Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

Undani wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa

USICHOKIJUA KUHUSU FREEMAN MBOWE.
Msimulizi: GWANDUMI MWAKATOBE

NAKUMBUKA ilikuwa Julai, mwaka 2002,
ambapo nilikutana na Freeman Mbowe akiwa
na kiu ya kweli ya kuleta mabadiliko na siasa
mbadala nchini baada ya kushuhudia
kuporomoka vibaya kwa NCCR-Mageuzi na
TLP.
Akiwa kijana pekee alishiriki kikamilifu kuasisi
CHADEMA mwaka 1992 katika jengo
analofanyia biashara zake – Billicanas.
Nilipokutana naye ilikuwa imepita miaka 10
tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa
na alisema amefanya tafakuri ya kina na
kuhuzunishwa namna mwamko wa mageuzi
ulivyopoa.
Alisikitikia jinsi ukandamizaji wa chama kimoja
unavyoshika kasi na kuifanya nchi idumae na
kurudi nyuma, akiamini mfumo wa chama
kimoja unalemaza umma na kukosa watetezi
wa mabadiliko ya kweli.
Akaniambia ni bahati mbaya kwamba hata
viongozi wenye ujasiri wa kukemea na
kuwatoa watu usingizini kama Mwalimu Julius
Nyerere hawapo.
Niliguswa sana na maneno hayo kwa kuwa
ndicho nami nilihofia na kujiuliza endapo
hatapatikana jasiri mwingine kama Mwalimu
Nyerere, nchi yetu itakuwa ikielekea kuzimu.
Niliamini kuwa tegemeo pekee lilikuwa ni
kupata vyama vya siasa mbadala ili viwe
majukwaa ya kuikemea serikali na kuamsha
umma.
Mbowe aliniambia kuwa CHADEMA walitamani
sana umoja imara wa vyama vya upinzani au
kwa usahihi zaidi vyama vya ushindani.
Kudhihirisha hilo chama hicho kilimuunga
mkono mgombea urais Augustine Mrema
mwaka 1995 kupitia NCCR-Mageuzi.
Jambo hilo lilinishangaza sana kwa kuwa
CHADEMA kilikuwa chama cha kwanza nchini
kupata Mbunge Amani Walid Kabourou,
kupitia upinzani katika Jimbo la Kigoma Mjini
mwaka 1994, kabla ya uchaguzi mkuu wa
1995.
Ni CHADEMA waliosifiwa na Mwalimu Nyerere
kuwa wana sera nzuri kuliko vyama vingine.
Lakini pamoja na hayo wakaunga mkono
mgombea wa chama kingine.
Hawakuishia hapo, mwaka 2000 CHADEMA
hawakuweka mgombea wa urais bali
wakamuunga mkono wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba, na baadaye Mchungaji Mtikila wa DP
akaongezeka kuwapa nguvu CUF.
Hata hivyo bado wabunge wengi wa CUF
walitokea Zanzibar (Pemba) ambapo ni wawili
tu walitokea Tanganyika (nasisitiza Tanganyika
kwa kuwa hatujawahi kuwa na nchi inayoitwa
Tanzania Bara!), ambao walikuwa Wilfred
Lwakatare wa Bukoba Mjini na Frank Magoba
wa Kigamboni.
Chama mbadala na chenye nguvu kwa
Tanganyika hakikutokea! Kwa mwenendo huo
ndipo Freeman Mbowe alipoamua kutafakari
na kujiuliza ni jinsi gani CHADEMA wangeinuka
na kuleta mabadiliko ya kweli nchini baada ya
vyama walivyoviunga mkono kukwama.
Mbowe aliamini kuiangusha CCM kunahitaji
upinzani imara na akaniomba tusaidiane
kubuni dira mpya ya mabadiliko nikiwa
nimetambulishwa kwake na Hebron
Mwakagenda aliyeshauriana na Martin
Mung’ong’o.
Awali Martin Mung’ong’o alimjulisha Mbowe
kuwa kuna wanaharakati vijana kutoka
National Youth Forum, ambao wana moto na
mwamko wa mabadiliko ya kweli. Nikiwa
nafanya harakati zangu binafsi niliibuliwa na
Hebron Mwakagenda baada ya kusoma makala
zangu za mageuzi kwenye mitandao.
Mbowe alikubali kutokata tamaa kushirikiana
na vyama vya upinzani lakini tukaamua
kubadili watu wa kushirikiana nao.
Agosti 2002, tulifanya vikao mfululizo ofisini
kwa Mbowe, na hata bungeni, kuwaomba
wabunge wote wa upinzani waingie mitaani,
mijini na vijijini kuhamasisha mabadiliko nchi
nzima.
Tuliandaa mkutano mkubwa Jangwani ambapo
wabunge wengi wa upinzani walihudhuria
kuzindua kampeni za kuzunguka nchi nzima
kuuamsha umma katika kutetea haki,
demokrasia na kulinda rasilimali za taifa.
Hata hivyo, mkakati wa kutumia wabunge wa
vyama vya upinzani haukuendelea sana kwa
madai ulikuwa ni maamuzi ya wabunge na si
wa vyama walivyotoka.
Baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya
upinzani walipinga wakidai hawajabariki na
wengine waliona ni mkakati wa Mbowe kwa
kuwa tulitumia ofisi yake kuratibu kampeni.
Kuna wengine walidiriki kusema vyama vya
siasa vimetekwa na wabunge wake.
Baada ya kuona dhamira ya kuwaunganisha
wapinzani imepata mkingamo mzito, niliketi
na Mbowe kutafakari upya wapi pa kuanzia.
Mbowe aliazimia kuomba baraka kwa viongozi
wake wa juu ili CHADEMA waruhusu watu
wengine, na hususan wanaharakati na asasi za
kijamii kufanya kazi pamoja katika kuleta
ukombozi wa kweli nchini.
Bila kusita Mwenyekiti wa taifa, Bob Makani,
alikubali na kubariki juhudi za Mbowe za
kuungana na Watanzania wengine katika
kubuni na kutunga sera mbadala na kuleta
matumaini mapya.
Tukaanzisha kamati maalumu ambayo tuliiita
Kamati ya Mbowe ya Mabadiliko (Mbowe
Committee for Change), ambayo ilikuwa
inafanyia vikao vyake Billicanas.
Nikiwa na Martin Mung’ong’o, Hebron
Mwakagenda, Israel Ilunde, Wallace Mayunga,
Juma Kilimba na Stanley Ngesa wa kutoka
Kenya tukaanza kwa kila mmoja kutoa ushauri
wake kwa Mbowe namna gani CHADEMA
waongoze harakati mpya za mageuzi nchini.
Yalitolewa mapendekezo mengi mazuri lakini
wengi wakaamua kuendelea na asasi zao za
kiraia. Hakuna hata mmoja aliyetaka kuwa
mwanachama wa CHADEMA isipokuwa Martin
Mung’ong’o ambaye alishakuwa miongoni mwa
viongozi waandamizi wa chama. Tulipokuwa
tumebaki wawili, mimi na Mbowe, bado
hatukukata tamaa.
Nakumbuka Mbowe aliniambia yafuatayo:
“CHADEMA ikiwa taasisi inayolenga
kuukomboa umma wa Watanzania haina budi
kuanza kujikomboa yenyewe na kufanya
mabadiliko ya ndani ya chama kabla ya
kufanya mabadiliko ya nchi.”
“Mwakatobe, CHADEMA tukiwa taasisi ya
umma tunapaswa kwanza tubadilike ndipo
tudai, tupiganie na tupambane kuleta
mabadiliko ya mfumo mkubwa wa utawala wa
nchi.”
Kwa bahati nzuri CHADEMA wakampa baraka
zote za kusimamia mageuzi ya ndani ya
chama. Nikawa Mshauri Elekezi wa Masuala ya
Kisiasa wa Kujitolea huku pia nikiwa msaidizi
wa Mbowe wa miradi ya maendeleo jimboni
kwake Hai kabla ya yeye kupumzika kati ya
2005 – 2010 baada ya kugombea urais 2005.
Ilituchukua muda mrefu kujua tuanzie wapi,
wakati mwingine tulijadiliana kuanzia Dar es
Salaam hadi kwake kijijini, Nshara Machame,
bila kufikia mwafaka na kurudi Dar es Salaam
tukiendelea kutafakari.
Tulikuwa tukihamia Dodoma bungeni
tukiendelea kukuna vichwa tuanze na lipi kati
ya maazimio mengi na njia nyingi za kuyafikia.
Hatimaye tuliafikiana kuainisha maeneo
makuu matatu ya kimkakati na kuyafanyia
marekebisho au kuyaunda upya.
Kuipitia, kuichambua, kuifumua na kuiandika
upya katiba ya chama.
Kutunga sera mbadala na bora za chama na
kwa ajili ya nchi katika sekta kuu 12.
Kubuni Mkakati Kabambe (2003 – 2005) wa
kufufua chama na kueneza sera za chama nchi
nzima.
Tulianza kazi hii kwa kujitolea kwingi kiakili,
kifedha na muda. Nakumbuka tulikuwa
tunakesha kuipitia Katiba ya CHADEMA,
tukaichambua, tukaifumua upungufu wake.
Hatukuacha eneo lolote kwani tulianzia neno
la kwanza, ukurasa wa mbele na kuanza
kuandika upya marekebisho na mapendekezo
tuliyoyaainisha ili kupanua demokrasia ndani
ya chama na maamuzi ya chama
yanayoendana na uadilifu, uaminifu na
uzalendo kwa chama na taifa.
Mbowe alikuwa anawasilisha kila marekebisho
na mapendekezo kwenye vikao vya dharura na
vya kawaida vya chama ili kupata maoni zaidi
na kuridhiwa na viongozi wa chama.
Gharama zote za kufanya marekebisho ya
katiba na kuandika mapendekezo alilipa
mwenyewe isipokuwa mimi tu niliyekuwa
nikijitolea.
Sitasahau siku tulipokuwa tunakesha Protea
Hotels kwa siku kadhaa ambapo ilipofika saa 8
usiku nilikuwa nimechoka sana na kusinzia
ovyo. Niliamua kulala ili nipumzike kidogo,
lakini bila kujitambua kumbe usingizi mzito
ulinipitia hadi saa 1:30 asubuhi.
Nilipoamka nikashangazwa sana kukuta Mbowe
bado yuko mezani anachambua katiba
kipengele kwa kipengele huku akiwa
amezungukwa na makaratasi mengi na vitabu
vingi kila upande. Hakulala!
Ni wanachama wachache sana wa CHADEMA
ambao walitutembelea Protea Hotels
tulipopiga kambi na kutupa pole kwa kazi
nzito, na mmoja wao, mzee Sylverster
Masinde kutoka Ukerewe, alikwenda mbali
zaidi kwa kutusaidia uchambuzi, kutoa maoni
yake na kututia moyo.
Awali nilishashiriki kutunga Katiba ya chama
cha Demokrasia Makini na hayati Profesa
Leonard Shayo na chama nilichoasisi mwaka
2001 kwa jina la Harakati za Mabadiliko Sahihi
(HAMASA), alichokifuta John Tendwa mwaka
2004, akidai kuwapo vijana wengi nyuma
yangu waliohofiwa kutaka kuleta vurugu
nchini.
Kazi ya kuipitia Katiba ya CHADEMA,
kuichambua na kuifanyia marekebisho
ilinisaidia sana kuongeza uzoefu wa kutunga
katiba za vyama vya siasa na hata vya kijamii
baada ya kupata maarifa zaidi kwa Mbowe.
Hapo ndipo nilipogundua umahiri, uzalendo
na kiu yake katika kuleta mabadiliko ndani ya
chama na nchi.
Uwezo wa kujielimisha kwa kujisomea vitabu
na kupata mafunzo anuai ndani na nje ya
nchi, hata kama hakupata stashahada au
shahada, umemfanya kiongozi huyu awe na
ufahamu mkubwa wa mambo mengi.
Nimesikia watu wakisema Mbowe ni mcheza
disco, labda kwa sababu anamiliki ukumbi wa
starehe wa Billicanas, lakini kusema kweli
miaka yote niliyofanya kazi naye sikuwahi
kuona akicheza au hata akiimba.
Muda mwingi akiwa ofisini kwake alikuwa
akisoma au akiandika makala ambazo zilikuwa
zinatoka kwenye gazeti la Rai wakati huo
likimilikiwa na kina Jenerali Ulimwengu.
Takriban asilimia 80 ya muda wake aliutumia
kwa ajili ya chama; asilimia 15 kwa ajili ya
Jimbo la Hai na biashara zake, na asilimia 5 tu
kuwa na familia – na pengine baada ya miezi
kadhaa kupita!
Bila shaka naamini si baba bora, si kwa
kutoipenda familia yake, bali kwa kukipenda
chama zaidi kuliko familia yake. Nasema
ukweli kwa kuwa Mbowe si malaika, lakini
hapa siongelei udhaifu wake bali uwezo wake,
utumishi wake wa kujenga chama na kiu yake
ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Ni bahati mbaya sana kwamba wanachama
wengi wa CHADEMA hawajui jinsi Freeman
Mbowe alivyojitolea kiakili, kifedha na hata
kiutu kujenga chama imara na chama mbadala
kwa CCM.
Naamini pia ni wanachama wachache zaidi
wanafahamu mchango wangu na kujitolea
kwangu jinsi ya kufufua na kueneza CHADEMA
nikiwa bega kwa bega, si tu na Mbowe, bali na
uongozi wa juu wa chama.
Watanzania wengi walishangaa na hata
kushangilia kufumuka kwa kasi kwa CHADEMA
nchi nzima bila kujua kazi ngumu tuliyofanya.
Nathubutu kusema usione kitu kizuri ukadhani
ni rahisi kukiunda; nyuma yake kuna nguvu
nyingi, akili nyingi, mali nyingi, kujikana
kwingi na kujitolea kwingi.
Wengi wamenufaika sana na matunda ya kazi
yetu CHADEMA bila kujua tulivyoumia na
kulaumiwa tukiwa tunajitolea kupindukia.
Kubuni itikadi ya chama
Niweke wazi kwamba wanachama wengi wa
vyama vya siasa ni mashabiki tu wa vyama
husika lakini wengi hawajui itikadi na falsafa
za vyama vyao.
Ukimuuliza Mwana CCM nini itikadi na falsafa
ya chama chake au ya chama kingine, nina
uhakika wengi hawana habari. Hata maswali ya
wengi wanapouliza nini itikadi yako kisiasa,
kwanza wanakosea kwa kuuliza hivyo kwa kuwa
hulenga kujua chama anachoshabikia mtu.
Anayejibu kwa kutaja jina la chama badala ya
itikadi ya chama anakosea pia. CHADEMA,
CCM, UDP na vingine ni majina ya vyama vya
siasa na si itikadi za vyama husika. Jina la
chama si itikadi!
Wakati tunatafakari na Mbowe tulikubaliana
tuunde itikadi na falsafa ya namna umma
unavyoweza kujiletea mabadiliko. Nikasema
chama kinafanya tu uhamasishaji wa
mabadiliko lakini wenye dhamana, nguvu na
jukumu la kuleta mabadiliko ni umma wa
Watanzania.
Nikatunga Itikadi na Falsafa ya Nguvu ya
Umma (People’s Power). Mbowe aliposoma na
kufanya marekebisho tukakubaliana rasmi
Itikadi na Falsafa ya CHADEMA iwe ni kuamini
Nguvu ya Umma katika kuleta mabadiliko.
Chama pia kikakubaliana na mapendekezo
yetu. Tukaachana kabisa na itikadi za mirengo
ya utajiri wa kiuchumi ambayo watu wengi
wamefungwa kwayo iwe ujamaa, ubepari au
ukomunisti.
Haijalishi ni mfumo gani wa maisha ya kisiasa,
kijamii au kiuchumi chama au nchi inafuata,
lakini mfumo husika lazima uletwe, uridhiwe
na unufaishe umma.
Itikadi na Falsafa ya Nguvu ya Umma ikawa
mwanzoni kabisa mwa katiba, na huenda bado
ipo maana sijajua endapo mabadiliko ya
kiitikadi yalifanyika baadaye.
Hata hivyo, bado nawaona na kuwasikia Wana
CHADEMA kwenye mikutano wakitamka na
kuitikia People’s – Power! Waasisi wa People’s
Power ni Mbowe na mimi!
Nembo ya itikadi na falsafa ya Nguvu ya
Umma
Baada ya chama kuafiki itikadi na falsafa ya
Nguvu ya Umma, tukabadili nembo ya alama
ya vema ya vidole viwili ili iendane na nguvu
ya umma. Tukabuni mkono ulioshiba misuli na
kukunja ngumi uwe ndiyo nembo mpya ya
chama.
Mbowe akatafuta mchoraji mzuri ambaye
alikuja na mkono uliokomaa na kujaa misuli
na ngumi iliyokunjwa mithili ya wale
mabingwa wa masumbwi duniani. Ni kweli
ngumi ilikuwa inatisha!
Lakini ni ukweli pia kwamba hatukulenga
kupigana ngumi na yeyote bali kuonyesha
ishara ya kwamba umma una nguvu ya kuleta
mabadiliko kwa njia za haki, kidemokrasia na
amani.
Tulipowasilisha nembo ya mkono uliokunja
ngumi, CHADEMA wakatishika na kushauri
tuiache nembo husika isije ikaonekana chama
kinataka kupigana ngumi.
Ingawa nembo ya CHADEMA imebaki ileile ya
alama ya vema kwa vidole viwili ikiashiria
ushindi, bado mikutano mingi ya hadhara ya
chama inashereheshwa kwa kukunja ngumi na
kisha kupiga hewani (si mtu yeyote!), kwa
kutamka na kuitikia kwa sauti kuu: People’s –
Power!
Nguvu ya Umma inalenga kuwapa wananchi
fursa na mamlaka ya kufanya mabadiliko
pasipo ghasia, kughilibiwa au kuingiliwa kwa
namna iwayo yoyote ile.
Kwa kufanya hivyo, mikutano mingi ya
CHADEMA imekuwa inafanyika kwa amani nchi
nzima bila mtu kupigwa ngumi isipokuwa
miaka ya hivi karibuni ambapo ama polisi
wamesababisha vurugu kwa kupiga na/au kuua
waandamanaji, au watu wengine wakorofi
kuingilia mikutano ya hadhara na kuleta
vurugu. Naomba Mungu apishe mbali uhalifu
huu.
Wakati wote wa kufanya marekebisho ya
katiba sikuwahi hata siku moja kusikia Mbowe
akitaka kupata cheo chochote ndani ya chama.
Kila tuonanapo mimi ndiye niliyekuwa
nikimshawishi agombee uenyekiti wa taifa.
Jibu alilokuwa akinipa ni kuwa anatumikia
chama, si kupata cheo chochote bali kukijenga
chama ili kiwe imara na kiweze kumudu
mawimbi makali yatakayokikuta katika
kuelekea mabadiliko ya kweli kitaifa.
Alithubutu kusema unamtosha ubunge alionao
na anataka kubakia mwanachama mwadilifu na
mwaminifu kwa chama na taifa.
Nikijua upeo wake wa kuipenda nchi, umahiri
wake katika kuchapa kazi, uzalendo wake na
jinsi anavyojitolea kwa hali, mali na muda,
nilijitahidi kumshawishi na kumfanyia kampeni
agombee uenyekiti wa chama wa taifa kwa
kumrithi Bob Makani.
Hatimaye viongozi na wanachama wa kawaida
wa CHADEMA wakamchagua awe Mwenyekiti
wa chama wa taifa.
Mpaka leo naamini uenyekiti wa chama si
yeye binafsi aliyetaka bali chama kilimwamini
kutokana na kazi aliyofanya na jinsi chama
kilivyoanza kukua kwa kasi kutokana na
mikakati tuliyobuni na kupanga katika maeneo
makuu matatu nilivyoainisha hapa juu.
Aghalabu namjua Mbowe hapendi kufanya
maamuzi binafsi bali anaheshimu sana
maamuzi ya kitaasisi – yaani maamuzi ya
chama, yawe mabaya au mazuri.
Inawezekana jambo hilo linamponza na
huenda ndio udhaifu wake, kwa kuwa hataki
kushawishi chama kifuate mtazamo wake
binafsi hata kama ni mzuri. Anapenda chama
kiamue badala ya kushawishi chama kikubali
hoja zake.
Sina uhakika kama hilo analijua Zitto Kabwe,
maana alitaka apambane na Mbowe katika
nafasi ya uenyekiti wa taifa mwaka 2009,
lakini chama kikamwomba asigombee.
Baada ya Katiba ya CHADEMA na kanuni zake
kuundwa upya, ndipo kazi nyingine nzito ya
kutunga sera mbadala na bora ikaanza kama
ambavyo tutasoma sehemu ya pili ya makala
hii mfululizo.
Nihitimishe kwa kusema kuwa pamoja na
kwamba kuna masuala mengi niliyotofautiana
na Mbowe, hatukuwahi hata siku moja
kugombana. Tulitofautiana bila kuhitilafiana,
kwa kuwa tulikuwa tunaangalia zaidi
yanayotuunganisha kuliko yanayotutofautisha
from TANZANIA DAIMA
 
Hongera kijana wangu ni uchambuzi yakinifu na wenye kuwa elimisha vijana wetu.


Pianiwape pongezi kwa kazi kubwa mliyoifanya na kukifikisha chama hapa kilipo,


'mbowe ni mzalendo wa kweli mwenye nia thabiti na nchi hii"
na nina pendekeza awe mwenyekiti hadi 2019,kwenye uchaguzi wa awamu nyingine dipo atafutwe mmbadala wake.



Naomba wanachadema wote tuwe imara na harakati hizi za ukomboza wa pili.
 
Hongera kijana wangu ni uchambuzi yakinifu na wenye kuwa elimisha vijana wetu.


Pianiwape pongezi kwa kazi kubwa mliyoifanya na kukifikisha chama hapa kilipo,


'mbowe ni mzalendo wa kweli mwenye nia thabiti na nchi hii"
na nina pendekeza awe mwenyekiti hadi 2019,kwenye uchaguzi wa awamu nyingine dipo atafutwe mmbadala wake.



Naomba wanachadema wote tuwe imara na harakati hizi za ukomboza wa pili.

Asante sana kwa kuona umuhimu wa hoja yangu.Chadema kina watu makini ambao kamwe hawatafanya makosa.
 
Wale wanaofuham mchezo wa
Kombolela wataelewa vizuri
Sana kinachoendelea cdm,
Kama hujui nkudokezee kidogo tu, huwa linawekwa kopo katikat ya uga kisha wengine wanajificha, akibaki mmja hajaonekana na akalibutua kopo puuuuuu wote wanarudi kujificha,
 
Wale wanaofuham mchezo wa
Kombolela wataelewa vizuri
Sana kinachoendelea cdm,
Kama hujui nkudokezee kidogo tu, huwa linawekwa kopo katikat ya uga kisha wengine wanajificha, akibaki mmja hajaonekana na akalibutua kopo puuuuuu wote wanarudi kujificha,

Acha kujidanganya!
 
Kwa kazi kubwa wanayofanya viongozi hawa ni wazi Watanzania wanazidi kuwafahamu.

Mungu awape Maisha marefu.
 
WanaJF,

Nimekuwa mfuatiliaji wa wanasiasa mashuhuri Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla.Nimekuwa nikipenda kufanyia uchunguzi wanasiasa hawa walipoanzia harakati zao na mafanikio yao binafsi na ya wananchi wao wanaowaongoza.Nitakuwa nikijadili wanasiasa mbalimbali kwa awamu na leo ningependa nianze kuwajadili wanasiasa mashuhuri Tanzania, Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Kwanini nimewachanganya Pamoja?

Ni ukweli ulio dhahiri kwamba huwezi kuwatenganisha wanasiasa hawa wawili hasa unapojadili mafanikio ndani ya Chadema.Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Wilbroad Slaa ni Katibu mkuu wa Chadema Taifa.Viongozi hawa wawili wamekuwa mhimili mkuu wa siasa za Chadema. Kitu kikubwa walicho nacho viongozi hawa wawili ni Ushirikiano wao.

Kila mmoja ana utaratibu wake katika uongozi lakini ushirikiano wao katika kazi umeifanya Chadema iwe moja na imara kama ilivyo.Ni vigumu kumsikia yeyote kati yao akisema kitu tofauti na mwenzake.Ninaamini hata kama kuna lolote ambalo wanakuwa hawakubaliani wanalimaliza ndani kwa ndani na kamwe humsikii yeyote akiongea tofauti na mwenzake.

Huu ndio uongozi unaotakiwa na hakika ndio siri kubwa iliyofanya Chadema ifike hapa ilipo.Kitu kikubwa kilichowapa credit kubwa viongozi hawa wawili ni pale Mwenyekiti Freeman Mbowe alipoachia nafasi ya kugombea urais kwa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Kwa aina ya viongozi wa Afrika tulio nao ni vigumu sana kuona spirit ya aina hii.

Na endapo kama hili lingefanikiwa basi Tanzania kwa mara ya kwanza ingekuwa kama nchi za Ulaya na Marekani ambapo Rais wa nchi siyo mwenyekiti wa chama tawala.Lakini kingine kikubwa kinachowapa sifa wakuu hawa wawili ni wazi wanaongoza jopo la vijana mbalimbali wasomi na wenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Tunajua kuongoza vijana ni kazi hasa tunaposema vijana bado damu inachemka,lakini vijana hawa wamefundwa na wanawatii viongozi wao mfano John Mnyika,Godbless Lema,Halima Mdee,Tundu Lissu,Ezekiah Wenje,John Heche,Joseph Mbilinyi-Sugu na wengine wengi.


Mafanikio yao

Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamepata mafanikio makubwa katika uongozi wao ambayo hata tukiyataja hatuwezi kuyamaliza kwa leo.Lakini kwa uchache nitataja yale makuu.

1.Kuitoa Chadema kutoka Chama kidogo kabisa hadi kuwa Chama tishio na mbadala wa Chama Tawala
2.Kutoka wabunge 11 katika bunge lililopita hadi kufikia wabunge 48
3.Kuwa Chama kikuu Rasmi cha Upinzani nchini.
4.Kuwa Chama tulivu na kisicho na migogoro ya kipuuzi.
5.Kuwa msemaji na kimbilio la watanzania
6.Kuongoza operesheni mbalimbali nchini zilizoingiza maelfu ya wanachama na kufungua matawi kote nchini
7.Kukuza mapato ya Chadema kwa njia mbalimbali
8.Kujenga ngome yake kuu kwa wasomi hususani katika vyuo vikuu.
9.Kujenga demokrasia ndani ya chama
10.Kufuta kabisa ule usemi kwamba vyama vya upinzani ni vyama vya msimu.

Maadui wa Chadema wanatakaje?

Katika uchunguzi wangu nimegundua kitu kimoja.Kwamba wale wote wasioitakia mema Chadema wanaamini njia pekee ya kukimaliza chama hicho ni kuwatenganisha viongozi hao wawili.Mtu mmoja alinipa mfano jinsi ilivyokuwa rahisi kuisambaratisha NCCR kutokana na tofauti za viongozi wake wakuu.Imekuwa ni rahisi zaidi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko kuivuruga Chadema chini ya Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.

Ni ukweli kwamba Freeman Mbowe mwanasiasa na mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa hapenyeki kirahisi.Kwanza maadui wengi wanapenda kutumia pesa kurubuni watu, sasa Freeman mtamnunua kwa bei gani? Hali kadhalika Dr Wilbroad Slaa msomi aliyebobea na kulingana na falsafa,hulka na itikadi yake amekuwa injini kuu ya chadema kwa nafasi yake ya Katibu mkuu ambapo ndiye mtendaji mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za siku kwa siku za chama.Sasa kwa hali hii na kwa vyovyote vile maadui wa chama hiki wasingependa umoja wa viongozi hawa wawili.


Changamoto zao.

Penye mafanikio hapakosi changamoto.Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya bado viongozi hawa wanatakiwa kuongeza juhudi zaidi katika kufungua matawi ya wanachama hadi kwenye mashina.Si vibaya wakatumia mfumo wa washindani wao wakuu CCM ambao wana utaraibu wa uongozi unaojulikana kama balozi wa nyumba kumi.

Njia hii imeisaidia sana CCM hasa nyakati za uchaguzi.Changamoto nyingine ni kuwa na ofisi kubwa na ya kisasa ya makao makuu inayoendana na hadhi ya chama hicho. Mwisho viongozi hawa wanatakiwa waandae program ya kuwapata wanachama wenye sifa na wanaofaa kugombea nafasi za serikali za mitaa,udiwani na ubunge.Chadema waachane na mfumo wa zima moto wa kupata wagombea.


Mwisho
Kama nilivyoeleza juu viongozi hawa wawili Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa wamekuwa ni nguzo kuu ya chama hiki.Hapa Chadema kilipofikia kipo kwenye hatua ya mwisho yenye uwezekano wa kukamata dola 2015 kwa njia ya kura. Ni wazi hapa ndipo panapohitajika uwajibikaji na ushirikiano wa hali ya juu.Ningelikuwa mwanachama wa Chadema ningehakikisha katika uchaguzi wa ndani wa chama majabali hawa wawili hawaguswi. Wabaki kama walivyo. Wakamilishe kazi waliyoianza ambayo ni kukamata dola.Kisha baada ya hapo historia itakuwa imeandikwa.

WanaJF Karibuni kwa mjadala!
Asante kwa taarifa tuletee undani wa Kikwete pia
 
Kweli wawili ao Mbowe na Slaa wana mafanikio ya kufanana:
1. Wizi wa mali za Chama.
2. Wote ni malaya wasiojieshimu.
3. Hawako tayari kwa hali yoyote ile kuachiangazi zao.
4. Hawako tayari Chama kikaguliwe kisheria.
5. Hawako tayari kusikia ushauri wa mtu yoyote yule juu ya uchaguzi ndani ya Chama...
Hayo ndo mafanikio ya mahadui ao wawili kwa maendeleo ya CDM.
 
Kweli wawili ao Mbowe na Slaa wana mafanikio ya kufanana:
1. Wizi wa mali za Chama.
2. Wote ni malaya wasiojieshimu.
3. Hawako tayari kwa hali yoyote ile kuachiangazi zao.
4. Hawako tayari Chama kikaguliwe kisheria.
5. Hawako tayari kusikia ushauri wa mtu yoyote yule juu ya uchaguzi ndani ya Chama...
Hayo ndo mafanikio ya mahadui ao wawili kwa maendeleo ya CDM.

Huwa hata wapumbavu kama wewe mna haki ya kusomwa kama hivi.Ndiyo Demokrasia hivyo!!
 
Chaguzi ngazi za msingi zinaendelea na baada ya chili zoezi kukamilika Chadema itaimarika sana. Mungu ibariki Chadema
 
Hizi ni pumba tupu kama ni akili hiyo basi mbowe uliyemjua wakati huo si wa sasa kis ha geuka baada ya kuonja utamu ni fisadi mkubwa playboy mkubwa mbinafsi mkubwa kalaga baho
 
Mkuu fmpiganaji, hakika umeandika kwa kirefu ufasaha na rahisi kwa mwanachama yeyote kuelewa. Hii ni analyisis ya hali ya juu. Hakika kwa uliyoandika kuhusu hawa viongozi ni wazi usione vyaelea vimeundwa.

Asante sana.

Tupia na elimu zao basi mkuu
 
Kama wana taka hiki chama kiimarike zaidi wamsamehe Zito ile chama kiondokane na lawama toka kwa wanachama na mashabiki wa upande huo.Yule Zito ana watu wengi sana nyuma yake .
Kumfukuza ni kuleta mgogoro usiokua na maana kwa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi.

Kumrudisha zito itakua ni mbinu nyingine ya kuhuisha chama na kuwaziba mdomo mahasimu wa chama.

Pia uchaguzi wa ndani utakua mgumu kutabirika jambo litakalo vuta hisia ,macho na masikio ya watanzania wengi, na anayeibuka mshindi ni rahisi kukubalika zaidi kwa wananchi.

Kwa sasa uchaguzi ndani ya CCM unakua ndo kama uchaguzi mkuu kutokana na ushindani uliopo kwa wagombea wake.
 
Hata mimi nakipenda sana chama cha chadema Dr na Mbowe wanajitahidi kupiga kazi. Lakini watafakali kwa makini wamrejeshe Zitto kwenye chama na Ikiwezekana wampe uongozi, anaushawishi wasibeze mawazo yetu kwa kuwa hatuna majina makubwa hapa nchini. Tambua kwenye mpira shabika anajua makosa ya mchezaji kuliko mchezaji mwenyewe, wasibeze ushauri huu.
 
Back
Top Bottom