Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

16 units ac mpk asbhi non stop
 
Unalipau shilingi ngapi kwa mwezi. Km ni chini ya shs 172,000 ni mwongo
Yaani anatumia 16 Unt kwasiku
Sasa kwa Hesabu za 1000 = 2.8 Unt
yaani anatumia 5700+
sawa 171428 Kwamwezi
Aisee
Mm natumia 0.6 Unt kwa siku niwe mkweli
na Kunasiku Hata 0.5 Sifikishi
 
Nalipa 200,000 umeme kwa mwezi sawa na units kama 550 hivi. Kwa siku average ni units kama 18 hivi.
-Nawasha AC full time chumbani
-Nina friji kubwa sebuleni na Dogo chumbani
-Nina washing mashines
-Nina Air matress
-Music systems
-Nina appliance nyinginezo
 
NI kama.unatumia umeme mwingi sana kwa mwezi
Check wattage ya hizo appiliances unazotumia
Ac full time chumban ?😁😁😁😁!! We hutoki humo chumbani?
 
NI kama.unatumia umeme mwingi sana kwa mwezi
Check wattage ya hizo appiliances unazotumia
Ac full time chumban ?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]!! We hutoki humo chumbani?
We mtu muongo mwenye kujikweza huwezi kumuelewa kweli?
 
Unatumia unit ngapi za LUKU kwa siku?

Wajemeni, siku hizi naona kama mita ya umeme inakimbia. Hivi kwa wastani yuniti ngapi za LUKU hutumika kwa nyumba ya kawaida tu?
Sijali sana "units" lakini najua nanunua umeme wa 60,000 unakaa kama wiki 3 hivi
 
Acha maneno yako, nina vitu hivyo ulivyotaja lakini haifiki hiuo hela.
 
nilikua nalalamika nimesoma comment za watu nimeona kumbe mimi umeme wangu uko poa...
mimi nna wastani wa matumizi ya unit 2.5-2.9 kwa siku.....
Nna bulb kama kumi nyumba nzima, fridge masaa 24, natumia jug kuchemsha maji mara kadhaa kadhaa na tv laptops nk kama kawaida na nina nikaona kama umeme unaenda sio poa
 
Matumizi ya umeme inategemea na vifaa vilivyopo majumbani na frequency usage yake mfano washing mashine uwezi tumia kila siku , taa za kisasa hizi ni nzuri ila na matumizi yanaongezeka , vifaa vya jikoni vya umeme vinasaidia kupunguza mda ila inabidi upate vipya sio mtumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…