Nakumbuka mzee, wakt nilikuwa standard three au four pale mpakani primary school, manzese dsm. Baazi ya wachezaji walikuwa hawa:
Beya Simmba
Mao Mkami
Hussein Masha
Paul Rwechungura
Madata Rubigisa
Deo Njoore
Rajabu Risasi
Wengi wa wachezaji walihamia simba ya dar. Je mnamkumbuka yule mtangazaji wa rtd aliyekuwa mwanza, utapenda akitangaza mechi ya pamba na simba au pamba na yanga.
Nimemkumbuka Nteze John Lungu naye alikuwa kwenye hiki kikosi
Kipaji cha ukweli.Hamis Thobias Gagarino (R.I.P)
Kipaji cha ukweli.
Gaga asingeedekeza pombe na msuba angelifika mbali.Jamaa lichana nyavu mara kibao sijui nyavu zenyewe zilikuwa za kuunga unga au kweli kick ilikuwa kali mpaka ikachana
Mkali wa kweli.Masha alikuwa super
kulikua na nyanda mmoja toka kanda ya ziwa KICHOCHI LEMBA[biashara shinyanga] duh alikua na mbwembwe sana langoni,kweli kila zama na enzi zake.
Alikuwa RTC Kagera, akipiga kapelo kama alivyokuwa Manyika Petre wa Yanga.
Musimsahau Hussein Tindwa, aliekufa kiwanjani siku simba ilipocheza na Raccah Rovers ya Nigeria, hapo ilikuwa baada ya Simba kuipiga Mufulira Wandereres goli tano bila, kumbuka mechi ya mwanza iliochezwa uwanja wa taifa simba ilipigwa nne bila, huo ulikuwa ni mwaka 1978 sijui wangapi wanakumbuka hii