Binafsi mimi niliweza kuweka akiba kwa kuanza kutengeneza bajeti yangu ya mwezi. Maana yake ujue kwenye mwezi matumizi yako yote ni kiasi gani na pia kipato chako ni kiasi gani. Baada ya hapo utaona kabisa pesa inayozidi baada ya bajeti yako ya matumizi muhimu kwa mwezi inaenda kwa account kama akiba.
Na kipato kingine chochote mbali na kipato kikuu kinaenda kwenye akiba. Kwa maana nyingine ukiona matumiz yako kwa mwez ni laki tatu, na mshahara wako ni laki 7 unaweza fanya saving ya laki 3, laki tatu matumizi na laki moja for emergency. Na ikitokea ukapata kipato chochote nje ya huo mshahara kiweke kwenye account maana hakipo kwenye bajeti. Usiongeze matumizi yasiyo ya lazima kisa tu umepata ela ambayo haikuwepo kwenye mpango.
Pia banks siku hizi zinaturahisishia kufanya saving sana. Mfano kuna accounts ambazo huwez access pesa zako kwa kutumia ATM cards au mobile banking, kwa hiyo unapohitaji ela zako ni mpaka uende bank. So kama hizo pesa unazihitaji kwa mambo yasiyo muhimu unakuta unaghair kwenda kutoa. Pia kuna huduma ya kuhamisha pesa automatic kutoka kwenye account yako ya mshahara kwenda akaunt yako ya akiba kila mwezi, kwa hiyo mshahara ukitoka unakatwa moja kwa moja akiba yako unabakiwa na ya kutumia tu. Kitu kingine hizo akaunt za kuweka akiba nyingi zina riba, so unaweza kuta akiba yako imeongezeka hata elf 20 saa nyingine, sio kidogo hiyo.
Cha msingi kwenye kuweka akiba kwanza uwe na lengo, sio unaweka tu akiba hata hujui unaiweka ya nn, mwishowe utaila tu. Kingine jua matumiz ya lazima na yale yasio ya lazima yaepuke kwa nguvu zako zote, sisemi watu msile good time, mara moja moja sio mbaya ila isiwe too much good time. Kingine epuka gharama zisizo na msingi, mfano mimi nlikua nalipia king'amuz Tsh 84,000 kwa mwezi ila baada ya kuchuza zaid kwa nn nalipa hivyo niliacha maana nakuta channel nazozitaka labda za movies ni mbili au tatu tu na channel nyingine sina time nazo. So niloacha kulipia hicho kiasi nikajikuata na tsh elf 50 ya ziada. Nikitaka moviea sa hivi na download au naenda nunua, movies library zipo nyingi sana siku hizo.
Huo ni mfano kwangu, naamini kila mmoja wetu ana vitu visivyo vya msingi sana anavilipia wakati kuna mbadala wake kuepuka hizo gharama.