Ungekuwa wewe ungefanyaje, ungemsaidiaje?

Ungekuwa wewe ungefanyaje, ungemsaidiaje?

U think it is easy to see ur friend cries infant of u, do u know how does that feel??
Sio rahisi kumuona mwanaume akilia au akikwambia mambo yake mazito na anakuwa kama anakata tamaa mtu ambae ana great vision, mpambanaji na anayependa kujitoa kisa tu mwanamke mshenzi
Anyway ahsante kwa ushauri
Ujue kumwita rafiki yako.aje kuona ni.kuweka mazingira ya yeye kuona mambo ya mkewe na jamii ya watu wa karibu yake ukiwa wewe muweze kumnasua kwenye janga. Tatizo halifichwi lina angaliwa ili tujue njia gani upitie kujinasua
 
Habari za ndugu, jamaa na marafiki wa JamiiForums

Katika maisha, tunakutana na watu tofauti ambao hatukuwatarajia na wanakuja kuwa kama ndugu zetu tulioshibana nao tukisaidiana katika changamoto za hapa na pale.

Nina kisa kimoja kilichotokea na kuniacha katika njia panda ya nn kilicho sahihi nifanye.

Iko hivi nina rafiki yangu ambae tumekuwa kama ndugu, kwanza tunafanya kazi sehemu moja, na pia katika investment tumewekeza pamoja na almost kila kitu cha kupiga hatua tunapambania pamoja.

Sasa kuna kipindi alikuwa na ugomvi na mke wake ambao ilifikia kuwepo Vikas vingi na usuluhisho usiofikia Kikomo. Jamaa yeye sio mnywaji ila mkewe ni mnywaji sana na mtu ambae anapenda kutoka kwenda Maclub na kujichanganya na ndio moja ya sababu ya wao kupumzishana ili ajirekebishe tabia.

Sasa weekend moja niko maeneo napata kinywaji, namuona mke wa huyo jamaa yangu nae yuko hapo anajiachia, kwanza kavaa mavazi ambayo yanasikitisha, pili kalewa balaa anashikwa shikwa hovyo na wanaume na yeye kajiachia hovyo.

Kiukweli roho yangu iliumia sana mpaka nikahisi ndio mm kama nafanyiwa, sikuwa na amani tena nikaondoka lakini jambo hili linanikosesha amani kiasi kwamba naona kama namsaliti jamaa yangu nisipomwambia.

Lakini pia sitaki kuwa sehemu ya kuwatenganisha kama wataachana mazima maana najua kwa Aina hii ya mwanamke watoto watapata shida sana 😢 maana mwanamke huyu sio mlezi mzuri kabisa na jamaa yangu ana Wadena sana wanae na hapendi walelewe na mzazi moja.

Je, wewe ungekuwa kwenye nafasi kama yangu ungefanya maamuzi gani?
Wengne wanakua wameshawaka hawana time wa wake zao kuwafatilia kuwa mpole.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom