Unawezaje kutatua jambo hili?

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,138
Ni siku fulani nzuri na tulivu, ikichagizwa na weekend kuingia

Moja kwa moja kwenye mada,

Ni hivi, ukiwa kama mwanaume halafu ukaletewa malalamiko na Dada yako wa damu yaani tumbo moja.

Kuwa hapati huduma muhimu toka kwa mumewe ambaye ni shemeji yako,namaanisha Chakula kizuri,mavazi na vitu vidogo vidogo vingi.

Ukaamua kumshauri Dada yako kwamba atulie/avumilie pengine jamaa anapitia nyakati ngumu kidogo hasa ukizingatia gharama za maisha zimeongezeka

Unaamua kumtetea mwanaume mwenzio huku ukiendelea kutoa msaada kadri ya uwezo wako kwa Dada yako,maana damu ni nzito kuliko maji.

Mwisho wa siku ukagundua jamaa ana mwanamke mwingine, mbaya zaidi wamekuwa wakitumbua pesa ovyo, bila msaada kwa familia yake halisi

Halafu dada yako hajui kinachoendelea, ukaamua kupiga kimya dada yako asijue huku ukimuhimiza azidi kumuelewesha mumewe hali ya hapo kwake.

Je, wanajamvi ni hatua ipi inapaswa ichukuliwe,

Kumbuka Kuna magonjwa, kusambaratika kwa familia na mengine mengi

Kumwambia dada pengine haiwezekani maana wanandoa wanajulikana usije aibika baadaye

Michango yenu ni muhimu.
Screenshot_20220513-121919.jpg
 
Dada ako usimwambie

Yan usithubutu kuwachonganisha na kuwaingilia watu wawili wanaolala uchi pamoja…siku wakipatana sijui utaweka wapi huo uso wako.

Kama unajimudu mwambie huyo shemejio, mwambie dada ako kakupa ABC hizi na wewe nina ushahidi kuna mahali unafanya 123… then ongeeni kuanzia hapo..

Mkipigana mtajiju..
 
Kwanini usimwambie?, Kwanini ukae kimya????... Huwezi mbadilisha shemeji eti Kwa mikwara yako, huwezi ingilia ndoa ya shemejio Kwa kumuwekea Sheria zako, ilhali Ile ni nyumba yake... Sana Sana atabadili njia ya kuchepuka basi, kama ulimkuta lamada open place basi huwezi tena mkuta apo,ataingia Chocho za ndani ndani kbs, huku ukijua umekomesha kuumbe unazd muumiza sister yako.

Dada yako ndiyo anatakiwa kubadilika, dada yako ndiye mwnye maamuzi, kusuka ama kunyoa, kuvumilia ama kuondoka. Ila si kwa ww kumpa mikwara shemeji yako. Mchane ukweli sister yako, na umuulize uamuz wake yeye ni nini na ww pia umpe ushauri namna ya kufanya vile unavyoona wewe, maana ni ndugu yako usimuache ateketee...

Lakini la mwisho, mapenzi upofu,,, mwambie awe makini katika maamuzi yake
 
Changamoto zpo kila mahali, s vyema kumuambia ukweli dada yako maana utakuwa unawagombanisha.

Kama unammudu shemejio bas zungumza nae(kiuanaume na s kimbea mbea), afanye uamuz kama n kumuacha amuache dadayo kuliko kumletea magonjwa.

Na pia kama dadayo afany kaz mtafutie shughuli ya kufanya, hii itamsaidia kwa namna moja ama nyingine.
 
Nakubali
 
Ahsante sana
 
Hachelewi kukuambia “kwanza dada’ko simwelewi hana maajabu kabisa kitandani ndio maana nimeamua kuwa na mchepuko kama vipi mchukue wewe”
 
nimejaribu kupitia nyuzi za humu ila nikagundua kua nyuzi kwa kiingereza ni thread, ila sa itakuwaje

au tumuulize msukule mkuu atupe majibu ya kuridhisha
 
Anayekuhusu hapo ni dada yako, maana unaweza kumwambia shemeji yako kumbe dada ndio mzinguaji, na umesema unatoa pesa shemeji anaenda kuenjoy na mchepuko una uhakika?? Usikute mchepuko ndio unaomuweka shemeji yako mjini.
 
Pesa inatolewa kuwasaidia Dada na wapwa zangu,sijasema natoa pesa ili shemeji aka enjoy na mchepuko
 
Kwanini usimwambie?, Kwanini ukae kimya????... Huwezi mbadilisha shemeji eti Kwa mikwara yako, huwezi ingilia ndoa ya shemejio Kwa kumuwekea Sheria zako, ilhali Ile ni nyumba yake... Sana Sana atabadili njia ya kuchepuka basi, kama ulimkuta lamada open place basi huwezi tena mkuta apo,ataingia Chocho za ndani ndani kbs, huku ukijua umekomesha kuumbe unazd muumiza sister yako.

Dada yako ndiyo anatakiwa kubadilika, dada yako ndiye mwnye maamuzi, kusuka ama kunyoa, kuvumilia ama kuondoka. Ila si kwa ww kumpa mikwara shemeji yako. Mchane ukweli sister yako, na umuulize uamuz wake yeye ni nini na ww pia umpe ushauri namna ya kufanya vile unavyoona wewe, maana ni ndugu yako usimuache ateketee...

Lakini la mwisho, mapenzi upofu,,, mwambie awe makini katika maamuzi yake
😅😅😅 Mapenzi siku hizi yashaisha watu wanatafuta pakutolea stress tu 😅😅
 
Pesa inatolewa kuwasaidia Dada na wapwa zangu,sijasema natoa pesa ili shemeji aka enjoy na mchepuko
Kama dada ako ana kazi au kabiashara aelekeze akili zake kule

asimfatilie huyo dingi wala nini a’mute’ kana kwamba hamna lililotokea huyo dingi haipitu hata mwezi atajirudi tu

Dada anachokosea ni kuonesha haezi ishi bila huyo jamaa na ndo maana linaongeza kukitembeza huko nje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom