Ungekuwa wewe ungefanya nini????

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,698
1,395
Una mpenzi/ rafiki yako wa kike, mnapendana sana
hata hivyo wazazi hawajui lolote.
Wote ni wanafunzi sema ni vyuo tofauti. Wewe
mwanaume unakaa katika geto lako, binti
analindwa sana kwao, mlikuwa mmefanya kila kitu
katika mapenzi isipokuwa ngono. Likizo ya binti
ilivyofika hakutoa taarifa yoyote kwao akafunga
safari kuja kwako, Mlikuwa MMEKUBALIANA. Binti
hakumshirikisharafiki yake hata mmoja juu ya suala
hili kwani hakuwa akiwaamini
Baada ya kufurahia naye kwa siku tatu sasa binti
akafunga safari ndefu kwenda kwao, napo hakutoa
taarifa tena.
Ajali mbaya ya gari ikaua watu kumi na tano huko
njiani binti naye akiwa mmoja wao wa marehemu,
tena akiwa amesagwasagwa vibaya hali
iliyosababisha asijulikane kabisa. Mbaya zaidi
hakuwa na kidhibiti chochote cha kumtambulisha.
Wewe unafahamu basi alilopanda na hakika
unatambua kuwa ni mmoja kati ya waliokufa.
Ni wakati wa kuuonyesha upendo wako kwa
marehemu mpenzi wako.
Je unaifikishiaje taarifa familia yake pasipo kuweka
uongo tafadhali ili mwili wa mpenzi wako
usizikwekama MZOGA???????? Na serikali baada ya
ndugu kukosekana???/
FIKIRIA SANA KABLA YA KUTOA MAONI.
Aliyefikwa na jambo hili alizidiwa na msongo wa
mawazo na kufariki kwa kunywa sumu!!!!!!
UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI????
 
Ni wewe tu wa kufanya huyu dada azikwe na ndugu zake,
Ni vyema kuweka wazi juu ya safari na ajali hiyo kwa ndugu zake na kuelezea jinsi ya kumtambua ili wamzike
 
Ni wewe tu wa kufanya huyu dada azikwe na ndugu zake,
Ni vyema kuweka wazi juu ya safari na ajali hiyo kwa ndugu zake na kuelezea jinsi ya kumtambua ili wamzike

Unadhani hao wenye ndugu yao watakuacha huku eakijua fika wewe ndio chanzo cha kifo cha mpendwa wao??,
 
Nitawaeleza ndugu zake, potetelea mbali liwalo na liwe kua nilimpenda kiukweli.
 
Suala liko wazi lazma niwaambie tu kwani kuna shida gani?
Mambo mengine yatapa yenyewe taarifa wakipata coz kwani mimi ndo nimemuua?
 
Suala liko wazi lazma niwaambie tu kwani kuna shida gani?
Mambo mengine yatapa yenyewe taarifa wakipata coz kwani mimi ndo nimemuua?

Mmmnh kwani asingekuja kwako kuspend angevuta kwa style hiyo kaka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom