Unayosababu (reasoning) - kipimo cha IQ yako

Unayosababu (reasoning) - kipimo cha IQ yako

Sijaona uhusiano wa IQ na hayo uliyotaja.
Kasome chakula cha Akili kina kitu unaona ...
Uwezo wa mtu kutenda kwa kutumia sababu sahihi .. mfano mtoto akitenda jambo ambalo ametumia akili sana kutoa sababu anahesabiwa kuwa na IQ ya juu. Kufanya mambo makubwa ambayo labda watu wa rika linalokuzidi ndo wanafanya inaonekana una IQ kubwa!
Sasa kwa yaliyotajwa huoni kwamba wahusika wanakuwa na sababu za kitoto wakati wao ni watu wazima?
 
Kila siku utasikia watu wengi wakiongelea kuwa IQ ya watanzania ni ndogo - iko kwenye asilimia 70. Ufafanuzi uko hivi: ni kutokana na matendo ya walio wengi kutotenda kwa sababu sahihi.

ONA HAWA WATU:

1. Siwezi kujenga slop, najipanga nijenge nyumba ya maana (ana miaka zaidi ya 15 anapanga chumba kimoja na sebure)

2. Mwanangu hawezi soma shule za kata (analalamika eti shule wamepandisha gharama na vyuma vimekaza)

3. Siingii kwenye nyumba haijaisha (anaendelea kupanda na anadaiwa kodi miezi 6 nyuma)

4. Siwezi kulima mchicha mjini hapa (ananunua mchicha kila siku)

5. Siwezi kununua gari la hivyo (anapanda bajaji kila siku)

6. Siwezi kulala na mifugo (kuku) ndani ya nyumba (ana bill ya mayai ya mtoto kila mwezi.

ONGEZA NA NYINGINE …

Hicho ndo kipimo cha IQ za watanzania … hawana sababu za msingi kwa yale wanayoyatolea maamuzi. Kama na wewe ni wa hivyo … BADILIKA.
2 haieleweki.
 
Kuna wale wa siwataki single mom lakini amewazalisha wadada zaidi ya mmoja na hajawaoa
 
Kazi ya ualimu ni kazi ya kijinga subiri afungiwe mshaara atatukana kuanzia mkuu wa shule mpaka DEO na kukesha Halmashauri akilia kweli IQ ni nadharia ya kufikirika.
 
Kazi ya ualimu ni kazi ya kijinga subiri afungiwe mshaara atatukana kuanzia mkuu wa shule mpaka DEO na kukesha Halmashauri akilia kweli IQ ni nadharia ya kufikirika.
Yaani ... mnazoongeza zinanifanya niwafikirie watu fulani walioenda kwa afisa wa serikali kuanika mambo yao ya ndani ...
 
Ona hii ...
Mke: Usinibabaishe nina kwetu nitaenda ... na watoto siwezi kuwahacha wateseke ...
Baadaye
Kanitelekeza na watoto miezi tisa sasa ... NINI HIYO!
 
Unachowaza ndicho kinachotokea, ukiwaza kujenga kibanda, utafanikiwa kibanda, ukiwaza bangaloo utafanikisha bangaloo.
 
Unachowaza ndicho kinachotokea, ukiwaza kujenga kibanda, utafanikiwa kibanda, ukiwaza bangaloo utafanikisha bangaloo.
Tangu nimeanza mafunzo ya mazoezi ya akili kuna matokeo chanya nayaona kwenye kuishi kwangu. Uko sawa mkuu.
 
Siwezi kuvaa mitumba kamwe ( ana suti moja ya mchina, shilingi elfu sitini, Kariakoo, kauka ni kuvae).
 
Back
Top Bottom