leroy
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 1,590
- 2,141
- Usiharakishe kuingia kwenye mahusiano mpaka utakapokutana na mtu sahihi ambaye atakupenda bila masharti.
- Jizawadie, pata mtoko wako mwenyewe, na ujijali. Huna haja ya kuwa kwenye mahusiano ili kufurahia maisha yako.
- Jambo baya zaidi maishani si kuwa peke yako, bali ni kuishia kuwa na mwenzi asiyekufaa. Chagua mtu atakayekamilisha maisha yako.
- Chagua kuoa mwenzi ambaye ni kama teammate sio soulmate. Upendo pekee hautoshi kwa mahusiano ya muda mrefu na yenye kujitolea.
- Jenga uhusiano imara na mwenzi wako kabla ya kuamua kuoana.
- Usichumbie mtu ikiwa maisha yako hayaeleweki. Jenga kwanza uwezo wako wa kimwili, kiakili, na kifedha.
- Usioe mtu wa umri wako. Tafuta mtu mwenye uzoefu wa maisha zaidi yako.
- Jifunze jinsi ya kukabiliana na hisia zako na kupona majeraha ya utotoni kabla ya kuyafanya maisha ya mtu kuwa mabaya.
- Wekeza katika mavazi mazuri na usipuuze muonekano wako kwa sababu unavutia watu wa kiwango chako.
- Chumbiana na vunjika moyo. Utafahamu jinsi ya kukabiliana na hasara na kutambua watu sahihi.
- Ikiwa uko kwenye miaka ya 20, hama kutoka kwa wazazi wako. Utafahamu jinsi ya kuwa huru na kujisikia vizuri peke yako.
- Kujipenda mwenyewe ni jambo bora zaidi. Jipende na kujithamini kwa sababu hakuna mtu atakayekupenda kama wewe unavyojipenda.
- Ingia kwenye mahusiano ili kutimiza maslahi yako binafsi, sio kwa sababu ya shinikizo la jamii.
- Kuwa single haimaanishi kuwa mpweke. Take your time mpaka ujisikie tayari kuwa na mtu.
- Jipe nafasi na ufanye kitu kizuri kwako. Kuwa na furaha kwanza kabla ya kujitoa kwa mtu yeyote.