Ungekuwa wewe ungefanya nini?

thadei kimambo

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
220
126
Vuta picha umelala mida ya alfajiri hivi, usingizi ule wa kukesha jana yake, halafu kuna mtu anakuja kukugongea mlango kwa fujo sana kwenye mida ya saa moja moja hivi.

Ile unaamka kwa hasira kwenda kumfungulia unajikwaa kidole cha mwisho cha mguu katika kona ya kitanda - ile ndiii!, ukaruka kwa maumivu ukapamia ndoo ya maji yakamwagika sakafuni.

Mara unateleza katika yale maji unaangukia meza unaangusha TV, deki na wewe chini mara waya wa umeme unakupiga short mgongoni unafika mlangoni na maumivu ya kidole na uchovu + hasira+hasara na short juu unakutana na jamaa anakwambia nasajili line za simu halafu anakutolea meno kwa tabasamu, eti pozi la biashara.

Sipati picha utamfanyaje?
 
Hahaha! Dah kwa hasira nampamia nayeye asikie maumivu nlopata!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom