki yakwe kumweleza kuwa amefulia!!

Walipofika baa walianza kugida bia kama kawaida ilipofika bia tatu tatu kila mtu; yule aliyetolewa out akaanza kwa kumshukuru sana rafiki yake kwa kumtoa ile out maana alikua anajiona mpweke mno......

Baada ya muda kidogo bia ikiwa nusu chupa mtolewa out akaanza kumwambia rafiki yake kwamba kwa kweli tumejaaliwa wake tumeoa wake zetu ni wazuri sana jamaa akamjibu kwa upole na tabasamu kuwa ni kweli na ni jambo la kumshukuru mungu kwa kuwapatia wake wazuri na walio wema.

Ikaagizwa raundi ya nne kisha ya tano....mtolewa out akarudia yale maneno ya awali kumwambia rafiki yake... naye akamjibu ni kweli tumuombe tu mungu wazidi kuwa wake wema kwetu.. kisha mtolewa out akaweka msisitizo kuwa mke wa rafiki yake ni mzuri sana ameumbika vizuri, amejaaliwa wowowoo la kutisha sasa kasema ni lazima ambandue tuu... jamaa aliinuka akaenda mita kama tano akasimama akamtazama yule rafiki yako huku akisema jamani siamini ninayoyasikia kwa huyu best yangu au naota.???.......huku ameduwaa haamini kabisaa......huku mtolewa out akisistiza lazima ambandue mkewe mshikaji......

Wana JF hivi mngemshaurije huyu jamaa ???!!!!
hadithi hii kakufundisha nani?
amekuambia ina maana gani??

makofi tafadhali
 
Usikurupuke kutaka kujua nini kinaendelea kwa haraka hivyo. Angemsapoti kwa aliyosema si ajabu jamaa angezungumza kila kitu. Kama asingesema siku hiyo, angemtoa out siku nyingine na nyingine mpaka angahadithia kila kitu. Halafu shughuli ingehamia kwa wife. Si yule tena....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom