Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Kama wana taka hiki chama kiimarike zaidi wamsamehe Zito ile chama kiondokane na lawama toka kwa wanachama na mashabiki wa upande huo.Yule Zito ana watu wengi sana nyuma yake .
Kumfukuza ni kuleta mgogoro usiokua na maana kwa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi.

Kumrudisha zito itakua ni mbinu nyingine ya kuhuisha chama na kuwaziba mdomo mahasimu wa chama.

Pia uchaguzi wa ndani utakua mgumu kutabirika jambo litakalo vuta hisia ,macho na masikio ya watanzania wengi, na anayeibuka mshindi ni rahisi kukubalika zaidi kwa wananchi.

Kwa sasa uchaguzi ndani ya CCM unakua ndo kama uchaguzi mkuu kutokana na ushindani uliopo kwa wagombea wake.

Acha Urongo wewe!

Uchaguzi ndani ya CCM Mwenyekiti Taifa anashindanishwa na nani?
 
Hata mimi nakipenda sana chama cha chadema Dr na Mbowe wanajitahidi kupiga kazi. Lakini watafakali kwa makini wamrejeshe Zitto kwenye chama na Ikiwezekana wampe uongozi, anaushawishi wasibeze mawazo yetu kwa kuwa hatuna majina makubwa hapa nchini. Tambua kwenye mpira shabika anajua makosa ya mchezaji kuliko mchezaji mwenyewe, wasibeze ushauri huu.

Mkuu NJALI

Chadema inaongozwa kwa Katiba na Taratibu.

Mbowe na Slaa hawana mamlaka ya kumrudisha mvurugaji mmoja anayetaka kuua chama kwa kushirikiana na maadui...

Anayejiona amefanya makosa na kutaka kurudi kundini atubu uovu wake mbele ya wanachama na aombe msamaha.Wanachama ndiyo watakuwa na uamuzi wa mwisho.
 
Last edited by a moderator:
Acha Urongo wewe!

Uchaguzi ndani ya CCM Mwenyekiti Taifa anashindanishwa na nani?

Usilinganishe mfumo wa kidemokrasia uliopo ndani ya CCM na uliopo CDM.
CCM ni chama kikongwe ambacho kilianza kama chama cha kidikteta na ilikua ni lazima kila msomi,mfanyakazi,na mkulima kuwa mwanachama,jambo ambalo CDM haiwezi kujengwa kwa namna hiyo kwa sasa.

Na pia ni utaratibu wa chama kwa mtu anayeshinda nafasi ya urais anakua pia mwenyekiti wa chama.Huu ni utaratibu wa kuendeleza mfumo wa Chama dola.
Hata hovyo huu utaratibu unakinufaisha chama kinachokua madarakani dhidi ya vyama vingine.
Kwa hiyo CCM wenyewe wameweka utaratibu wa kupita vikwazo vikubwa sana ili mtu aupate uenyekiti jambo linalomfanya apite bila kupingwa.Kikwazo cha kwanza ni cha kupita kwenye kinyang'anyiro cha kugombe urais ndani ya chama.Kikwazo cha pili ni kuingia kwenye uchguzi mkuu wa taifa kwa kushindana na vyama vingine.

Kwa hiyo unaposema Mwenyekiti wa CCM hashindanishi na mtu kwenye nafasi hiyo unasahau vikwazo na ushindani alioupitia mpaka kufikia nafasi ya kupata uenyekiti.

Jambo lingine ni kwamba wakati huu wa mfumo wa vyama vingi ambapo bado hatujapata chama cha upinzani cha kitaifa ili kushindana na CCM yenye wanachama wenye imani kubwa na mapenzi kwa chama, ni vyema kuepuka migogoro midogo midogo ambayo ingeweza kuepukwa.
Mimi mpaka leo najiuliza hivi viongozi na wapenzi wa chadema haowaoni kwamba mgogoro wa Zito kama busara ingetumika usingekuwepo.Na kuwa mgogoro huo unarudisha sana nyuma ustawi wa chama.

Ukweli ni kwamba hakuna uadui kati ya Zito na Chadema kwa maana ya wanachma bali ni mtu au watu wasiozidi watatu ambao wanajali maslahi binafsi ya kisiasa na madaraka kwa kutamani nafasi ya jimbo lake na Unaibu katibu mkuu.Hawa hawatamani kuona Zito anarudi kundini bila kuangalia adhari za kumtosa Zito.Hawataki kuona watu maarufu wanajitokeza ndni ya chama.Hawa ndio maadui wa kubwa ndani ya chama na ndio watakao ua chama kama wataachwa kuendeleza majungu ndani ya chama

Tukubali
 
Mkuu,

Kwa sasa Zitto ni historia ndani ya Chadema,amefukuzwa miezi zaidi ya sita iliyopita.Anashikilia ubunge wake tu kwa huruma ya mahakama.

Kumjadili tena Zitto leo ni sawa na kujilisha upepo.Huyo ameshapotea katika ramani ya siasa kwa Tamaa yake!
 
Popote pale ukitamka jina la Mbowe na Dr Slaa ma-CCM yanaugua. Tazama kuna mtu anajiita Dr. Kwa hofu ya kisaikolojia mbele ya msomi halisi wa Dr
 
Kiukweli tu ni kuwa CDM inatetemesha magamba na mawakala wao wa act ile mbaya,kila nia ovu lazima ishindwe na kulegea.Hiki chama hakika kimepewa kibali machoni pa Bwana aliyeumba mbingu na nchi.
 
Hata mimi nakipenda sana chama cha chadema Dr na Mbowe wanajitahidi kupiga kazi. Lakini watafakali kwa makini wamrejeshe Zitto kwenye chama na Ikiwezekana wampe uongozi, anaushawishi wasibeze mawazo yetu kwa kuwa hatuna majina makubwa hapa nchini. Tambua kwenye mpira shabika anajua makosa ya mchezaji kuliko mchezaji mwenyewe, wasibeze ushauri huu.

Mkuu umefunga au?
 
Kiukweli tu ni kuwa CDM inatetemesha magamba na mawakala wao wa act ile mbaya,kila nia ovu lazima ishindwe na kulegea.Hiki chama hakika kimepewa kibali machoni pa Bwana aliyeumba mbingu na nchi.

Mkuu m4cjb

Asante sana.Ni wazi hiki chama kina mkono wa Mungu mwenyewe.Vinginevyo kingekuwa kimeshapotea kwenye ramani ya siasa Tanzania.

Hila za maadui ambao ni wasaliti na wasaka tonge zimeshindwa vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Popote pale ukitamka jina la Mbowe na Dr Slaa ma-CCM yanaugua. Tazama kuna mtu anajiita Dr. Kwa hofu ya kisaikolojia mbele ya msomi halisi wa Dr

Hakika kabisa mkuu Fabys.Na ndiyo maana wanachama kwa umoja wao wanatamani majabali hawa waingoze Chadema hata kwa zaidi ya miaka 20 ijayo!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu m4cjb

Asante sana.Ni wazi hiki chama kina mkono wa Mungu mwenyewe.Vinginevyo kingekuwa kimeshapotea kwenye ramani ya siasa Tanzania.

Hila za maadui ambao ni wasaliti na wasaka tonge zimeshindwa vibaya.

Mungu ni wa wote si wa CHADEMA au MZEE wa Gongo pekee
 
Last edited by a moderator:
ni viongozi makini sana hata ukoo wa panya wanalifahamu hilo wakuu
 
Ombi langu kwa wajumbe wa mkutano mkuu mpeni Freeman Mbowe kura zote za NDIYO.

Hatutawaelewa kabisa endapo kama Freeman Mbowe ushindi wake utakuwa wa chini ya asilimia 100%

Hao wahuni waliotumwa na CCM kugombea naye hata wakipata kura 1 watajitapa.

Msiwape nafasi ya kupumua vibaraka hao.Wapate kura 0 ili iwe salaam tosha kwa mabwana zao.
 
Back
Top Bottom