Je, Tanganyika Ilifutwa baada ya Muungano? Ilifutwaje?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,033
3,913
Kuna swali najua watu wanajiuliza na mimi pia najiuliza.

Je Tanganyika IPO lakini haina Serikali yake au Tanganyika Haipo kabisa?

Je Ulipoundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Tanganyika Ilifutwa kabisa?Ilifutwaje?

Naomba kama kuna ambaye ana taarifa za uhakika kabisa maana nikisoma kwenye Katiba naona kama vile Tanganyika haikufutwa lakini in practice kama vile ilifutwa.

Nataka kujua tu ni kiongozi gani ambaye ni mkuu kimaamuzi katika masuala ya Tanganyika Kama Tukimuondoa Rais wa Muungano ambaye anahusika Kote? Je ni Makamu wa Rais? Je ni Waziri Mkuu? Je ni Spika wa Bunge au ni nani?
 
Kuna swali najua watu wanajiuliza na mimi pia najiuliza
Je Tanganyika IPO lakini haina Serikali yake au Tanganyika Haipo kabisa?
Je Ulipoundwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Tanganyika Ilifutwa kabisa?Ilifutwaje?
Naomba kama kuna ambaye ana taarifa za uhakika kabisa maana nikisoma kwenye Katiba naona kama vile Tanganyika haikufutwa lakini in practice kama vile ilifutwa.Nataka kujua tu Ni kiongozi gani ambaye ni mkuu kimaamuzi katika masuala ya Tanganyika Kama Tukimuondoa Rais wa Muungano ambaye anahusika Kote?Je ni Makamu wa Rais?Je ni Waziri Mkuu?Je ni Spika wa Bunge au ni nani?
Tanganyika haipo. Soma Katiba ya JMT (1977)

Ibara ya 1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Ibara ya 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

Kwa kuwa hskuna Tanganyika ila JMT
Ibara ya 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
 
Back
Top Bottom