Mikoa yenye vipaji vya juu sana katika soka...

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,173
1,582
Katika mikoa ya Tanzania Bara, ni mikoa michache tu, yenye timu zinazoshiriki ligi kuu, mingi ikiwa na timu zaidi ya moja.
"Dar es Salaam ina timu nne, Mbeya, Tanga na Pwani kila mmoja una timu mbili, wakati mikoa ya Tabora, Arusha, Morogoro na Kagera ina timu moja moja."
Ajabu, kuna baadhi ya mikoa inayosifika kwa kutoa vipaji vya soka au iliwahi kuwa na timu tishio katika miaka ya 1980, 1990 na 2000 mwanzoni lakini sasa haina kitu.
Hali hiyo huenda inatokana na matatizo ya ubinafsi wa watu, kutojituma na ikiwezekana viongozi kutokuwa wabunifu au kukosa mapenzi ya dhati na mchezo huo. Fuatilia mikoa hii.
Mwanza:
Mwanza ilipewa jina la Brazil ya Tanzania na hiyo ilitokana na rundo la vipaji ndani ya mkoa huo ambao umewahi kutikisa vilivyo na Klabu ya Pamba au TP Lindanda. Baada ya hapo stori ikawa ni Toto African.
Lakini ajabu Wanamwanza wenyewe wakaongoza kujipiga vita, sasa wameingia katika mikoa isiyokuwa na timu Ligi Kuu Bara, hiki ni kichekesho.
Aibu kubwa kwa Mwanza kutokuwa na timu wakati imezalisha wachezaji kibao mahiri kama akina Ibrahim Magongo, Bakari Malima ¡®Jembe Ulaya¡¯, Deo Mkuki, Fumo Felician, Salum Kabunda ¡®Ninja¡¯, Khalfan Ngassa, Hussein Masha, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Oscar Joshua na Jerry Tegete.
Inawezekana baadhi ya wachezaji hao asili yao si Mwanza, lakini wamejifunzia soka mkoani humo na kuanza kutamba wakiwa huko na timu za huko.
Vipi leo hata timu moja hakuna na hata ukiangalia wakati wa Toto African, kila msimu ilikuwa ikipigana kuepuka kushuka daraja? Hakuna ubishi ni majungu na chuki ndivyo vimechukua nafasi kubwa ya vipaji vya soka mkoani humo.
Dodoma:
Ilikuwa na timu mbili zenye upinzani mkubwa kama Kurugenzi na CDA. Karibu kila timu iliyokuwa inatua mjini humo, ilijua kazi ya timu hizo.
Ingawa Kurugenzi iliendelea kubaki daraja la kwanza kwa kipindi kirefu lakini ilizalisha wachezaji wengi waliocheza katika timu za juu.
Kati ya wachezaji wake nyota ni Iddi Athumani ¡®Pajero¡¯, baba mzazi wa beki wa Yanga, Athumani Iddi ¡®Chuji¡¯ ambaye pia alichipukia mkoani hapo akicheza katika timu ya Polisi Dodoma.
Sasa hakuna timu ya ligi kuu, lakini karibu kila kitu kuhusiana na soka kimedorora, Dodoma umekuwa mji wa bunge tu, dalili zinazoonyesha wananchi wake kama hawana habari tena na mpira au wanaupenda lakini chama chao cha soka kimelala usingizi wa pono.
Ruvuma:
Achana na uimara wa Majimaji tu enzi hizo, lakini angalia wachezaji kibao waliozalishwa kutoka katika mkoa huo bila ya kujali ni wenyeji wa wapi.
Wengi watamkumbuka Steven Mapunda ¡®Garincha¡¯ lakini kulikuwa na rundo la wachezaji kama Peter Mhina, Amri Ayoub ¡®Beki Mstaarabu¡¯, Celestine Sikinde Mbunga na kaka yake, Emmanuel Mbunga, Isihaka Majaliwa, Mohammed Mkandinga, kiungo wa ukweli Octavian Mrope ¡®Oko¡¯ na wengine wengi.
Ruvuma ni kati ya mikoa michache ambayo imewahi kutoa bingwa katika Ligi Kuu ya Muungano, kazi hiyo ilifanywa na Majimaji.
Lakini leo haina timu Ligi Kuu Bara na hata kama Majimaji ikipanda imekuwa ikisuasua na mambo mengi ni ya kubahatisha. Hakuna viongozi wenye uchungu? Au hakuna kiongozi mwenye mipango kama ile ya Lawrence Gama wakati wa enzi zake? Hii ni aibu!
Tabora:
Kwa Tabora, sifa ya Milambo inajulikana, ni mkoa wa soka hasa. Kweli sasa kuna timu ya ligi kuu ya Rhino, lakini hadi kwa msaada wa jeshi ndiyo timu imepatikana. Kumbuka enzi za Milambo au timu imara ya mkoa ya Mashujaa wa Unyanyembe.
Huenda kwa nguvu ya wananchi kama wanapenda soka, basi timu ya jeshi isingekuwa ya pili kwao kushiriki ligi kuu. Tabora ni kati ya mikoa inayoongoza kwa vipaji vya soka, angalia wachezaji hawa wa enzi hizo na baadhi wanaoendelea kucheza.
Quresh Ufunguo, Ally Manyanya, Mikidadi Jumanne, Idd ¡®Mnyamwezi¡¯, Mrisho, Ally na Haruna Moshi ¡®Boban¡¯, Ahmed Mwinyimkuu, Said Mwamba ¡®Kizota¡¯, Athumani Shabani ¡®Tippo¡¯, Abubakari Kanyoro, Seif Juma, Ramadhani Hamis ¡®Mvulana¡¯, Mohammed Banka na wengine kibao.
Shinyanga:
Anzia timu ya Mwadui, timu iliyokuwa inamiliki ndege na ndiyo pekee Tanzania kuwahi kufanya hivyo. Baadaye RTC Shinyanga kabla ya kuitwa Biashara na baadaye Shinyanga Shooting.
Shinyanga ilikuwa na wachezaji kadhaa mahiri kama Michael Paul ¡®Nylon¡¯ ambaye baadaye alitikisa Simba, Paul John Masanja aliyetua Yanga na kuongoza ukuta mgumu na Mwinyimvua Komba ¡®Masolwa¡¯ aliyegoma mara kibao kujiunga na timu hizo kongwe akisisitiza anataka kubaki kwao.
Wapo wengine wengi kama Abdallah Magubika aliyetua Yanga baadaye, Alfred Kategile ¡®Kate¡¯ aliyekwenda Simba na Steven Nyenge ambaye pia aliwahi kuichezea Simba.
Bado kuna Nteze John Lungu aliyetokea Kigoma kama ilivyo kwa Edibily Lunyamila, lakini wakasoma na kukulia Shinyanga huku vipaji vyao vikianza kuonekana ndani ya mji huo.
Nteze hakuwahi kucheza ligi kuu akiwa Shinyanga, badala yake alisomeshwa na soka, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita alilipiwa karo na timu ya Halmashauri ya Mji iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, baada ya kumaliza shule, akatua Pamba. Lunyamila akaenda zake Yanga.
Angalia sasa, ligi kuu imekuwa ndoto kwa zaidi ya miaka kumi huku viongozi wakiendelea kuwa asilimia kubwa ni walewale na maneno kibao, vitendo hakuna.
Kigoma:
Kwa mkoa huu ni aibu nyingine kusema hauna timu ya ligi kuu, ndiyo unaotikisa kwa vipaji katika mchezo wa soka. Wengi wanalazimika kutoka na kwenda kucheza nje ya mkoa kwa kuwa viongozi wa chama cha soka na wale wa klabu ni watu wa maneno tu.
Achana na asili, kama utasema wachezaji wa soka waliotokea Kigoma, basi inaweza kuwa asilimia 35 ya wote wanaocheza soka nchini.
Wachache ni hawa hapa ambao ni Said Sued ¡®Scud¡¯, Juma Kaseja, Selemani Matola, Said Maulid ¡®SMG¡¯, Alphonce Modest, Hemed Ally ¡®Matobango¡¯, Beya Simba, Hamza Maneno, Nassor Idd ¡®Cheche¡¯, Athumani Bilal ¡®Bilo¡¯, Dadi Fares, Mavumbi Omary, Abeid Mziba, Makumbi Juma ¡®Bongabonga¡¯ (nimechoka kutaja).
Kwa kifupi wapo wengi sana, lakini baada ya Reli na RTC Kigoma ikafuatia Mmbanga, baada ya hapo ni majanga na hadithi ya mkoa wenye vipaji imebaki palepale na ligi kuu wanaendelea kuisikia kwenye bomba au kuiangalia kwenye ¡®kideo¡¯.
Mtwara:
Moja ya mikoa yenye vipaji vya juu sana katika soka ni Mtwara, hilo halina ubishi. Lakini ndiyo mkoa ambao umedorora kupita kiasi kisoka.
Pamoja na umaarufu wa kulima korosho lakini wenyeji wake wanapenda sana soka, bahati mbaya hamasa yao inaangushwa na viongozi wao ambao haijulikani wanafanya kitu gani.
Wachezaji kama mshambuliaji Mohammed Hussein ¡®Mmachinga¡¯ aliyeng¡¯ara Yanga, Simba na Taifa Stars au mshambuliaji mwingine hatari, Idefonce Amlima, wote ni mali ya Mtwara.
Kwa vijana wapo wengine, mfano Nizar Khalfan ni kati ya Watanzania wachache waliocheza ligi kubwa za soka duniani. Kacheza Kuwait lakini akapaa hadi Marekani, mdogo wake Razak Khalfan pia ni jibu kwamba Mtwara kuna vipaji.
Ajabu, tangu Bandari Mtwara ilipotelemka daraja mwishoni mwa miaka ya 1990 na kutamba kidogo baadaye mwanzoni mwa miaka ya 2000, hadi sasa ¡®kwishney¡¯.
Mara:
Huenda kuna wengi hawakukulia mjini Musoma au katika sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mara, lakini hakuna anayeweza kusema Mkoa wa Mara hauna vipaji vya soka.
Mshambuliaji wa zamani wa Pamba na Simba, Bhita John Musiba, kiungo mahiri enzi hizo kama Nico Bambaga, aliyekipiga Pamba, Simba, Yanga na Malinzi ya Zanzibar, wote asili yao ni mkoani humo.
Wengine ni Athumani Jumapili ¡®Chama¡¯, Ramadhani Magoye, Dhikiri Mchumila, Mussa Janja na Leonald Juma. Wapo wengi sana ambao wametokea Mara na walikuwa wachezaji nyota, lakini hakuna kitu kabisa na mara nyingi timu za mkoa huo zimekuwa zikipambana na kuishia daraja la kwanza.
Hadi sasa, Ligi Kuu Bara ni kama Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Mkoa wa Mara, hakuna timu yenye ndoto ya kugusa katika hatua hiyo, viongozi wa soka wapo, maisha yanaendelea.
Kilimanjaro:
Unaikumbuka Ushirika ya Moshi? Ni moja ya timu zilizokuwa zinacheza soka la ¡®Kizungu¡¯ utafikiri zinavyocheza sasa baadhi ya timu kubwa barani Ulaya.
Simba, Yanga na timu nyingine kubwa zilikuwa zikihaha zinapokutana na Ushirika bila kujali ni kwao Moshi au nje ya hapo. Jamaa walikuwa wanapiga soka tu, tena la uhakika.
Wachezaji kama Wema Juma, Abuu Juma, Willy Martin au kipa Ofen Martin ni kati ya vizazi vya mwanzo vya Ushirika, lakini sasa mchezo wa soka unaonekana hauna nafasi tena mkoani humo.
Sifa ya Kilimanjaro ni biashara, soka ni biashara pia, huenda viongozi wa soka mkoani humo hawalijui hilo na wamesahau kazi nzuri ya Ushirika enzi hizo.
 

rubaman

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
4,977
3,067
Great post. Lakini sifa zingeenda zaidi kwa mikoa bila kujali asili ya makabila ya hao wachezaji. Naona kuna sehemu umeorodhesha asili ya makabila mf. kina Lunyamila, Nteze. Anyway, kwa kumbukumbu zangu nadhani mikoa iliyozalisha wachezaji wengi waliowahi kutesa ligi kuu Tanzania Bara bila kujali asili ya makabila ya wachezaji ni Mbeya, Mwanza, Tanga, Ruvuma inasikitisha kuona hakuna timu (except Tanga & Mbeya) zinazowakilisha hiyo mikoa katika ligi kuu ya Tanzania Bara. Timu za hiyo mikoa zilikuwa zinatoa ushindani katika medani ya soka na kama ulivyosema makombe makubwa yameshatua katika hiyo mikoa pia timu zimeshaiwakilisha mikoa yao katika Ligi kuu ya Muungano hata katika klabu bingwa Afrika hasa Pamba imeshashiriki, sijui kama Tukuyu stars na Majimaji kama ziliwahi kushiriki. Historia inaonyesha Tukuyu stars ni timu pekee iliyowahi kupanda daraja la kwanza na kuchukuwa kombe katika msimu huo huo kama sikosei ilikuwa 1986.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom