Unga wa dengu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unga wa dengu

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtoto halali na hela, Aug 12, 2012.

 1. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  Nina tatizo la kuota chunusi usoni, nimeshauriwa na mtu nitumie unga wa dengu. Hii itasaidia kumaliza tatizo?
   
 2. M

  Mbwayuwayu Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukitaka kutoa chunisi usoni naomba unitafute ktk face book kwa jina la imma kullaya ntakupa njia na utafurahi
   
 3. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  sina akaunt huko fb, nieleze 2 hapa.
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Inawezekana maana inakaza ngozi, kama vile ute wa mayai unavyofanya. Jaribu utuhabarishe
   
 5. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Unachanganya unga wa dengu kiasi na kiini cha yai. Paka then kaa nayo hadi uone imekauka. Kujua imekauka utaona imekakamaa usoni na inaweka kama ufa. Sugua kwa mkono kutoa halafu osha kwa maji safi na salama. Hakikisha una kitaulo special kwa ajili ya kujifutia usoni.
   
 6. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  asante kwa ushauri.
   
 7. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  nitawapa feedback.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Sababu za wanawake kuandamwa na chunusi

  TATIZO la chunusi, linawasumbua wengi wanawake sana hadi baadhi yao kufikia hatua ya kukata tamaa kutokana na kukosa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo.

  Je, unaelewa kuwa kwa asilimia 99, chunusi kwa mwanamke husababishwa na yeye mwenyewe?

  Mambo yanayosababisha chunusi kwa mwanamke ni haya yafuatyo:

  Ulaji usio makini: Wakati mwingine ulaji wa vyakula vyenye mafuta humweka mlaji hususani mwenye ngozi ya mafuta kupata chunusi. Si hivyo tu, wakati mwingine kutokula chakula bora kunaweza kukuletea tatizo hilo.

  Matumizi ya nguo chafu: Kulala kwenye foronya chafu zenye vumbi na mafuta pia hukuweka kwenye hatari ya kupata chunusi, ni vyema hili likatambuliwa na kila mwanamke.

  Unashauriwa kuvaa kofia ya kulalia wakati wa kulala ili kuepuka kuchafua foronya zako, na pia kufanya usafi wa mara kwa mara wa foronya na shuka za kulalia.

  Kujishika usoni mara kwa mara: Wanawake wengi wanapenda kujishika usoni mara mwa mara, bila kuwa na hawana uhakika na usafi wa mikono yao. Jambo hili mara kadhaa limekuwa likisababisha, maambukizo ya bakteria katika ngozi wanaoleta maradhi kama vile ya chunusi na mengineyo.

  Kuzembea wakati wa kuosha nywele: Kwa kawaida vipodozi vya nywele huambatana na mafuta wingi. Hivyo mhusika asipokuwa makini wakati wa kuosha, wakati mwingine husababisha mabaki ya mafuta hayo kuingia usoni na hivyo kuiweka ngozi ya uso katika hatari ya kupata chunusi.

  Matumizi yasiyofaa ya vipodozi: Kutumia vipodozi bila kufuata ushauri wa wataalamu, husababisha wahusika kuzalisha chunusi. Kwa mfano mwenye ngozi ya mafuta anapotumia vipodozi vya mafuta husababisha kutokea kwa chunusi.

  Ukosefu wa elimu ya utunzaji wa ngozi: Kila ngozi ya mwanamke inatakiwa kufanyiwa huduma mbalimbali kama vile scrub, kuondoa seli zilizokufa, kuwekewa mvuke na nyingine nyingi. Wakati mwingine ikiwa haya hayakufanyika , huwa ni chanzo cha uzalishaji wa chunusi katika ngozi.

  Kulala na vipodozi: Hili ni tatizo sugu kwa wanawake wengi. Wengi kutokana na hali fulani hushindwa kuondoa vipodozi wakati wa kulala hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata chunusi. Hakikisha unaondoa vipodozi vyote kabla ya kwenda kulala.

  Dawa ya kutibu Vipele (chunusi) Na Ngozi:

  Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu

  inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
   
 9. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  naona umeongelea upande mmoja tu.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kitu kama sikijuwi mimi huwa sipendi kusema kuhusu Unga wa (unga wa dengu) Sijuwi mimi ndio maana nimekupa Dawa ya Vipele na chunusi mkuu unataka niseme maneno ya uongo? Mkuu.@Mtoto halali na hela Au wewe ni mtoto wa Kiume unazo chunusi?
   
 11. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  kijinsia
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  sawa nimekuelewa lakini Wewe ni Mume au mke? Mtoto halali na hela
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  WOTE tunaamini kuwa wanaume hawapendelei masuala ya urembo. Pia watu wengi wanaamini kuwa mambo ya urembo ni kwa ajili ya wanawake tu. Tafiti za hivi karibuni zimeonyesha kuwa wanaume pia wanapenda urembo. Kwa mantiki hiyo, si vibaya ikiwa tutawaletea dondoo muhimu za urembo kwa wanaume.

  • Usafishaji wa uso

  Kuondoa chunusi usoni.Hakikisha uso wako unakuwa safi muda wote. Pia unashauriwa kutumia sabuni zisizo na kemikali kuosha uso wako. Ni vema uoshaji uso ufanyika si chini ya mara mbili kwa siku. Fanya steaming’ uso wako, kwani husaidia kukuondolea tatizo la chunisi usoni.


  Kama utatumia ‘toner’ni vizuri ukatumia zenye ‘alovera’ au vitamini E kwa wingi. Kwa upande wa midomo, unaweza kutumia Vaseline kulainisha ngozi ya midomo yako.

  • Matunzo ya nywele Kwa maisha ya sasa, hata wanaume wamekuwa makini katika kuboresha muonekano wa nywele zao. Tofauti na wanawake, wanaume hawaitaji vipodozi vingi. Pakaa mafuta nywele kila siku.

  Kama utaratibu huu utakupa shida, basi hakikisha unafanyia ‘masaji’ ya mafuta ngozi ya kichwa chako kila mwisho wa wiki. Kisha osha nywele zako kwa shampoo baridi isiyo na kemikali zinazodhuru. Ikiwa unasumbuliwa na tatizo la kukatika kwa nywele, hakikisha unachagua nywele fupi badala ya ndefu. Ikiwa umri unaruhusu si vibaya ukatumia jeli ya nywele.


  • Matunzo ya mwili Wakati mwingine inawezekana ukawa na vinyweleo vingi mwilini. Ili kuonekana mtanashati unashauriwa kupunguza, hasa vinavyokuletea kero au kuharibu muonekano wako.

  Ukiachilia mbali suala la vinyweleo, mapumziko ya mwili ni muhimu sana katika kuboresha muonekano na pia afya ya mwili wako.

  Unashauriwa kufanya ‘masaji’ ya mwili wako mara moja kwa wiki. Hii itasaidia kurahisisha mzunguko wa damu mwilini mwako na hivyo kukufanya ujione mwepesi na usiye na uchovu.


  Boresha muonekano wa kucha zako za mikono na miguu kwa kuzikata mara kwa mara. Pia unashauriwa kufanya mazoezi na kula mlo kamili,hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kujenga mwili wako.


  • Vipodozi Tumia marashi yanayoendana na harufu yako. Usipake marashi kwapani kwani wakati mwingine huunguza na kufanya ngozi ya kwapa kuwa nyeusi. Pendelea kutumia poda kwa vile hupunguza harufu mbaya mwilini. Ikiwa unasumbuliwa na ukavu wa midomo, tumia ‘lip balm’
  Dondoo za urembo kwa wanaume
   
 14. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  kuna aina za cream na ointment zinazodeal na haya matatizo,eg Persol 2.5,persol cream etc,ni tiba njema,personally nilikuwa na tatizo kama hili nilitumia Persol 2.5 nw m doing great kwa moda mfupi,so mtafute mtaalamu wa magonjwa ya ngozi utafanikiwa ol the best,tunasubiria feedback!
   
 15. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  asante Gilo
   
 16. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  ua welcome!
   
 17. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa poa sasa, asanteni kwa ushauri mlionipa ndugu zangu. Nimetumia huu unga na matokeo ni mazuri.
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya kwa kina dada na wanaume manaotaka usharabalo karibu sana
   
 19. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,185
  Likes Received: 2,883
  Trophy Points: 280
  usharabalo!!?
   
Loading...