Japo Huu Uzi ni wasiku nyingi, nitajibu ili kuwasaidia wengine wengi walio na tatizo sawa na ili kwakua limekua common sana!
Ili tatizo ni common sana kwa almost simu zote za huawei!
Long story short,njia pekee simple ya kulisolve ni ku install stock rom simu ianze upya.
Fata Yafuatayo ili kusolve tatizo;
Vitu na Nyezo utazo hitaji kufanya na kuwanazo ili kukamilisha process hii ni;
1./ Toa Data mako muhimu kwenye simu nyenye tatizo, (In this case haina haja Kwakua alishasema ame hard factory reset)
2./ Computer au Simu nyingine kwaajili ya kudownload hiyo stock rom.
3./ MicroSD card (Memori kadi) isiwe < 1GB.
4./ Bundle ya kutosha isiwe < 700MB.
5./ Archiver software kwaajili ya kuextract file utalo download. (lipo kwenye .zip format)
NB:- Huitaji root privileges kufanikisha zoezi hili.
Kwanza download stock rom ya simu husika kutoka kwenye
Offical Huawei Website Mfano in this case, y560-u02 stock rom hili
hapa
Then extract hilo file kwa kutumia any archive software uliyo nayo. Mfano kwa Windows unaweza tumia {
Winrar-32bit /
Winrar-64bit } , Android
B1 Archiver iko fresh zaid ,na kwa Unix & Linux huitaji kuinstall software yoyote, Fungua Terminal kisha cd kwenye folder file lipo then extract kwa unzip command i.e. {
Code:
unzip Huawei_Y5_Firmware_Y560-U02_V100R001C328B105_Ghana.zip
}
Weka ile sd card kwenye computer/simu uiliyo downloadia hilo file, then Ingia kwenye extracted folder then copy folder linaitwa ' dload ' kama lilivyo na lipaste kwenye root folder ya sdcard yako (yani usiliweke ndani ya folder lingine)
Toa sd card then weka kwenye simu yenye tatizo,hakikisha ipo off, na inachaji atleast asilimia 50.
Then bofya Volume Up button + Volume Down button + Power button kwa pamoja, kisha zi release ikisha ingia kwenye recovery mod, then subiri mpka imalize installation, then reboot simu na tatizo litakua solved.