Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Nimeishi naye tangu mwaka 2017 baada ya 2014 kumzalisha mtoto nikaamua nimchukue tujenge familia 2023 tukapata mtoto wa tatu nakuja kugundua mwenzangu anamahusiano nje na mchumba wake wa awali kabla sijamchukua.

Uchunguzi binafsi nikabaini Wana zaidi ya miaka mitatu wapo kwenye mahusiano hayo
Mi nipo wilayani kusaka maokoto wakati yeye yupo mjini tulipojenga.

Baada ya dharau kuzionesha nikamwambia najua chanzo Cha ujinga wake, nikamtajia anayempa jeuri, nikamueleza nayajua mahusiano yake tangu mwaka 2020, najua anapokutana na huyo mtu wake, nikamuonesha ushahid wote.

Aliduwaa akabaki mdomo wazi, akaomba sana msamaha, akadai hatorudia

Nimerudi kazini sijaongea lolote, sijamwambia nimemsamehe, sijampa nafasi ya kujua nini nawaza.

Nimemruhusu aendelee na mtu wake maana hainidhuru mie ila roho inauma.

Mpaka Sasa anadai anaumwa moyo unamkimbia maana hajui nini nitafanya na uamuzi gani nitachukua.

Je, nipo sahihi?

Kama ni wewe ungefanya nini?

Mawazo yako ni muhimu
Kazia hapo hapo wewe kula buyu
 
Ogopa sana mtu mwenye mahusiano na mpenzi wake wa zamani kabla yako! Nasisitiza ogopa sana.

Hutokaa uweze kuwaachanisha, hapo wewe ndio uachane nao.
Kwa hiyo na wewe tukuogope?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom