Undani wa John Mnyika na John Heche

Undani wa John Mnyika na John Heche

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
WanaJF,
Mara ya mwisho kuzungumzia undani wa wanasiasa ilikuwa mwezi January mwaka huu kwa kuwazungumzia wanasiasa mashuhuri Tanzania Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Niliahidi nitarudi tena na mada hii hii kuwajadili wanasiasa wengine.Na nitakuwa nikifanya hivyo mara kwa mara nipatapo nafasi bila kubagua wanasiasa kwa itikadi zao.

Leo nitaomba kuwajadili wanasiasa wengine mashuhuri katika anga la Tanzania.Wanasiasa hao ni John Mnyika-Mbunge wa Jimbo la Ubungo na John Heche-Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Nimewachanganya Pamoja kwa sababu wanashabihiana kwa mambo mengi lakini lamsingi likiwa Itikadi yao na misimamo yao kuhusu mambo ya msingi.

Mafanikio Misimamo yao:

-Kwanza wote hawa ni vijana na wamekuwa kama Role model kwa vijana wengi si kwa vijana wa CDM tu bali kwa vijana wa Itikadi zote.
-Ni vijana wenye misimamo isiyoyumba na wanakitetea kwa nguvu kile wanachokiamini bila kuogopa vitisho kutoka kwa yeyote.
-Kutokana na Karama za kiuongozi walizo nazo wamefanikiwa kufika nafasi za juu kabisa za uongozi kwa umri wao.John Mnyika mbali ya kuwa mbunge anayeongoza jimbo kubwa kabisa la Ubungo pia yeye ndiye msemaji mkuu wa chama chake cha CDM.John Heche ni kiongozi wa BAVICHA Taifa na mjumbe wa Kamati kuu ya chama chake CDM,chombo cha ngazi ya juu kabisa ndani ya chama chake.
-Vijana hawa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ndani ya chama chao hasa kuimarisha chama vijijini na kukipigania chama.Mafanikio yoyote ndani ya CDM huwezi kuwakosa hawa vijana.
-Ni vijana ambao hawaamini katika siasa za makundi.Sikuzote wanaamini katika CDM Imara.Huwezi kuwakuta wakishabikia majina ya watu ndani ya chama chao bali wanashabikia sera na Itikadi ya CDM.
-Ni wanyenyekevu,watiifu na wanapenda kukosolewa.
-Vijana hawa wana heshima kubwa kwa viongozi wao ndani ya Chama na huheshimu siku zote busara za wazee.Lau wakikosoa basi hukosoa kwa staha kubwa.

Changamoto zao:

-John Heche na John Mnyika pamoja na sifa zote zilizotajwa juu bado wanachangamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana wengi zaidi hasa wa vijijini na kuwapa somo la Uraia hususan umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura kwani inaonekana vijana wengi ni wafuasi sugu wa CDM lakini hawajiandikishi wala kupiga kura.
-Kutokana na umaarufu wao wamejitokeza vijana wengine wenye chuki na mafanikio yao na kuwaandama kwa matusi na maneno ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii.Hata hivyo bado vijana hawa wameonyesha subira kubwa kwa mashambulizi hayo.Hawajakata tamaa bali wanasonga mbele.

Kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA.

-Kutokana na yote niliyoandika juu viongozi wakuu wa CDM wanapaswa kuwatia moyo vijana hawa ili wasonge mbele zaidi na wasikatishwe tamaa na maadui wa CDM.
-CDM kama chama wanapaswa kuandaa vijana wasomi wanaofuata nyayo za kina Mnyika na Heche.Hata hivyo nafarijika kuona wapo vijana ndani ya CDM wenye uwezo wa kufuata nyayo hizi.Kwa mfano yupo kijana anayeitwa Ben Saanane,kwa wanaofuatilia siasa zake watagundua kwamba ni kijana anayeonyesha uvumilivu wa hali ya juu.Ben Saanane amewahi kupata misukosuko ya kisiasa lakini alisimama imara kutetea anchoamini.Hakuwahi kukashifu viongozi wake wa chama katika uficho au kwa uwazi.Ben anaamini CDM kama taasisi imara na siyo makundi ya watu.Ninaweza kusema Ben Saanane ni matunda ya kazi nzuri za kina Mnyika na wenzake.Hata hivyo chama kiandae vijana wengi zaidi wa kufuata nyayo za kina Mnyika na Heche na siyo Ben Saanane tu...

WanaJF Karibuni kwa mjadala!
 
Mkuu laiti ningejua mwalimu wako aliyekufundisha ningeomba walau anipe Tuition kidogo kuhusu Analysis.Umetisha kwa analyisis yako.

Niongeze jambo moja tu ili nisiharibu uhondo wa mada yako.Kuhusu Ben Saanane nafarijika sana kumuona jinsi alivyo mkomavu.Nimekuwa nikifuatilia Post nyingi za Ben hakika ni mtu mwenye heshima ya hali ya juu kwa viongozi wote wa CDM.Na pia ninapenda sana pale anapotetea CDM kama Taasisi na siyo makundi ya ufuasi.Ninapenda sana viongozi kukosolewa lakini siyo kumkosoa kiongozi wako kwa matusi ya nguoni kama muhuni.Kama Ben ni matunda ya Mnyika na Heche basi nawapa hongera sana na naunga mkono mada hii 100%.
 
Nashukuru sana mkuu Molemo.Nitajitahidi kuja na analysis nyingi zaidi tena kwa vyama vyote bila ubaguzi.Sifa zako pia zimwendee Professor wangu aliyenifundisha.
 
Mkuu hapo kwenye BENARD SAANANE nakuunga mkono kwa asilimia 1000000000%, huyu jamaa ni hatari kwa hoja na mara nyingi huko nyuma nilikuwa bado sijamsoma vizuri, Kwa kweli naamini kwamba mpaka kufika 2015 CHADEMA itakuwa na majembe haswaaaa, pia siku hizi naona kama nyota inazidi kung'ara kama jua....... Lakini bado kuna vijana vichwa maji wanaotaka kumchafua lakin naamin dogo hawatamuweza kuanzia elimu, ujengaji wa hoja.

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA.
 
Mkuu laiti ningejua mwalimu wako aliyekufundisha ningeomba walau anipe Tuition kidogo kuhusu Analysis.Umetisha kwa analyisis yako.

Niongeze jambo moja tu ili nisiharibu uhondo wa mada yako.Kuhusu Ben Saanane nafarijika sana kumuona jinsi alivyo mkomavu.Nimekuwa nikifuatilia Post nyingi za Ben hakika ni mtu mwenye heshima ya hali ya juu kwa viongozi wote wa CDM.Na pia ninapenda sana pale anapotetea CDM kama Taasisi na siyo makundi ya ufuasi.Ninapenda sana viongozi kukosolewa lakini siyo kumkosoa kiongozi wako kwa matusi ya nguoni kama muhuni.Kama Ben ni matunda ya Mnyika na Heche basi nawapa hongera sana na naunga mkono mada hii 100%.

mkuu nakuunga mkono by 1000%,
 
Mkuu ni kweli mpaka kuleta maandishi haya hapa nimefanya utafiti kwa takriban miezi 8.Ben sijawahi kuonana naye zaidi ya kusoma maandishi yake na nimejitahidi kumfuatilia mpaka chuo alichosoma.Huyu kijana ni nyota inayongaa ndani ya chama kwa hoja zake.Viongozi wakuu wa CDM kama wasiporidhika na maneno yangu waanzishe utafiti wao wa siri kuhusu Ben na wataona.Ninaweza hata kuonyesha namna maadui wa CDM walivyomtafuta Ben ili akisaliti chama chake lakini Ben aliwafukuzilia mbali na hawakuamini macho yao.Ben akisoma haya maandishi yangu atashangaa nimejuaje lakini ajue dunia ni kijiji na jambo lolote jema halifichiki.
 
Mkuu laiti ningejua mwalimu wako aliyekufundisha ningeomba walau anipe Tuition kidogo kuhusu Analysis.Umetisha kwa analyisis yako.

Niongeze jambo moja tu ili nisiharibu uhondo wa mada yako.Kuhusu Ben Saanane nafarijika sana kumuona jinsi alivyo mkomavu.Nimekuwa nikifuatilia Post nyingi za Ben hakika ni mtu mwenye heshima ya hali ya juu kwa viongozi wote wa CDM.Na pia ninapenda sana pale anapotetea CDM kama Taasisi na siyo makundi ya ufuasi.Ninapenda sana viongozi kukosolewa lakini siyo kumkosoa kiongozi wako kwa matusi ya nguoni kama muhuni.Kama Ben ni matunda ya Mnyika na Heche basi nawapa hongera sana na naunga mkono mada hii 100%.

nimekuwa nikimsoma ben saanane
huyu jamaa ni hazina na ni mzuri sana kwa kukitetea chama kwa ujumla

kwa sasa ben yupo kwenye uelekeo sahihi sana

MNYIKA NA HECHE kila mama duniani anatamani hawa wangekuwa watoto wake wa kuwazaa

Namtabiria Mnyika kuwa ndiye rais wa kwanza kutokea upinzani kuikalia IKULU
 
Nashukuru mkuu kwa hoja zako.
 
Mkimaliza kujadili hii,mje mtuambie kwanini katika uchaguzi uliopita wa madiwani mmeambulia kata 5 tu!,ingawa mmefanya kampeni kubwa sana kila sehemu husika,kwa kutumia fedha za mzee sabodo.
 
nimekuwa nikimsoma ben saanane
huyu jamaa ni hazina na ni mzuri sana kwa kukitetea chama kwa ujumla

kwa sasa ben yupo kwenye uelekeo sahihi sana

MNYIKA NA HECHE kila mama duniani anatamani hawa wangekuwa watoto wake wa kuwazaa

Namtabiria Mnyika kuwa ndiye rais wa kwanza kutokea upinzani kuikalia IKULU
Kama ni hazina mbona mlimpiga chini bavicha? Halafu vipi mnyika ataikalia ikulu? Weka maneno sawa sawa bana,watu wataelewa vingine
 
Yah Ben Saanane ni Jembe na Hazina ya Chama
 
Heche nae ni kijana kweli maajabu yapo Chadema.Halafu wote hao uliowataja ni wapeleka maji bafuni wa mwenyekiti
 
Hakika nikiwaondoa hawa walotajwa hapo juu, ktk vijana wa Chadema wanaonitia moyo na wanaoandika vitu vya maana hapa JF ni Ben Saanane, huyu ananipa hamu, nguvu na matumaini makubwa juu ya vijana wetu.

Nakushukuru mkuu Mkandara kwa kuunga mkono sehemu ya hoja yangu.
 
Last edited by a moderator:
Hakika nikiwaondoa hawa walotajwa hapo juu, ktk vijana wa Chadema wanaonitia moyo na wanaoandika vitu vya maana hapa JF ni Ben Saanane, huyu ananipa hamu, nguvu na matumaini makubwa juu ya vijana wetu.

Mkuu ahsante kwa kuliona hilo, jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Pia nashangaa baadhi humu wakianza kumponda dogo ila kiukweli huyu kijana anakuja vyema sana.
 
Last edited by a moderator:
kama huo ndo utafiti inabidi vyuo vya utafiti vifungwe. huo ni ushabiki.
 
Hivi inamsaidia nini mtu kila siku kumtaja mwenzake kwa kuzungumzia mambo yake binafsi?
Mambo binafsi ya mtu, mathalani John Mnyika ama Ben Saanane yana athari gani chanya ama hasi kwa ustawi wa Chadema?
Wasiwasi wangu ni kwamba Ben ameonyesha kupiga hatua kubwa sana kisiasa sasa kuna watu wanamuonea wivu na wanadhani njia ya kumkwamisha ni kuanza kuzungumzia mambo yake binafsi.
Mwanzoni kulikuwa na fununu mitaani kwamba vijana wote waliogombea Bavicha na kuenguliwa wameunda alliance ya kuushambulia uongozi wa Bavicha na Chadema kwa ujumla.
Kwakuwa Ben naye alienguliwa akatajwa kuwemo katika huo ushirika haramu. Kadri siku zinavyokwenda ukweli umebainika kwamba Ben hayuko nao bali amefocus kukijenga chama na si kujenga watu binafsi. Naona hii ndiyo inamletea shida kidogo lakini naona ameshaishinda hiyo vita kwani mwenye macho haambiwi tazama.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni hazina mbona mlimpiga chini bavicha? Halafu vipi mnyika ataikalia ikulu? Weka maneno sawa sawa bana,watu wataelewa vingine

hawezi kupambana na combination ya mboni mhita na sadifa wa Uvccm.Kama ni shule hata sadifa ana masters na wakili Anthoni Mavunde mjumbe wa baraza UVCCM anayo
Ana kazi sana kuongoza bavicha mwakani mbele ya hawa wadomi wa Uvccm.Kwa bahati nzuri mamluki wake paul makonda na akina felician tuliwadhibiti uvccm .hataweza dogo huyo
 
Back
Top Bottom