SoC01 Unaweza kujiajiri ukiwa bado mwanafunzi kwa kutoa huduma hizi

Stories of Change - 2021 Competition

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,477
2,148
Kujiajiri ni kinyume cha kuajiriwa. Yani mtu kufanya kazi fulani kwalengo la kujipatia kipato, Mtu wa ngazi yeyote ya elimu anaweza kujiajiri mradi tu anaufahamu wa kile anachotaka kukifanya. Kwa hali ya kawaida iliyozoeleka katika akili za wengi ni kuwa wakati wa uanafunzi ni wakati wa utegemezi. Sio jambo baya ikiwa hivyo lakini ni vyema tukafahamu kila mmoja anayo namna yake ya kuishi na namna yake anayokuzwa. Makala hii inalengo la kushirikisha baadhi ya njia ambazo mwanafunzi anaweza kuzitumia kujiajiri na zikamnufaisha kiuchumi angali shule. njia hizo zinaweza kutumika na mtu mwingine pia lakini kwa namna nyingine yenye ubora zaidi, njia hizo ni pamoaja na,

Mosi, Kushiriki tafiti zinazolipa mtandaoni (online paid survey), Makampuni mbalimbali duniani huhitaji watu kwaajili ya kufanya tafiti zao kuhusu masuala mbalimbali kama vile afya, biashara na nyinginezo. mshiriki hutakiwa kukamilisha utafiti kwa kujibu maswali maalumu na mwisho wa utafiti hulipwa kiasi fulani kulingana na makubaliano. Pamoja na hayo baadhi ya makampuni hayalipi kweli hivyo unapaswa kuwa makini kabla ya kuamua kufanya utafiti wowote ule mtandaoni, pia kama wewe ni mwanafunzi nilazima upange ratiba yako vyema ili usiathiri muda wako wa masomo. bBaadhi ya makampuni bora ya utafiti wa mtandaoni ni, GeOpol, Taluna influencer, swagbucks, life point,i-say, You Gov,na Marketagent.

Pili, Programu za uafiliati (affiliate marketing program/revenue share), Hii ni programu ambayo mmlikiwa biashara (merchant) kulipa sehemu ya faida ya bidhaa au huduma kwa mtangazaji wa hudumaau bidhaa(affiliate) kwamfano kama umejiunga na progaram ya duka mtandao la Amazon au Jumia na ukatangaza link ya bidhaa mtu akaibofya na kununua utapata mrabaha (commission) kulingana na makubaliano yaliyowekwa. Baadhi ya makampuni yanayotoa nafasi hizi ni pamoja na 22bet, Amazon, A-libaba, Jumia market, winprincess, premierbet, eBay namengineyo. unaweza kutafuta mengine kwa kutumia mtambo tafutishi wa Google.

Tatu, Andika na uza vitabu umeme mtandaoni (sell E-books) Kama unakipaji cha uandishi huu ni uwanja wako unaweza kuandika vitabu mbalimbali na kuvihariri vizuri kisha kuviuza katika mitandao kama Amazon kindle, Bluu, na lulu. Hata ikiwa huna kipaji cha uandishi unaweza kutafuta vitabu vilivyoandikwa kwa kingereza vinavyohitajika sana na kuvifasiri au kukifanya katika umbo la audio na kuviuza tena mtandaoni.

Nne kuchapa, kuhariri, na kusoma prufu (type,edit, and proofreading) Kama upo katika ngazi ya chuo na unamiliki tarakilishi unaweza kuanza kutoa huduma ya kuchapa na kuhariri kazi mbalimbali za kitaaluma na ukajipatia kipato. Hakikisha unatoa huduma kwa bei nzuri kuliko ile ambayo ingepatikana steshenari.

Tano, Toa huduma ya kusafirisha chakula, vinywaji (delivery service) ikiwa unausafiri unaweza kuifanya hii, lakini unaweza pia kutembea kama umbali sio mrefu sana na ukatoza malipo fulani kulingana na makubaliano yako na mlaji.
Pamoja na hayo unapaswa kupanga ratiba yako vizuri na pia kujiepusha na na biashara za upatu kama Multi level marketing kwani zitakupotezea muda mwingi na mwisho hutambulia chochote
 
ongezea hapo kuna survey app ambazo ukiwa nazo utaweza kuinvest m.b zako kuwa pesa, lkn itakuchukuwa muda mrefu ambapo jinsi unavyozid kufanya survey zakutosha, ndpo unajinyakulia point ambazo baadae zikitimia kiwango walichokiweka uta weza kutoa pesa kupitia namba yako ya sim,,kikubwa uvumilivu tu
 
shukrani mkuu pia usisahau kubofya sehemu ya vote katika posti hii
 
hili la tozo unalizungumziaje?
litazungumzwa kwa makala nyingine lakini nivyema kila mtu afahamu uchumi wa kidigitali ni muhimu sana na unahitaji huduma nafuu ili kila mtu aweze kuzitumia. usisahau kubofya sehemu ya vote katika chapisho hapo juu
 
asante kwa wote mnaoendelea kupiga kura kwaajili ya chapisho hili
 
ongezea hapo kuna survey app ambazo ukiwa nazo utaweza kuinvest m.b zako kuwa pesa, lkn itakuchukuwa muda mrefu ambapo jinsi unavyozid kufanya survey zakutosha, ndpo unajinyakulia point ambazo baadae zikitimia kiwango walichokiweka uta weza kutoa pesa kupitia namba yako ya sim,,kikubwa uvumilivu tu

Mkuu hii inakaaje...
Naomba ufafanuzi kidogo.
 
Cheza na Fiverr, Freelancer na UpWork utumie muda mwingi kujitengenezea profile uko. Baadae utaanza kupata tenda ndogondogo

Kuwa mwandishi na ulipwe. Au anzisha blog
 
Kujiajiri ni kinyume cha kuajiriwa. Yani mtu kufanya kazi fulani kwalengo la kujipatia kipato, Mtu wa ngazi yeyote ya elimu anaweza kujiajiri mradi tu anaufahamu wa kile anachotaka kukifanya. Kwa hali ya kawaida iliyozoeleka katika akili za wengi ni kuwa wakati wa uanafunzi ni wakati wa utegemezi. Sio jambo baya ikiwa hivyo lakini ni vyema tukafahamu kila mmoja anayo namna yake ya kuishi na namna yake anayokuzwa. Makala hii inalengo la kushirikisha baadhi ya njia ambazo mwanafunzi anaweza kuzitumia kujiajiri na zikamnufaisha kiuchumi angali shule. njia hizo zinaweza kutumika na mtu mwingine pia lakini kwa namna nyingine yenye ubora zaidi, njia hizo ni pamoaja na,

Mosi, Kushiriki tafiti zinazolipa mtandaoni (online paid survey), Makampuni mbalimbali duniani huhitaji watu kwaajili ya kufanya tafiti zao kuhusu masuala mbalimbali kama vile afya, biashara na nyinginezo. mshiriki hutakiwa kukamilisha utafiti kwa kujibu maswali maalumu na mwisho wa utafiti hulipwa kiasi fulani kulingana na makubaliano. Pamoja na hayo baadhi ya makampuni hayalipi kweli hivyo unapaswa kuwa makini kabla ya kuamua kufanya utafiti wowote ule mtandaoni, pia kama wewe ni mwanafunzi nilazima upange ratiba yako vyema ili usiathiri muda wako wa masomo. bBaadhi ya makampuni bora ya utafiti wa mtandaoni ni, GeOpol, Taluna influencer, swagbucks, life point,i-say, You Gov,na Marketagent.

Pili, Programu za uafiliati (affiliate marketing program/revenue share), Hii ni programu ambayo mmlikiwa biashara (merchant) kulipa sehemu ya faida ya bidhaa au huduma kwa mtangazaji wa hudumaau bidhaa(affiliate) kwamfano kama umejiunga na progaram ya duka mtandao la Amazon au Jumia na ukatangaza link ya bidhaa mtu akaibofya na kununua utapata mrabaha (commission) kulingana na makubaliano yaliyowekwa. Baadhi ya makampuni yanayotoa nafasi hizi ni pamoja na 22bet, Amazon, A-libaba, Jumia market, winprincess, premierbet, eBay namengineyo. unaweza kutafuta mengine kwa kutumia mtambo tafutishi wa Google.

Tatu, Andika na uza vitabu umeme mtandaoni (sell E-books) Kama unakipaji cha uandishi huu ni uwanja wako unaweza kuandika vitabu mbalimbali na kuvihariri vizuri kisha kuviuza katika mitandao kama Amazon kindle, Bluu, na lulu. Hata ikiwa huna kipaji cha uandishi unaweza kutafuta vitabu vilivyoandikwa kwa kingereza vinavyohitajika sana na kuvifasiri au kukifanya katika umbo la audio na kuviuza tena mtandaoni.

Nne kuchapa, kuhariri, na kusoma prufu (type,edit, and proofreading) Kama upo katika ngazi ya chuo na unamiliki tarakilishi unaweza kuanza kutoa huduma ya kuchapa na kuhariri kazi mbalimbali za kitaaluma na ukajipatia kipato. Hakikisha unatoa huduma kwa bei nzuri kuliko ile ambayo ingepatikana steshenari.

Tano, Toa huduma ya kusafirisha chakula, vinywaji (delivery service) ikiwa unausafiri unaweza kuifanya hii, lakini unaweza pia kutembea kama umbali sio mrefu sana na ukatoza malipo fulani kulingana na makubaliano yako na mlaji.
Pamoja na hayo unapaswa kupanga ratiba yako vizuri na pia kujiepusha na na biashara za upatu kama Multi level marketing kwani zitakupotezea muda mwingi na mwisho hutambulia chochote
kujiajiri huku unasoma wapi na wapi, uliskia wapi mshika mawili moja humponyoka.
 
kupiga kura kwaajili ya chapisho hili bofya palipoandikwa vote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom