Unaujua Mtori?

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Inasemekana mtori una husika sana katika kutengeneza
afya yako na kukuwezesha kumudu vyema maisha ya "ndoa".

Nime jifunza kuutengeneza,ningependa ujue pia na ujaribu mara moja moja.

VIPIMO

Ndizi mbichi 10
Nyama kilo 1
Nazi ya kopo 1
Chumvi Kijiko 1 cha chakula
Ndimu 1
Bizari ya manjano Kijiko 1 cha chai
Pili pili mbichi 3
Nyanya (tomatoes 2
Kitunguu maji 1
Thomu na Tangawizi ya kusaga Kijiko 1 cha chakula

.NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
2. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
3. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
4. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
5. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
6. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
7. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
8. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
9. Weka pembeni zipoe.
10. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

Karibuni.
 
Ila kuwa mwangalifu,
Utapata kitambi afu pafomensi ishuke zaidi

Asante kwa mapishi, mie nimezoea kupika mtori wa kienyeji
 
Ila kuwa mwangalifu,
Utapata kitambi afu pafomensi ishuke zaidi

Asante kwa mapishi, mie nimezoea kupika mtori wa kienyeji

Yooote hayo mwishoni una fanya + mazoezi.
Lakini pia haukuli mtori kila siku,..........
babu zetu walikua wana kula nyama mbichi,leo hii tunaambiwa nyama nyekundu
zina madhara,.....kwao hazi kuwadhuru pamoja na kwamba walikua wana kula mbichi,
HAWAKUWA WANAKULA NYAMA KILA SIKU......AU KILA WIKI.

Siku hizi nyama ikikosekana nyumbani inaonekana wewe masikini,.....mtori ni sawa pia,...
HUTAKIWI KULA KILA SIKU.

Huo wa kienyeji una pikwa vipi?
 
Ila kuwa mwangalifu,
Utapata kitambi afu pafomensi ishuke zaidi

Asante kwa mapishi, mie nimezoea kupika mtori wa kienyeji

Mimi pia tena wa kule kwetu mindizini..

@Speaker, leo una appetite kweli..naona uliposikia mtori umekimbia gengeni, angalia usichane bwana!! Thanx kwa recipe
 
Mimi pia tena wa kule kwetu mindizini..

@Speaker, leo una appetite kweli..naona uliposikia mtori umekimbia gengeni, angalia usichane bwana!! Thanx kwa recipe

We ndo ume nikumbusha bana,....ila kazi ya jioni hiyo lazima niukule leo.
Raha ya mtori uwe wa motoooooooooo.
 
Mkuu umenisababishia njaa!

Ohoooo,mda wa lunch lakini huu bana.
Au ulitaka ku-skip chakula?
Sio vizuri wahi mapemaaaaa,...

DSC00852.JPG

Ila mtori mzuri ni wa nyumbani kwako sio wa magengeni au hotelini
Na ukule jioni au asubuhi.
 
Kwa dar kama ni mchana lazima uvue na shati.
ila mtamu...

Ndo maana nikasema inapendeza ukiwa home,....
asubuhi sana au jioni,....raha mpaka kisogoni.

Hata kama ulikuwa mvivu mechini lazima damu ichemke siku hiyo.
 
Ohoooo,mda wa lunch lakini huu bana.
Au ulitaka ku-skip chakula?
Sio vizuri wahi mapemaaaaa,...

View attachment 48122

Ila mtori mzuri ni wa nyumbani kwako sio wa magengeni au hotelini
Na ukule jioni au asubuhi.
Yaani huu uzi wako umenichanganya kabisa! Maana huku nilipo sioni namna ya kupata mtori mchana huu, na njaa ndo inazidi lkn kila nikiwaza nile nini nasikia tu sauti za ndani; Mtori! Mtori! Mtori...!!! Yaani ni noma mkuu.
 
Pole sana bana,jitahidi ukamate mtori saaaafi usiku.
Nimeona ume quote ugali wangu nikajua umeupenda haha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom