Unawezaje kutenganisha maslahi ya Muungano na Tanganyika?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,920
Kwa mfano unawezaje kujua sasa serikali inafanya jambo kwa ajili ya Tanganyika na sasa inafanya kwa ajili ya Muungano??

Je, Rasirimali zilizopo Tanganyika ni mali ya Muungano ama ni mali ya Tanganyika. Faida inayopatikana kutokana na Utalii, madini, uuzaji mazao nje, ni mali ya Tanganyika ama ni mali ya Muungano.

Mtoto wa kizanzibari anaposoma kwenye shule zilizoko Tanganyika anahesabika anasoma kwenye shule za Muungano ama za Tanganyika? Ni wapi kisheria na kisiasa unapojua kama hili ni jambo la Tanganyika na hili ni jambo la Muungano?
 
😂😂😂👇👇👇

1637754672913.jpg
 
Hakuna kitu kinaitwa Tanganyika kwa sasa. Hii nchi ilishakufa.

Haitambuliki Umoja wa Mataifa, haitambuliki katika katiba. It is a ghost country.

Labda jaribu kujieleza vizuri.
Nadhani umeshindwa kunielewa kwa kujikita zaidi kwenye kuangalia jina la nchi Tanganyika bila ya kujali kama Muungano haukuua mambo ya Tanganyika bali ulichagua baadhi mambo ya Tanganyika ya kushughulikiwa na Serikali ya Muungano.

Kama Nchi Tanganyika imekufa, Kwa nini nchi Zanzibar ipo? Na kama nchi Tanganyika imeuawa na Muungano ni kwa nini nchi ya Zanzibar haijauawa na Muungano. Kwa hiyo siyo kila jambo la Tanganyika liliingizwa kwenye Muungano, bali mambo machache yanayotajwa kwenye hati ya Muungano.

Kusema kwamba Tanganyika haitambuliki popote duniani ni sawa, lakini si sawa kusema kwamba hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania nayo pia haiitambui Tanganyika. Katiba ya Muungno inapotaja kuyatambua baadhi ya Mambo kuwa ni ya Muungano, moja kwa moja kisheria ndiyo inasema kuwa kuna baadhi ya mambo si ya Muungano ambayo yanapaswa kushughulikiwa na kuwafaidisha watanganyika pekee.

Katiba hiyo ya JMT inapoitaja Zanzibar na Serikali yake, ni kuonesha kwamba kuna serikalil nyingine ambayo si ya Zanzibar wala si ya Muungano. Hata kama Tanganyika ni nchi msukule (Ghost Country) kwa mtazamo wa kawaida, lakini kikatiba Mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano yapo.

Hayo mambo yasiyo ya Kimuungano ni pamoja na Mafuta, utalii, misitu, madini na mengineyo kadhaa ambayo kwa muktadha wa mjadala huu hakuna sababu ya kuyataja. Sasa fedha zinazotakana na mambo hayo yasiyo ya Muungano zinajadiliwa wapi matumizi yake na watanganyika ama kuna Akaunti maalum ya kuweka hela hizo?
 
Kwa mfano unawezaje kujua sasa serikali inafanya jambo kwa ajili ya Tanganyika na sasa inafanya kwa ajili ya Muungano??

Je, Rasirimali zilizopo Tanganyika ni mali ya Muungano ama ni mali ya Tanganyika. Faida inayopatikana kutokana na Utalii, madini, uuzaji mazao nje, ni mali ya Tanganyika ama ni mali ya Muungano.

Mtoto wa kizanzibari anaposoma kwenye shule zilizoko Tanganyika anahesabika anasoma kwenye shule za Muungano ama za Tanganyika? Ni wapi kisheria na kisiasa unapojua kama hili ni jambo la Tanganyika na hili ni jambo la Muungano?
Kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano,inadaiwa mwanzo palikua na vipengele 11 tu Ila Sasa vipo 20+..madini si suala la muungano
 
Madhabahuni kivipi??
Muungano ni wa kulazimishwa na mabeberu (USA na UK),walimuhofia mjamaa prof Babu,waliona atamtoa karume,so wakamtumia Julius kuhakikisha anakichukua kisiwa,muungano ukafanyika Kama dharura jumapili,baada ya mwanasheria wa karume kuambiwa akanyoe ndevu,baada ya kuungana nao tukawa na agenda 'zingine'..miongoni mwazo Kuna padre alizisema 2005/6
 
Nadhani umeshindwa kunielewa kwa kujikita zaidi kwenye kuangalia jina la nchi Tanganyika bila ya kujali kama Muungano haukuua mambo ya Tanganyika bali ulichagua baadhi mambo ya Tanganyika ya kushughulikiwa na Serikali ya Muungano.

Kama Nchi Tanganyika imekufa, Kwa nini nchi Zanzibar ipo? Na kama nchi Tanganyika imeuawa na Muungano ni kwa nini nchi ya Zanzibar haijauawa na Muungano. Kwa hiyo siyo kila jambo la Tanganyika liliingizwa kwenye Muungano, bali mambo machache yanayotajwa kwenye hati ya Muungano.

Kusema kwamba Tanganyika haitambuliki popote duniani ni sawa, lakini si sawa kusema kwamba hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania nayo pia haiitambui Tanganyika. Katiba ya Muungno inapotaja kuyatambua baadhi ya Mambo kuwa ni ya Muungano, moja kwa moja kisheria ndiyo inasema kuwa kuna baadhi ya mambo si Muungano ambayo yanapaswa kushughulikiwa na kuwafaidisha watanganyika pekee.

Katiba hiyo ya JMT inapoitaja Zanzibar na Serikali yake, ni kuonesha kwamba kuna serikalil nyingine ambayo si ya Zanzibar wala si ya Muungano. Hata kama Tanganyika ni serikali msukule (Ghost Country) kwa mtazamo wa kawaida, lakini kikatiba Mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano yapo.

Hayo mambo yasiyo ya Kimuungano ni pamoja na Mafuta, utalii, misitu, madini na mengineyo kadhaa ambayo kwa muktadha wa mjadala huu hakuna sababu ya kuyataja. Sasa fedha zinazotakana na mambo hayo yasiyo ya Muungano zinajadiliwa wapi matumizi yake na watanganyika ama kuna Akaunti maalum ya kuweka hela hizo?
Mkuu, umeibua hoja ambazo wataganyika hawazifikirii. Kuna umuhimu wa kuwa na serikari tatu.
 
Unauliza nini babu!!?..inamaana mapato ya madini hayajulikani yanakopita!?
Yanapitia Hazina ya Serikali ya Muungano, yakitoka hapo yanakwenda kujadiliwa kwenye Bunge la Muungano wakati mapato hayo si mali ya serikali ya Muungano.
 
Mapato ya muungano yanajulikana na yasiyo muungano yanajulikana,ni suala la kujumlisha na kutoa tu
 
Kama kuna kiongozi alilazimishwa kuukubali muungano, basi kiongozi huyo alikuwa dhaifu. Kama tunayaamini sana maandishi ya hao "mabeberu" tusichague ya kuyatumia, tuyakubali yote basi.
Mzee Joseph mihangwa na akina Ali nabwa wameyasema Sana hayo ya muungano Wala si mabeberu
 
Kwa mfano unawezaje kujua sasa serikali inafanya jambo kwa ajili ya Tanganyika na sasa inafanya kwa ajili ya Muungano??

Je, Rasirimali zilizopo Tanganyika ni mali ya Muungano ama ni mali ya Tanganyika. Faida inayopatikana kutokana na Utalii, madini, uuzaji mazao nje, ni mali ya Tanganyika ama ni mali ya Muungano.

Mtoto wa kizanzibari anaposoma kwenye shule zilizoko Tanganyika anahesabika anasoma kwenye shule za Muungano ama za Tanganyika? Ni wapi kisheria na kisiasa unapojua kama hili ni jambo la Tanganyika na hili ni jambo la Muungano?
Tusubiri jibu kwa anaekopa Kwa rehani za Tanganyika na kugawa na Zanzibar
 
Back
Top Bottom