Ungekuwa wewe ungefanya nini kwa mwanamke huyu?

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,641
11,956
ABARI ZA MWISHO WA WIKI?. Namshukuru Mungu kwa afya na uzima nilio nao hadi wakati huu, naamini kila mtu anasababu yake ya kumshukuru Mungu.

Naombeni ushauri wenu kuhusu hili ila nami nipate namna ya kumdaidia mjomba wangu.
Mjomba alioa mke miaka 6 iliyo pita na amefanikiwa kupata watoto wawili wa kiume likini mke alikuwa na tabia ya kukataa kuwanyonyesha watoto mjomba hakuelewa ni kwanini na hata mke hakuwa akitoa maelezo ya kueleweka kuhusu hilo. lakini baada ya kusemwa sana alikubali kunyonyesha.
sasa baada ya kipindi fulani watoto wakaanza kuumwa na baada ya kufanyiwa vpimo ikagundulika wana VVU wote wawili pamoja na mama yao. lakini mjomba alipopima hakuwa na maambukizi.
mke anadai kuwa yeye aliathirika mda mrefu kabla ya kukutana na mjomba ilahakutaka kumwambia likini na mjomba nae aliwahi kunieleza kuwa mkewa hakuwa mayala kwa sababu alimkuta bikra
likini kinachomuuzi mjomba ni kwanini alimficha na kwanini hakusema ukweli ili kuokoa watoto.
mjomba ameamua kumsusia watoto akidai kuwa aliamua kuwaua makusudi na kibaya zaidi mke nae ametengwa nyumbani kwao
pia hana kipato chochote cha kumuwezesha kulea watoto na mwezi uliopita mtoto yule wa pili amefiriki.
je nini cha kumshauri mjomba ili kunusulu mtoto aliye baki
natanguliza shukurani zangu kwenu
 
Wangepima afya zao kwanza walipokutana. Anyway mjomba anabahati, kama mama atakuwa anatumia ART kunachance asimumbukize mjomba lakini alitakiwa aseme ukweli mwanzoni. Hata ukikutana na mwanaume au mwanamke anatoka mbinguni dunia ya sasa si wa kumwamini.

Afya ni asset kama asset nyingine yeyote unatakiwa kuilinda.
 
Upo sahihi kabisa, kabla ya ndoa ni muhim sana kupima UKIMWI,

Aidha, ni muhimu sana mke anapokuwa mjamzito kwenda nae clinic ili wanandoa husika mume na mke wapimwe afya zao na kupewa ushauri stahiki.

Jamaa alipuuzia kwenda clinic na mkewe Hatimae mke kakutwa na UKIMWI bila yeye mume kujua,

Tujifunze kupitia huyu,
 
Kama ameamua kumuacha huyo mkewe ni juu yake, maana kamficha jambo zito wala simlaumu. Lakini anapaswa kutoa hela ya matumizi kwa ajili ya mtoto wao. Maana kiumbe cha watu hakina kosa! Ila jamani huyo mama ana roho ngumu! Kabisa akaamua kuwaambukiza watoto wake hivihivi kha!!
 
Hakuna kingine ni kusamehe na kusahau...
kuitekeleza familia ni kuamua kushiriki kuua hao watoto ambao hawahusiki na maamuzi ya wazazi
ukweli n kwamba mjomba anamchukia sana huyo mwanamke na hata alipoitwa na wachungaji bado alikataa kabisa kumsamehe
 
Poleni sana. Hapo kuna denial na unyanyapaa kutoka kwa mjomba wako. Hilo sio jambo rahisi na huwezi kulitatua. Wanahitajika wote wahudhurie ushauri nasaha wa jinsi ya kuishi kuishi salama na VVU na pia jinsi ya kuishi salama na mtu mwenye VVU. Unyanyapaa ni hatari sana.
 
Can you blame him for that? Lakini arudishe moyo kwa kiumbe asiye na hatia. Mbelez watoto wanaozaliwa na maambukizi wameanza kuwatibu na kupona.
 
Poleni sana. Hapo kuna denial na unyanyapaa kutoka kwa mjomba wako. Hilo sio jambo rahisi na huwezi kulitatua. Wanahitajika wote wahudhurie ushauri nasaha wa jinsi ya kuishi kuishi salama na VVU na pia jinsi ya kuishi salama na mtu mwenye VVU. Unyanyapaa ni hatari sana.

Amepona kutoka kwenye mdomo wa simba mkuu, hata ndoa ya Roma watamuelewa inataka moyo. Ingekuwa ulaya huyo mwanamke angeweza kufungwa. Ki sheria ukiwa na maambukizi mume wako na mwajiri wako lazima uwaeleze ukweli.
 
Wangepima afya zao kwanza walipokutana. Anyway mjomba anabahati, kama mama atakuwa anatumia ART kunachance asimumbukize mjomba lakini alitakiwa aseme ukweli mwanzoni. Hata ukikutana na mwanaume au mwanamke anatoka mbinguni dunia ya sasa si wa kumwamini.
Afya ni asset kama asset nyingine yeyote unatakiwa kuilinda.
Afya usiifananishe na asset yoyote, health is the number one thing, YES THE No.1
Cheza na mambo yotelkn sio afya, utajua hilo siku afya yako ikizorota kwa sababu yoyote ile.
 
Kama ameamua kumuacha huyo mkewe ni juu yake, maana kamficha jambo zito wala simlaumu. Lakini anapaswa kutoa hela ya matumizi kwa ajili ya mtoto wao. Maana kiumbe cha watu hakina kosa! Ila jamani huyo mama ana roho ngumu! Kabisa akaamua kuwaambukiza watoto wake hivihivi kha!!
Hii ni kutokana na elimu ndogo juu ya ukimwi japo ni rahisi hapa tukatoa kila mtu maoni yake, lkn linapokuwa liko kwako ni swala zito sana kuamua.
 
Wangepima afya zao kwanza walipokutana. Anyway mjomba anabahati, kama mama atakuwa anatumia ART kunachance asimumbukize mjomba lakini alitakiwa aseme ukweli mwanzoni. Hata ukikutana na mwanaume au mwanamke anatoka mbinguni dunia ya sasa si wa kumwamini.

Afya ni asset kama asset nyingine yeyote unatakiwa kuilinda.

Asante nimekuelewa mkuu
 
Upo sahihi kabisa, kabla ya ndoa ni muhim sana kupima UKIMWI,

Aidha, ni muhimu sana mke anapokuwa mjamzito kwenda nae clinic ili wanandoa husika mume na mke wapimwe afya zao na kupewa ushauri stahiki.

Jamaa alipuuzia kwenda clinic na mkewe Hatimae mke kakutwa na UKIMWI bila yeye mume kujua,

Tujifunze kupitia huyu,

ni kweli mkuu ni fundisho tosha,kwa kweli inauma sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom