Ungekuwa wewe ungefanya nini kwa mwanamke huyu?

Upo sahihi kabisa, kabla ya ndoa ni muhim sana kupima UKIMWI,

Aidha, ni muhimu sana mke anapokuwa mjamzito kwenda nae clinic ili wanandoa husika mume na mke wapimwe afya zao na kupewa ushauri stahiki.

Jamaa alipuuzia kwenda clinic na mkewe Hatimae mke kakutwa na UKIMWI bila yeye mume kujua,

Tujifunze kupitia huyu,

ni kweli mkuu ni fundisho tosha,kwa kweli inauma sana
 
Kama ameamua kumuacha huyo mkewe ni juu yake, maana kamficha jambo zito wala simlaumu. Lakini anapaswa kutoa hela ya matumizi kwa ajili ya mtoto wao. Maana kiumbe cha watu hakina kosa! Ila jamani huyo mama ana roho ngumu! Kabisa akaamua kuwaambukiza watoto wake hivihivi kha!!

kwa kweli anaroho mbaya sana anapoteza sifa ya kuitwa mama kabsaa kwanza sikutegemea kama angekuwa mtu wa namna hii
 
Mmh haya mazito mbona.........ila hapa kuna la kujifunza, jamani kupima muhimu,sikuhizi bado watu wanapima kwa macho na kuchotana akili.
Anyways,huyo baba kama ameamua kumuacha mkewe mi nasupport,maana kama mke amekaa kimya muda wote mume hajui kama mkewe ameathirika, ina maana kama ingetokea jamaa nae angepata mke angepata wa kumtupia lawama labda ye ndo kauleta and all that.
Ila mtoto amtunze tu jamani hana hatia hata kidogo,japo inauma ila hakuna jinsi.
Pole Mjomba.
 
Kuna watu wengine wana matatzo katika seli ndo mana anko haukwaa...mtoto kesha zaliwa na tatzo lishatokea kwo anko hana budi kukubali,wamlee tu mtoto uku wakitafta wengine maana,familia ni baba,mama na watoto..nawasilisha
 
ART bila shaka ulitaka kumaanisha ARV

art_therapy1.jpg

WHO


Standard antiretroviral therapy (ART)
 
Mbona kama mie hainiingii akilini wajamenii,yani mjombako kakaa na mke miaka sita na watoto wawili wakapata then inakuja kugundulika mke ana ngoma lakini kwa maajabu mume hana,na watoto wakaupata mara tuu baada ya kuanza kunyonya,hii story yako mbona ina plot holes nyingi,anormalies kibao.kwanza huyo mume amewezaje kuishi na mwathirika muda wote huo na kuzaa watoto na asipate maambukizi?.pili alipokuwa mjamzito wa mtoto wakwanza hakwenda kliniki,maana sheria lazima upimwe ngoma ww na mwenza wako kabla hajajifungua.inamaana hyo familia ni ya mataahira,maana mtu mwenye akili ya kawaida hawezi kufanya utumbo huo.
 
Jaman wanajamvi hamuoni kabisa hii stori ni ya kutunga na nyie mnamshauri kabisa.yaan kati ya 2010-2016 unaweza kuzaa watoto wawili katika nyakati tafauti na bado usigundue kuwa umeathirika,the. Katika kipindi hichohicho uishi na mume ndani na yeye asipate maambukizi ilhali wewe mwanamke umeathirika kwa muda mrefu.inaingia akilini hii,au ni mimi tu ndo nmedata?
 
Jaman wanajamvi hamuoni kabisa hii stori ni ya kutunga na nyie mnamshauri kabisa.yaan kati ya 2010-2016 unaweza kuzaa watoto wawili katika nyakati tafauti na bado usigundue kuwa umeathirika,the. Katika kipindi hichohicho uishi na mume ndani na yeye asipate maambukizi ilhali wewe mwanamke umeathirika kwa muda mrefu.inaingia akilini hii,au ni mimi tu ndo nmedata?
wewe tu ndo umedata; unahitaji elimu juu ya vvu na ukimwi. Maswali yote uliyouliza jibu lake ni ndiyo, inawezekana.
 
Mbona kama mie hainiingii akilini wajamenii,yani mjombako kakaa na mke miaka sita na watoto wawili wakapata then inakuja kugundulika mke ana ngoma lakini kwa maajabu mume hana,na watoto wakaupata mara tuu baada ya kuanza kunyonya,hii story yako mbona ina plot holes nyingi,anormalies kibao.kwanza huyo mume amewezaje kuishi na mwathirika muda wote huo na kuzaa watoto na asipate maambukizi?.pili alipokuwa mjamzito wa mtoto wakwanza hakwenda kliniki,maana sheria lazima upimwe ngoma ww na mwenza wako kabla hajajifungua.inamaana hyo familia ni ya mataahira,maana mtu mwenye akili ya kawaida hawezi kufanya utumbo huo.

Wanawake tuko more vulnerable kwenye maambukizi kwasabu all the semen enters female vagina.
 
Duuuhh, napenda kumpa pole mjomba na shangazi yako. Kwanza kwa kupoteza mtoto wao Mpendwa, pili kwa ndoa yao kuvunjika. Walikuwa na Malengo makubwa lakini yamegongana mwamba.

Nimekuwa siku zote nalaani "DINI" hasa hizi za kigeni kwa kachangia sisi waafrika kuwa wanafiki kupitiliza. Msingi mkuu wa DINI ya kikristo ni kumpenda "Jilani kama nafsi yako". Linatokea jaribu hutaki kukifanya kile ambacho unafundishwa miaka yote.

"Amri mpya ninawapa, pendaneni".
 
pia wanaume tuwe makini na hizo bikira siku hizi nyingi za kununuliwa kigoma zinauzwa elfu mbili tuu na unatoa damu ni bora umkute tuu hana utakuwa na akili ya kwenda kupima pia huyo dada ni muuaji mbona kule wanakochukulia dawa wanakuwepo wanaume wengi tuu wanaoana lkn sio kuja kutaka kumponza mjomba hiyo dhambi, po;e saana anko usiombe yakukute
 
Yaani hayo yalimkuta kaka mmoja msomali, alioa mke bikira lakini ndani ya miezi sita dada amegundulika na VVU. Yule mwanaume alichanganyikiwa.
 
ABARI ZA MWISHO WA WIKI?. Namshukuru Mungu kwa afya na uzima nilio nao hadi wakati huu, naamini kila mtu anasababu yake ya kumshukuru Mungu.

Naombeni ushauri wenu kuhusu hili ila nami nipate namna ya kumdaidia mjomba wangu.
Mjomba alioa mke miaka 6 iliyo pita na amefanikiwa kupata watoto wawili wa kiume likini mke alikuwa na tabia ya kukataa kuwanyonyesha watoto mjomba hakuelewa ni kwanini na hata mke hakuwa akitoa maelezo ya kueleweka kuhusu hilo. lakini baada ya kusemwa sana alikubali kunyonyesha.
sasa baada ya kipindi fulani watoto wakaanza kuumwa na baada ya kufanyiwa vpimo ikagundulika wana VVU wote wawili pamoja na mama yao. lakini mjomba alipopima hakuwa na maambukizi.
mke anadai kuwa yeye aliathirika mda mrefu kabla ya kukutana na mjomba ilahakutaka kumwambia likini na mjomba nae aliwahi kunieleza kuwa mkewa hakuwa mayala kwa sababu alimkuta bikra
likini kinachomuuzi mjomba ni kwanini alimficha na kwanini hakusema ukweli ili kuokoa watoto.
mjomba ameamua kumsusia watoto akidai kuwa aliamua kuwaua makusudi na kibaya zaidi mke nae ametengwa nyumbani kwao
pia hana kipato chochote cha kumuwezesha kulea watoto na mwezi uliopita mtoto yule wa pili amefiriki.
je nini cha kumshauri mjomba ili kunusulu mtoto aliye baki
natanguliza shukurani zangu kwenu
Mwambie amrudie haraka mkewe na waendelee kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha! Au amesahau kuwa aliapa 'mpaka kifo kitakapo watenganisha?…Hakuapa mpaka uongo utakapowatenganisha! Wanandoa wengi sana kwa bahati mbaya huingia kwenye ndoa kwa kudanganyana sana…na mara nyingi hupita ktk wakati mgumu sana ili kuufichua ukweli… Huyo mjomba wako, mwambie aliye mlinda asipate maambukizi ndie anaemkumbusha amrudie mkewe na Yeye Mungu atawalinda wote!
Wazae wengine na wawakuze wote!
 
Wangepima afya zao kwanza walipokutana. Anyway mjomba anabahati, kama mama atakuwa anatumia ART kunachance asimumbukize mjomba lakini alitakiwa aseme ukweli mwanzoni. Hata ukikutana na mwanaume au mwanamke anatoka mbinguni dunia ya sasa si wa kumwamini.

Afya ni asset kama asset nyingine yeyote unatakiwa kuilinda.
Nimependa sana hayo maneno ya last paragraph.
 
Back
Top Bottom