Unawakumbuka nguli hawa wa soka?

Kaka kwa kweli upo juu kuna huyo kwenye red jamaa alikuwa noumer...nadhani pia alikuwepo Juma Amir kama sikosei...David Mwakalebela hakuwa kwenye hicho kikosi kabla ya kwenda yanga? Kipa wao alikuwa anaitwa nani?
Mbona makipa wa Pamba wameshatajwa hapo juu kuwa ni Madata Rubigisa ambaye alifukuzwa baada ya kupokea pesa kutoka kwa Malindi fainali ya Klabu bingwa Tanzania Mwanza nzima ilizizima na Paul Rwechungura ndio alikaa sana kwenye timu na sijui kama ni yeye au vipi Jina lake nililiona kwenye list ya watu waliokufa kwenye meli ya Mv Bukoba.

Pamba ndio Timu Yangu hata leo ikifufuka na mimi nimo ila kwa sasa sifuatilii kabis ligi ya kibongo baada ya Pamba kushuka
 
Madundo Mtambo, Reli ya Morogoro
Rashid Iddi Chama Veteran Yanga, AFC arusha, Coach
Charles Msami - Ushirika Moshi muhahahaha
Ayoub Mzee - Reli Morogoro
Itutu Kigi - CDA , Simba
Rosta Ndunguru- Nyota Nyekundu(Red Star ya mtaa wa Kongo kwa wauza Mitumba... Ile Nyumba yao wajanja nadhani walishaiuza kuna Ghorofa kubwa kama bado waifufue niliipenda hii timu na ilipokufa nikahamia Pamba na Jamhuri ya Pemba kw upande wa Tanzania visiwani
 
Mimi ntamheshimu mtu mmoja anaitwa Hamis Thobias Gaga huyu mtu ni nouma sana pale kati nilikuja kumfananisha na Zinedine Yazid Zidane "Zizzou" japo kipindi kile zidane hangeona ndani mbele ya huyu jamaa.
 
Mbona makipa wa Pamba wameshatajwa hapo juu kuwa ni Madata Rubigisa ambaye alifukuzwa baada ya kupokea pesa kutoka kwa Malindi fainali ya Klabu bingwa Tanzania Mwanza nzima ilizizima na Paul Rwechungura ndio alikaa sana kwenye timu na sijui kama ni yeye au vipi Jina lake nililiona kwenye list ya watu waliokufa kwenye meli ya Mv Bukoba.

Pamba ndio Timu Yangu hata leo ikifufuka na mimi nimo ila kwa sasa sifuatilii kabis ligi ya kibongo baada ya Pamba kushuka
umemchanganya na PETER MHINA mkuu
 
Nawakumbuka...

Haruna Moshi Shaaban Mawela, wengi mlimuita BOBAN, wanaojua kabumbu walimuita FUNDI, vijana waliomkubali ktk soka walimuita MWALIMU, wazee waliomjua akifanya mambo makubwa ktk soka walimuita MTAALAMU, marafiki zake wa karibu tulimuita KICHWA CHA TRENI (GARI MOSHI)/ KICHWA MIMOSHI au MKEMIA

Zamoyoni Mogela "GOLDEN BOY"

Peter Tino "KOCHA MCHEZAJI"

Melkior Mbunda "MTAALAMU/ BABA MCHEZAJI/ WINGA MACHO KUONA"

Mkwasa masta

Wapo wengi sana... Sanaaaaaaa
 
umemchanganya na PETER MHINA mkuu

Kocha Pius Nyamko RIP ndiye alituuza siku ile!Kila mtu alijua Rwechungura atakaa golini lkn from nowhere akampanga mla rushwa mkubwa Juma Mhina!
Dakika ya 86 pasipo na ulazima wowote akamuangusha Victor John Bambo ktk 18 na bila ajizi Mohamed Ally Malaika akafunga
Rwechungura Paul yupo US kimaisha
 
ehee! ngoja na mm nikumbuke enzi yangu; Kichuya,mwanjale,kotei,bukundu,mkude,mzamiru duu nakumbuka kipindi kile wamekutana na Yanga kule zbar,kwenye nusu fainali weeeeee acha bwana enzi hizo rahaa sana
 
CDA Watoto wa Nyumbani
Mkala Maulidi (golini), Yusuf Ambwene (alivunjwaga mguu na Ahmed Amasha), Jumanne Chale, Charles Sulemani, Selemani Abeid (Mkoba), Charles Mngodo, Eric Sagala, Denis Saigulan, Justine Simfukwe (Mawazo Nelson).

Bila ya kumsahau "george best" mutafungwa
 
Miaka ya nyuma hawa jamaa walokuwa balaa kiwanjani wakilisakata gozi la ng'ombe,kwa uchache (waweza ongezea):
Ubwa Makame 'Mzungu'
Leonard William
Juma Mkambi 'Jenerali'
MohamedBakari 'Tall'
Athumani Juma 'Chama' Jogoo
Zamoyon Mogella 'Golden Boy'
Hussein Mwakuruzo
Beya Simba
Jella Mtagwa
Innocent Haule
Celestine 'Sikinde' Mbunga
Hamis Gaga 'Gagarino'
Hussein Marsha
Athumani China
John Makelele 'Ziggy Zaggy'
Juma Pondamali 'Mensah'
Charles Boniface Mkwasa 'Master'
Razak Yusuph 'Careca'
Edibilly Lunyamila
Frank Kassanga Bwalya
Kitwana Manara
Nk nk nk....,ilikuwa hatari tupu.
wanyakyusa bwana,mbn mwongo mwongo sana wewe,hatari yao ilikuwa ni nini na uliwaona wapi hata tv tu hazikuwepo zama zao na wewe ulikuwepo migombani ngopyoro huko,hakika tutaisoma namba daah!
 
Deo mkuki.
Raphael paul.
Mohamed mwameja.
Duwa said.
George masatu.
Hussein masha.
Hamis gaga.
John makelele.
Damian Kimti.
Selestine sikinde mbunga.
Nico njohole.
Twaha hamidu.
Kichochi lemba.
 
Sijaona kiungo kama Hamis Tobias Gagarino hata muwachanganye na wa ligi za mbere huko huyo jamaa alikua anajua mpira..
 
Historia wa mashujaa hawa ilitakiwa kuenziwa na serikali ama shirikisho la soka Tanzania sijui hili nalo tumlaumu FIFA au CAF?
 
Bora TFF irudishe michuano ya Kombe la Taifa. Halafu wahakikishe kila mchezaji akachezee timu ya mkoa wake, tunataka Mwanza heroes, Relu Eagles, Igembensabo, n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom